Nisaidieni nifanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nisaidieni nifanyaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Makubi, Jul 26, 2011.

 1. M

  Makubi Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wapendwa wa mmu, ningependa mnipe ushauri kwa kilichonikuta mwenzenu, nina girlfriend wangu ambaye uhusiano we2 una mwezi1 sasa, ashawahi kuniambia kuwa aliachana na ex boy wake kutokana na jamaa kutomjali sasa leo kaja kaniambia kuwa ana mimba ya mshikaji na alijarib kwenda kuitoa ikashindikana na ni ya miez 3 na kamwambia jamaa, jamaa kampotezea na atak hata kumwona sasa kaniambia ili asikie mi nitasemaje, jamani nisaidien nifanyaje?
   
 2. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Makubi pole kaka... Ushauri unategemea saana wewe una umri gani?
  Unafanya kazi? Unajiweza/jitegemea? Is she worth it? Usha fall in love?

  Walau jibu in blue... then ni rahisi kukushauri kitu ambacho kitafaa....
   
 3. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  mkuu swala lako ni kubwa na gumu sana mkubwa Makubi, lakini una'advantage moja ya muda.. Mwezi mmoja si kitu, nakushauri Achana nae, ujauzito wa miezi mitatu usiwe mzigo kwako BUT kama waona sawa waweza endelea, Just like Joseph (Baba mlezi wa yesu), Fikiria kwa dhati!
   
 4. M

  Makubi Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kusema kweli nampenda na niko A level (form 6) na nina umri wa miaka 19 na yeye kamaliza a level mwaka jana
   
 5. M

  Makubi Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanx @gagurito
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Yani miezi mitatu iliyopita alikua na mshkaji...na tayari wewe na yeye mmeshamaliza mwezi?!HAPUMZIKI kutafakari hili na lile kabla ya kujichanganya tena?!

  Nwy ungesema hisia zako zinakutuma vipi ingekua rahisi zaidi kukushauri maana kukwambia fanya hivi au vile bila kujua unachofikiria wewe ni kama tutakua tunakuagiza na maagizo yatakua mengi kweli kweli .
  Muhimu ni wewe kujua una malengo gani nae...kama nia yako ilikua kumchezea ni bora umwache mapema hii badala ya kumjengea matumaini kibao yasiyokuwepo.Asije akatoa mimba kwaajili yako wakati wewe huna mpango nae.Kama malengo yako ni zaidi ya kupotezaniana muda na kuchezeana basi kaeni mjadili nini chakufanya na jinsi gani mtakabiliana na hali yake hiyo.Kama hujali unaweza ukamsaidia na kumsupport iwe kama rafiki au mpenzi.

  Na kuhusu yeye kutoa mwombe akwambie kwanini anataka kufanya hivyo...kama ni ili wewe na yeye muendelee kua basi tafakari kama ni sahihi kuua kiumbe kwaajili ya mahusiano au la...tena mahusiano yenyewe ukute ni ya mpito.Kama ni umri wake na hali ya kimaisha inayomfanya attake kufanya hivyo basi afikirie mara mbilimbili kabla ya kutoa.

  Zaidi ya hapo sina cha kusema maana maaisha ni yenu na maamuzi ni yenu kwahiyo fanyeni maamuzi yaliyo sahihi.
   
 7. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #7
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Makubi dear... Uko katika a wonderful age of falling in LOVE... Hivyo najua kabisa ni jinsi gani inakuumiza na jinsi gani unaamini kua Love is enough kwa ku survive kwa Mapenzi yenu... BUT The reality Makubi ni kua wewe bado ni mdogo, na tayari huyo binti as mdogo kidogo kwako au the same age tayari kisha kupita na ni mtu mzima sasa..... Ingekua mimba ni yako that would have been well and good na ungewahusisha home mje na solution...

  Wewe cha kuzingatia ni masomo na pia kua makini, ni dhahiri kabisa hutumii Condoms... Na ni dhahiri kabisa kua Unajivisha majukumu ambayo huwezi ya mudu, naongea hapa kwa upole sababu ni jamvini, ingekua ni nyumbani na ni mdogo wangu ningekua naongea huku nakusokonyoa kichwa chako nikisikitika kua mawazo yako ni Ovyo... na ningeenda kwa huyo binti na kumpa ushauri aeleze kweli kwa familia yao wao watajua what is best for her.... And please hali imekua mbaya msijidanganye mkasindikizana kutoa.... Pole saana.
   
 8. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,719
  Likes Received: 8,269
  Trophy Points: 280
  Eeeh...!???
   
 9. s

  shalis JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona wwe bado mdogo na majukumu unayoyataka ni makubwa
  pole
  sali sana
   
 10. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ndo ivo.
  ana miaka 19.
  Yuko A level.
  Ana demu kwa mwezi mmoja, mwenye mimba ya miezi mitatu.
  Anaomba ushauri.
  Crystal clear.
   
 11. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi wadogo zetu mtaweza kweli kufika walikofika akina Nyerere kama katika umri huo mdogo unawaza kutoa mimba..nwy ushauri wangu..hebu mwambie binti awajulishe wazazi wake..wewe hujui kitu bwana..usfikiri kutoa 'mimba ni sawa na kununua jaketi lako'
   
 12. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,272
  Trophy Points: 280
  Ukipenda boga penda na ua lake hapo we lea nimali yako!
   
 13. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Jinsi unavoojiexpress, ni kuwa una uamuzi tayari.
  Unawaza kuitoa mimba.
  Then kuoana?
  Then what?
  Hebu tuambie options zako and we will discuss along the line of your options and lead you to make your own decision.
  Hivyo vyekundu sijui kama unajua maana yake.
   
 14. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ndo mambo ya kitanda hakizai haramu hayo.
  Lakini bado ni haki elimu.
   
 15. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,719
  Likes Received: 8,269
  Trophy Points: 280
  Mh..Hilo ni boga ama ua la boga linaloweza kunyauka litokapo jua!??
   
Loading...