NISHAURIN JAMAN:-Kwa mapenz haya nitapelekwa jela.

NISHAURIN JAMAN:-Kwa mapenz haya nitapelekwa jela.

huyo anatishia mtu mzima nyau!!!!! We maisha yalivyo matamu eti anywe sumu akuache we unagegeda mwingine.........acha masikhara kifo cyo mchezo halafu eti mtu anataka kujiua mpaka rafiki yake anamkuta na kumnyang'anya sumu hivi inaingia akilini kweli???? Anayetaka kujiua huwa asemi bwana kimya kimya tu unackia msiba, ila uamuzi ni juu yako wa kumrudia ama la!!!!!!
 
Angalia na ufikiri mara 2 maana hawa watu wana sanaaa za hatari, Binafsi kwa maelezo hayo hiyo ni sanaa. Hajajua tu hiyo ni booonge la script.
 
Uwe na huruma. Kumbuka huyo binti ulimpenda na yeye alikupenda kwa bahati mbaya yeye alikupenda zaidi. Hebu rudi nyuma na umpe one more chance. Unajua ukipendwa kiasi hiki hebu kua na shukrani , mbona sababu zako sio nzito kiasi ushindwe kurudiana na mwenzio . Hebu jaribu kukutana na watu walioumia hata hawajiwezi mpaka sasa. Mpe nafasi mdada wa watu kwani amekukosea nini mbona ameweza kujirudi na aliporudi hukumpa nafasi bali ulimuumiza tu na unamuenjoy , sikuelewi eti uliitwa hospt na hukwenda kweli wewe una roho ngumu unaweza kuua . Unajua mtu ukijua kua unapendwa sijui kwanini hupenda kumuumiza anaekupenda. Hivi ni kweli ulimpenda au ulikua unacheza na feeling zake tu. Kaa chini rudi ndani ya moyo wako na ujiulize ungekua wewe ndio unahangaika kiasi hicho ungependa huyo unaemuhangaikia afanye nini. Jiulize tena je ulimpenda kweli toka moyoni mwako, Je ungekua wewe usingependa kupewa nafasi tena. Mwisho mshukuru Mungu.
 
Habar wana MMU!
Kipind cha nyuma kidogo nshawah kuomba ushaur hapa jukwaan kuhusu x-girl friend wangu, mlinishaur vzr sana na ushaur wenu niliutumia.

Short review
Nikuwa na msichana ambae tulidumu kwa mda.Ilitokea akaambiwa nina uhusiano na bint mwingine wakat c kwel.bila kuchunguza na bila kunisikilza aliniambia nisimjue.nilitahid kwa mda ilipo shindikana nikakubal yaishe.

Baada ya miez sita alianza mawasiliano na kuniomba turudiane nikakataa.baada ya kumkatalia kwa mda mrefu kulizuka ugomv.hakunitafuta kwa wiki moja na hapo nikaja pigiwa na ndugu zake kuwa amelazwa hospital na ajukal anaumwa ugonjwa gan coz kapimwa lakin hamna ugonjwa, kawa kama kichaa na kila mda ni kutaja jina langu.

Wazaz na ndugu zake walinipigia simu niende coz dactar aliwaambia wanitafute il nifike hospital.

Nilikataa kwenda,isitoshe nilisha hama mkoa na nipo masomon.baada ya hapo cjui nin kiliendelea na imepita miez mi tano sasa.(kwa jumla ni 2 years tangu tuachane)

JUMAMOSI ILIYOPITA
Nilipokea simu ya namba mpya kuuliza jina akajitambulisha ni Huyo X-girl friend.
Nikamuomba asirudie kunipigia simu akakataa na kudai anaenda kujiua.
Jpil nikapigiwa simu na rafik yake kuwa amenyang'anywa sumu na rafik yake.
Leo kanitumia sms akidai bila mim kubadil msimamo juu yake bas nijiandae kwa msiba.

Huyu msichana ameniweka ktk wakat mgumu na kwel anaweza kujidhuru na mim cwez rudiana nae kabisa ila kwa hal hii najiona nakaribia gerezan kwa kusababisha kifo cha mtu.
JAMAN NAOMBA MNISHAUR NIFANYEJE?

Kama haumtaki tena, mpe namba yangu ya simu kaka! Nitamsaidia.
 
Back
Top Bottom