Nishati ya umeme na kizazi kijacho

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,120
1,953
Kwa wale wenzangu na mimi mnaokaa kwenye sehemu za maisha ya watu wa kati(middle class) bila shaka mgawo wa umeme ni kitu cha kawaida.Lakini la kushangaza ni mustakhabali wa maisha ya watoto wetu na nishati hii muhimu ambayo ni HAKI YA MSINGI ya kila mwananchi wa taifa hili.Si mara moja au mara mbili nimeshuhudia umeme ukiwa umekatika,ukirudishwa unasikia nderemo na vifijo kutoka kwa watoto hawa.

Wasiwasi wangu ni kwamba,tunalea taifa la kesho ambalo linajijengea khali ya utegemezi,imefikia hatua ambapo watoto wanaopiga kelele umeme unaporudi,kuona kama ni favour fulani kwao.Hii ni saikolojia ya hatari inayojengwa ndani ya watoto wetu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom