Nisaidieni Wi Fi ni nini?

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
1,002
274
Wakuu habari za mida,naombeni kusaidiwa nini maana ya Wi Fi na inafanya kazi gani ktk simu plogram hiyo ninayo katika simu yangu ya Samsung Gallaxy 5830i ila sijajua matumizi yake.
 
Wakuu habari za mida,naombeni kusaidiwa nini maana ya Wi Fi na inafanya kazi gani ktk simu plogram hiyo ninayo katika simu yangu ya Samsung Gallaxy 5830i ila sijajua matumizi yake.

Ni vyema ukazoea kujipatia majibu ya maswali marahisi kama haya wewe mwenyewe, embu ifanye google sehemu ya maisha yako Google andika wi fi kisha bonyeza search
 
Kama haujui maana ya Wi-Fi na unatumia internet sidhani kama unahitaji simu ya Galaxy!!!! HUO NI UVIVU MKUU!
 
Wi-Fi (short for "wireless fidelity") , is a wireless networking technology used across the globe.

If you have a mobile device having WiFi technology, go to the places where there is access of wireless network, then turn on your mobile WiFi, automatically will search available WiFi around, choose one which is network full then connect, already you have connected to the Internet through WiFi, now you can surf the Internet
 
Asante wadau, mnajua ni vizuri kuuliza, siyo kila tulivyonavyo tunajua matumizi yake. Mie mwenyewe nilikuwa sijui sasa nimejua. Asante sana.
 
Wifi inapatikana wapi hapa nchini?

WiFi inapatikana vyuoni, mahoteli makubwa, maofisini,

kwenye vyuo wameweka wifi kwa ajili ya wanafunzi wao, kwenye mahotel makubwa wameweka wifi kwa ajili ya wageni wao ambao wengi labda ni watalii , pia wifi ipo kwenye baadhi ya ofisi za serikali na binafsi...
 
inamana ukiwa na Wifi una surf net bure?
 
inamana ukiwa na Wifi una surf net bure?

Ndio maana yake!! Pia ukitaka kuepusha msongamano unaweza kununua Wi Fi access point ya kwako ukajinafasi. Yaani hadi 50,000 unapata!
 
inamana ukiwa na Wifi una surf net bure?

chuo, ofisi, hoteli wanalipia access ya internet kwa ttcl, voda etc inategemea wameunganisha toka wapi, baadaye ndio wananunua wireless devices za kuweza kutoa wifi

sasa, watumiaji kama ni wanafunzi, wageni au wafanyakazi wanauwezo wa kuipata hiyo wifi bure. Ila kuna baadhi ya ofis/vyuo wameweka password ili kuzuia muingiliano mkubwa kwa wasio wahusika wa sehemu hiyo, hivyo kupelekea kupungua spidi ya wifi , ukisearch wifi ili kuunganisha internet inakudai password.

Kama ni wifi iliyowekewa password, wahusika kama ni wanafunzi ,wafanyakazi, wageni hupewa password. Ila kama ni wifi amabayo haijawekewa password ukisearch na kuipata ni kuconnect tu na kuanza kusurf!
 
Back
Top Bottom