Nipo wilaya ya Rombo kikazi hii wilaya ni ngumu sana kuishi

sijawahi kusikia BTP YA S/M YA MIEZI 6! au ndo mpango mpya wa serikali kuwajengea walimu uwezo na ubora? embu fafanua zaid hapa mkuu afu useme hiyo Rombo upo Maeneo gani? MAMSERA, MENGWE, MANDA, KENI, SHIMBI, MKUU, MASHATI, USERI, TARAKEA, RONGAI, KAMWANGA?
Itakuwa wiki sita
 
Si utafute jimama moja liwe linakusaidia huko maana wamama wengi hawana wenza huko au wewe ni ke?
 
Habari wanajamvi!

Wakuu nipo Wilaya ya Rombo kwa kazi ya miezi 6 field ya shule ya msingi, Huku kuna shida ya maji na kila baada ya mita 800 unakutana na visima vikubwa vya kuifadhia maji vikiwa vinavuja maji ila kwenye mabomba hayatoi maji! Waziri wa maji embu njoo huku uje utumbue hili jipu la hili shirika la maji, Linapoteza hela nyingi sana! na Mkuu wa wilaya sijui na hili halioni! Maji unayafuata kilomita 6 wakati visima vinamwanga maji chini!


Hiyo Rombo yako sijui ipi, mimi nimeishi Rombo tokea mwaka 1981, nyumbani nilikuta bomba la maji na sikuwahi kujuwa lilifungwa lini na hadi wiki tatu zilizopita nilikuwa huko sikujaona bomba likiwa halina maji. Ninakubali kuna maeneo ya mashariki yanayopakana na Kenya yalikuwa na shida ya maji, ila sidhani kama hali ipo hadi sasa hivi. Hata hivyo, ukiona shida ipo ujue kuna uzembe ambao kweli Mbunge na viongozi wengine ni wakutumbua tuu... Hujazungumzia umeme kaka ambao najua tokea 1984 ulikuwa unawaka wilaya nzima...
 
Back
Top Bottom