Nipo tayari kwa uchaguzi huu na ule

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,469
2,000
Nikiwa ni mtanzania mwenye sifa za kupiga kura, nimeshajiandikisha kwa ajili ya kura za Serikali ya Mtaa. Nimo pia kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura. Likianza kuboreshwa,nitawahi mapema kujiandikisha/kuboresha.

Nitawasikiliza wagombea wote kwa makini na kujiandaa kupiga kura. Siku ya kupiga kura nitapiga kura yangu kwa mgombea bora kwa vigezo visivyozingatia chama,rangi,kabila wala jinsia. Nitamchagua ninayemuamini kuleta maendeleo.

Nitapiga kura ya Serikali ya Mtaa nyumbani Visiga,Kibaha Pwani.Mwakani nitahamisha kura yangu toka Ubungo hadi Kibaha Mjini.

Muungwana mwenzangu vipi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom