Muombe Mungu kwanza akupe ushauri mzuri. Kama umemuomba basi yawezekana ni kupitia hii thread waweza kupata ushauri mzuri ingawa Shetani anaweza kujipenyeza pia. Nakushauri kuwa;
1. Sio lazima ufundishe, yawezekana Mungu hajakupangia hilo na wewe umezuia blessings nyingi kutoka kwake kwa kung'ang'ania kufundisha.
2. Subiri nafasi zikitoka za kufundisha hapo IFM utakubaliwa
3. Kama huna kazi, nenda kaipeleke CV yako Deloitte, KPMG, PWC au E&Y lazima watakuita na kama huna uzoefu mkubwa wa kazi kubwa, accept kuanza ktk level ya chini then after time utakuwa na experience itakayokupa 'kiburi' cha kubargain kwenye blue-chip companies. Waweza pia kuipeleka kwenye mabenki watakuchukua. Belittle yourself ili baada ya muda ulie kivulini.