Nisome vipi ili nifaulu vizuri mchepuo wa PCB?

Nisome vipi ili nifaulu vizuri mchepuo wa PCB?

Usome vp kvp??? kusoma hakuna njia ...we soma sanaa....iyo smartphone pia ungeiuza tu ela ukanunulie ata john bird uanze kusoma
 
Mdogo wangu tumia simu yako kutafuta material..humu jf wengi washamaliza secondary...tafuta wenzio uunde magroup ya discussion,discussion za humu if zitakuchanganya
 
Habari wakuu,

Naomba ushauri wenu, nasoma PCB shule iliyopo Zanzibar hivyo naomba ushauri jinsi ya kusoma na kufaulu vema.

Nina ndoto za kusoma MD Muhimbili na najua competition ni kubwa sana na masom ni heavy hivyo nawaombeni ushauri plz

Kama upo serious kweli fanya yafuatayo utapasua na utakuja kunikumbuka mkuu
1. Ingia google utafute syslabus za hayo masomo kwa form five na six hapa Tanzania zinaelekeza mwanafunzi asome kitu gani
Unaweza ukachek katika link ifuatayo syslabus ya hayo masomo ya PCB
A-Levels – ElimuTanzania
2. Hakikisha kila topic na kipengele chake unasoma na kukielewa na uzur mmoja sikuhizi katika google material ni mengi sana na yapo ya kila aina yanayoweza kumwezesha mtu kusoma kitu na kukielewa vizuri zaidi. Pia kitu kama hujakielewa gooogle hata picha zipo utakisoma na kuelewa vzr. Ukishindwa tupia jamii foramu wajanja wapo wengi watukuelewesha
3. Pia vitabu soma sana maana vinongeza uelewa ila soma kwa kuelewa concept
4. Ingia google tafuta past paper za miaka ya nyuma zipo nyingi ujipime ulichosoma kipo?
Form Six Exams (ACSEE) – Maktaba
5. Kwa sababu PCB kuna practical Nenda tution jifunze namna ya kuafanya practical. kama upo dar nenda mwenge Mapambano karibu na kituo cha ITV Tuition
Mkuu sikuhiz kupasua A-levael mbona ni rahis kuliko zamani.Material sasa yapo kibao
 
Piga shule wasikukatishe tamaa. Cha msingi jijue we ni mwanafunzi wa masomo ambayo ni very serious very technical.
Tumia muda mwingi kwenye kusoma tena kusoma kwa faida.
Kukesha si lazima unaweza kudevote muda wa mchana usiku unapumzika utafaulu hakuna kigumu chini ya jua.
Ila Angalizo kuwa makini na Physics na Bios
 
Invest Sana kwenye tutition zinazoeleweka...make sure kabla hujaingia form six... Topic zote za A-level usha maliza. Form six kazi yako iwe kusoma na kupiga ma paper tuuu. Karibu Muhimbili, Karibu Dar!
 
Back
Top Bottom