jamani mbona mnanipotezea wakati nahitaji msaada , watu wakianzisha mada za malavidavi mnazichangia kwa muda huu ingekuwa pg ya tatu km si ya tano nisaidieni mbona mnakuwa hivyo
jamani mbona mnanipotezea wakati nahitaji msaada , watu wakianzisha mada za malavidavi mnazichangia kwa muda huu ingekuwa pg ya tatu km si ya tano nisaidieni mbona mnakuwa hivyo
Acha ubahili,nenda kwa mwanasheria,atakuandikia mkataba kufuatana na matakwa yako.gharama ya mwanasheria inafuatana na thamani ya unachouza.kuwa mwerevu ndugu.pia usisahau kulipa kodi ukishauza,nchi yetu inategemea kodi kuendesha hospitali na huduma nyinginezo.
Hii Attachment ya contract document usiichukulie kama ilivyo kwa vile hiyo ni ya sheria za Marekani. Kila nchi ina sheria zake kuhusu ardhi na nyumba.
Nakushauri nenda wizara ya ardhi watakusaidia dondoo za kuandika mkataba wa kuuza nyumba yako. Ukitumia wanasheria utadaiwa asilimia kadhaa ya mauzo ya nyumba iende kwao.
Afadhali wape posho kidogo watu wa ardhi na asilimia zote utaingiza mfukoni mwako.
Utaratibu mwingine ambao ni gharama nafuu unaweza kuandika mkataba wako mwenyewe na ukampa mnunuaji asome na akikubaliana na yaliyomo basi nendeni pamoja mahakamani mkatie sahihi mbele ya hakimu na hakimu akishatilia sahihi huo ni mkataba wenye nguvu kisheria tayari. Hiyo ni njia wengi wanatumia, na mimi nimeshawahi tumia njia hiyo.