Nisaidieni, nina tatizo la kutokujali ndugu, marafiki na wapenzi

Super human

JF-Expert Member
Feb 26, 2015
1,147
748
Najishangaa na nahitaji msaada wenu, ule utu wa kujali umenitoka huwa nakaa hata miezi mi3 sijajua nyumbani wazazi wanaendeleaje, marafiki hua siwapigii hata simu labda niwe na shida nao tu.

Mahusiano ndo yamenishinda maana naweza kuwa na mdada tukabadlishana namba nikamsomesha akanielewa nikampigia siku moja baada ya hapo itapita miezi miwili na nitaogopa kumtafuta tena.

Hebu nisaidieni hivi hii ni kawaida au nini? Muda wa hewani hua naweka vuzuri ili na hua unaishia hewani is this a problem au nipo kawaida tu?
 
Hii ni Tabia ya Wana Dar Es Salaam tu so usishangae... Maana Ndugu na Jamaa ukiwa nao sana utaishia kupigwa vizinga na mikopo ambayo hulipwi na ndio chanzo kikuu cha kupotezeana Dar... Kama unanidai why nikutafute tafute mwendo kukukwepa wengine hata kwenye misiba au harusi hawaendi wakijua mdai wake atakuwepo pia... Kusalimia ulipotoka jitahidi tu hivyo hivyo jiwekee kiwango cha kupigwa mzinga isizidi buku ten
 
1.unavuta bangi? Au unatumia sana konyagi? Au unatumia kilevi gani sana
2.unasali au unaswali
3.unahela nyingi au unavijisent
4.unakaa kwa ndugu yako au umepanga
5.unapiga punyeto sana au unacheki sana porn
6.wew ni mwanaume au kavulana
7.unatongozaga kweli au unajitapa tuu

Ukijib maswali haya takuja kukushauli
 
Pole mkuu ila hata mim nahisi nina hako kaugonjwa mvivu sana kuwasiliana na watu yani marafiki hata familia.

Wakati napanga kuo nilijua lazma nitengeneze ukaribu na wakwe nikasema nibadilike niwe mwepesi kuwasiliana ila hapana nimeshindwa.

Toka nioe nimerudi kwa wakwe baada ya zaidi ya miezi 18 na hapo nimewasiliana kwa simu haizidi mara tano.

Wife kalalamika kwamba siwajali kwao mpaka kazoea kwa sasa kashajua ndo nilivyo kwani hata ndugu zangu kuwasiliana nao ni shida mno ila na nyinbani washanizoea kwani ndo nilivyo tokea mdogo nimekua na hako katabia

Si kwamba sijali najali mno na nawakumbuka sana ndugu jamaa na marafiki ila kuwatafuta ndo uzito.

By nature huwa napenda ku concetrate sana katika mambo yangu nahis hiki pia kimejenga hakankatabia.

Pia mzee wangu kukaa huko kwa wazungu basi na sisi alitulea na uzungu flani hivi yani msemo wake mkubwa "mind your own business" bas ndo tumekua katika mtazamo huo
 
Unauliza Maswali ya kipuuzi kama huelewi mada.. wadhania mtu akiomba ushauri anapiga magoti... watu wapo for having fun tu ... ficha upumbavu wako... mtoa mada ungekuwa ni ndugu yake nadhani angekutafuta kila baada ya miaka kumi na tano maana maswali kama hayo yanamfanya mtu akuone kinyaa na kinyaa huisha baada ya miaka hiyo
 
Mi pia naona huo kama ni ugonjwa ninao.. Ila nadhani ukiwa busy sana na mambo yako watu wanakutafuta uko busy.. Mara 2,3 uko busy tuu basi wao wanaona unawatenga so nao wanajitenga au kukutenga... BTW, mi personally sioni shida kwa hii hali as long as siku nikiwatafuta nawapa deal za kueleweka na hatugombani gombani anymore.
 
Pole mkuu ila hata mim nahisi nina hako kaugonjwa mvivu sana kuwasiliana na watu yani marafiki hata familia.

Wakati napanga kuo nilijua lazma nitengeneze ukaribu na wakwe nikasema nibadilike niwe mwepesi kuwasiliana ila hapana nimeshindwa.

Toka nioe nimerudi kwa wakwe baada ya zaidi ya miezi 18 na hapo nimewasiliana kwa simu haizidi mara tano.

Wife kalalamika kwamba siwajali kwao mpaka kazoea kwa sasa kashajua ndo nilivyo kwani hata ndugu zangu kuwasiliana nao ni shida mno ila na nyinbani washanizoea kwani ndo nilivyo tokea mdogo nimekua na hako katabia

Si kwamba sijali najali mno na nawakumbuka sana ndugu jamaa na marafiki ila kuwatafuta ndo uzito.

By nature huwa napenda ku concetrate sana katika mambo yangu nahis hiki pia kimejenga hakankatabia.

Pia mzee wangu kukaa huko kwa wazungu basi na sisi alitulea na uzungu flani hivi yani msemo wake mkubwa "mind your own business" bas ndo tumekua katika mtazamo huo
Nimekuelewa sana mkuu.
 
Tatizo limekuanza lini? Ni asili yako au limekuja kukutokea recently?

Kama ni asili yako basi jitahidi kujirejebisha na kuwasiliana mara kwa mara na Wazazi wako na pia Binti utakayempenda (ikiwa hujaowa bado) kwani hakuna namna hapo na hawa wenzetu wanapenda sana mawasiliano na kujuliwa hali.

Kuhusu marafiki wasiliana na WACHACHE SANA wale ambao at least unawaamini hata kama ni mmoja tu.
 
najishangaa na nahitaji msaada wenu ule utu wa kujali umenitoka hua nakaa hata miez mi3 sijajua nyumbani wazaz wanaendeleaje, marafiki hua siwapigii hata cm labda niwe na shida nao tu, mahusiano ndo yamenishinda Maana naweza kuwa na mdada tukabadlishana namba nikamsomesha akanielewa nikampigia siku moja baada ya hapo itapita miez miwil na nitaogopa kumtafta tena. hebu nisaidieni hiv hii ni kawaida au nn? muda wa hewani hua naweka vzr ili na hua unaishia hewani. is this a problem au nipo kawaida tu?
tueleze zaidi kuhusu wewe: umri wako na elimu yako?
 
Tatizo lako wanalo watu wengi sana siku hizi
sababu ya race za maisha
maofisini kuna targets na malengo
maisha binafsi nayo yana stress nyingi
so unakuwa unakosa ile quality proper time ya kwako
au ya ku socialize na watu...

Kenya nasikia misiba ni weekend only
i mean jirani yako akifiiwa unapewa taarifa lakini hata kama ni jumatatu
mnaendelea na shuguli zenu za kiofisi hadi jumamosi ndo mnaenda msibani

maisha yanakimbia sana....na wewe mbio za maisha hazikupi mda wa ku process kila kitu
ni kama kila mtu anaku interrupt hivi...
mara mamdogo anaumwa....arrgh
mara mtoto wa mjomba kaja ..arghhh
mara uko home umeme umekatika ....arrgh
mara ofisini ile ripoti imerudishwa iandae upya ..arrghh

ndo maisha ya sasa hayo ..hauko alone
 
Imesababishwa sana naule msemo wa Mtegemea cha Ndugu hufa Masikini... so watu wanachakarika usiku na mchana undugu na urafiki msibani.... Imefikia sasa mtu ana msiba wa ndunguye yeye anangalia kwanza mali zake ziwe salama ndio aende au kazini kwake ndio first Msiba baadae
 
1.unavuta bangi? Au unatumia sana konyagi? Au unatumia kilevi gani sana
2.unasali au unaswali
3.unahela nyingi au unavijisent
4.unakaa kwa ndugu yako au umepanga
5.unapiga punyeto sana au unacheki sana porn
6.wew ni mwanaume au kavulana
7.unatongozaga kweli au unajitapa tuu

Ukijib maswali haya takuja kukushauli
sivuti bang, pombe nakunywa kdogo, mm ni mwanaume nshapita umri wa uvulana kabsaa, hua siend kusal kabsaa.
 
Tatizo limekuanza lini? Ni asili yako au limekuja kukutokea recently?

Kama ni asili yako basi jitahidi kujirejebisha na kuwasiliana mara kwa mara na Wazazi wako na pia Binti utakayempenda (ikiwa hujaowa bado) kwani hakuna namna hapo na hawa wenzetu wanapenda sana mawasiliano na kujuliwa hali.

Kuhusu marafiki wasiliana na WACHACHE SANA wale ambao at least unawaamini hata kama ni mmoja tu.
thanks kwa ushauri mzur mkuu
 
Wengi tupo hivyo tunaonana tu kwenye social network na sometime hata like hatupeani tunaogopa mikopo na mizinga... haswa baada ya mambo ya mpesatigopesa na airtel money kuja.. maana mtu unatoa jasho lako we anakuja mtu mvivu anachukua kama zake...

Tutaonana kiaina aina hivi hivi....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom