Nishaurini katika hili ''kansa ya ziwa''

kwanza pole
pili hujaeleza kwa nn zoez la mionzi lilishindikana
tatu maamuzi ya nn cha kumfanyia yanategemea na clinical and histological staging.
 
mkuu pole sana,

kama alikatwa na bado anatakiwa kupewa mionzi inabidi ufanye upesi kapambane pale pale ocean road mpaka kieleweke, ukiendelea kukaa na kusuburi itazidi kusamba mbali na utakua too late..

kila la kheri mkuu
 
Jamani mama yangu anasumbuliwa na tatizo la kansa ya ziwa tangu mwaka jana, amepata matibabu ya awali kwa kukatwa ziwa pale hindu mandal hospital dsm na baadae akapelekwa ocean road kwa malengo ya kuanza mionzi. Japokua zoezi hilo halikufanikiwa mpaka sasa hivi, hali yake sio nzuri kwakweli nawaombeni msaada wenu wa hali na mali ili niweze kufahamu naanzia wapi maana nashindwa hata cha kufanya ukizingatia mimi ndiye tegemeo lake

1. Je huduma hiyo ya mionzi hulipiwa pale ocean road au???
2. Nilihangaika walau nikapata bima ya afya nhif je itaweza kunisaidia
naombeni msaada wenu kimawazo walau nifunguke maana sielewi hata pa kuanzia na mama yangu bado anapata shida sana yaani amekua mtu wa kulala tu hata uwezo wa kutembea hana mpaka wakati huu

natanguliza shukurani kwa msaada wako,
Jitahidi upate bima ya afya itakuwa msaada kwako sana.Nimeuguza mgonjwa wa kansa bima ilitusaidia sana. Vipimo kwaajili ya matibabu ni vingi ukiwa na bima inagharamia vyote..
Uende hapo Ocean mkaonane na dr kama mlivyoagizwa.Usiogope wala usihofu kansa ya ziwa ikitibiwa mapema atapona.
 
Pole sana shangazi yangu alikatwa ziwa miezi labda m4 au5 iliyopita pale appolo hosptal ipo mtaa wa libya na mshihiri nenda kwanza kaonane na dr wa pale umsikilize
 
kwanza pole
pili hujaeleza kwa nn zoez la mionzi lilishindikana
tatu maamuzi ya nn cha kumfanyia yanategemea na clinical and histological staging.

Mionzi ilishindikana coz mashine ziliharibika, nashukuru mungu kwa sasa zimeanza kufanya kazi tena ila napenda kufahamu kama huduma hizo hulipiwa na endapo bima ya NHIF (blue kama sijakosea) huweza kusaidia.
 
Pole sana, jitahidi sana uwahi hospitali,
Usikae naye nyumbani muwahishe tu hosp. MziziMkavu Assalamu Alaikum,
Heshima sana kwako mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Mionzi ilishindikana coz mashine ziliharibika, nashukuru mungu kwa sasa zimeanza kufanya kazi tena ila napenda kufahamu kama huduma hizo hulipiwa na endapo bima ya NHIF (blue kama sijakosea) huweza kusaidia.
pole mkuu
kuhusu bima kwa kweli ninavofahamu huduma zinatofautiana na aina ya bima uliyokata.MFANO bima ya laki 1 sidhan kama itacover gharama za surgery ya milioni 8 but all in all itapunguza gharama.
 
Pole sana mamaangu,mungu Ndo muweza wa yoote,keep it up god z great,mama atapona bana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom