Nipsey Hussle: Nyota ya Afrika Mashariki kutoka katikati ya magenge ya kihalifu na kuangaza katika sanaa ya Muziki wa kufoka foka (Hip Hop).

Ziggy Sobotka

Member
Feb 13, 2019
19
36
IMG_0642.JPG

Ermias Davidson Asghedom kijana wa miaka (Agusti 15, 1985 – Mach 31, 2019), akijulikana kwa jina la sanaa kama Nipsey Hussle. Ni msanii wa sanaa ya muziki wa kufoka foka (Hip Hop) kutoka Calfonia, Marekani.
Mtoto wa mhamiaji wa Kielitrea na mama mwenye asili ya Mmarekani mweusi pia Baba wa watoto wawili, aliyekulia katika mitaa yenye fujo na inayoogopwa kwa kuwa na mauaji mengi na matukio ya kihalifu.
Siku ya Jumapili tarehe 31 Machi 2019 ilikuwa siku ya masikitiko kwa wapenda sana na mashabiki wa Nipsey Hussle baada ya kuenea kwa uvumi uliokuja kuthibitishwa baadae kuwa Nipsey Hussle amapigwa risasi, mbele ya duka lake la nguo. Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na Nipsey Hussle wanasema alienda dukani hapo sababu kulikuwa na sherehe kidogo ya kumkaribisha nyumbani rafiki yake wa muda mrefu aliyekuwa ametoka jela alikokuwa anatumikia kifungo cha miaka 20 lakini furaha hiyo ikageuka majonzi kwa kupigwa risasi na mtu anayesadikika ni rafiki wa karibu ila sababu ya wivu na mafanikio ya Nipsey.
Nipsey Hussle katika kipindi cha uhai wake alichangia sana kuufahamisha ulimwengu kuhusu Afrika na hasa Afrika mashariki kwenye mizizi ya asili yake nchini Eritrea. Alifanya safari ya kwanza kusalimia ndugu zake akiwa na miaka 18 hata kabla hajapata umaarufu, na mwezi april 2018 alifanya safari nyingine kitembele Eritrea akiongozana na Baba yakebpamoja na mdogo wake. Alikutana na rais wa Eritrea ikulu pamoja na waziri wa mawasiliano pia alitembelea vijiji alivyokulia Baba yake pamoja na kiwanda cha nguo nchini humo.

Moja kati nyimbo zake anaitaja Lugha ya kiswahili kuonesha ni jinsi gani alikuwa anapenda uafrica wake

KEY TO THE CITY 2 LYRICS
I got the key to the city
I got a hoe that's saddity
Talk to that bitch in Swahili
Tattoo my name in graffiti
Wack at your hood in graffiti

Atakumbukwa kama mwanaharakati, mbunifu wa sanaa aliyejitoa kutoa elimu kwa jamii ya wamarekani weusi kuhusu kuwekeza na kuachana na utamaduni wa magenge ya kihalifu yanayoleta mauaji yasiyo na tija, aliyeishia kuuwawa na hao hao aliowapa Elimu. R.I.P


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom