Jamani mama yangu anasumbuliwa na tatizo la kansa ya ziwa tangu mwaka jana, amepata matibabu ya awali kwa kukatwa ziwa pale hindu mandal hospital dsm na baadae akapelekwa ocean road kwa malengo ya kuanza mionzi. Japokua zoezi hilo halikufanikiwa mpaka sasa hivi, hali yake sio nzuri kwakweli nawaombeni msaada wenu wa hali na mali ili niweze kufahamu naanzia wapi maana nashindwa hata cha kufanya ukizingatia mimi ndiye tegemeo lake
1. Je huduma hiyo ya mionzi hulipiwa pale ocean road au???
2. Nilihangaika walau nikapata bima ya afya nhif je itaweza kunisaidia
naombeni msaada wenu kimawazo walau nifunguke maana sielewi hata pa kuanzia na mama yangu bado anapata shida sana yaani amekua mtu wa kulala tu hata uwezo wa kutembea hana mpaka wakati huu
natanguliza shukurani kwa msaada wako,