Nipo njiapanda: Shule au Ajira?

Kwanza nikusahihishe, unaweza usiende na ukapata ajira tena....kukosa ajira ni mpaka uingizwe kwenye "Mfumo wa malipo ya mshahara" usipoenda hautaingizwa...So,siku nyingine unaweza kuomba.

Nimeanzia hapo kukufuta hayao mawazo.

Ngoja nikushauri sasa.....
 
Nakushauri nenda karipoti kituo cha Kazi (kuripoti hakumalizi hata siku mbili) baada ya hapo watakupa muda wa kurudi ulipotoka kujiandaa, kuja kuanza kazi rasmi.

Sasa, umesharipoti...umepewa na muda wa kujiandaa...Unarudi Chuo kufanya UE. Ukimaliza kufanya UE (kulingana na muda ulipewa kazini) ndo unarudi tena kazini kuwaambia maelezo kukuhusu wewe.

Utajieleza vyote...kama Afisa Utumishi atakuwa mtu fresh, atakupa ruhusa urudi kuendelea na masomo... Akikataa fresh tu, Chuo kikifungua unarudi kuhairisha Mwaka.
 
Wakati unaenda kuripoti, usiwaambie kwanza kama unasoma, ili kuepuka wasikuchanganye...Wee ripoti, pewa/omba muda wa kujiandaa kuanza kazi rasmi.....Rudi Chuo malizia UE yako....Halafu ndo urudi kazini ukajieleze...wakiwa fresh watakupa ruhusa, wakikataa utarudi chuo kikifungua kuhairisha mwaka.
 
Ahsante sana Mkuu
 
Mkuu ukishaajiriwa usiache kazi kisa chuo.ni bora usome evening class,ingia kazini mapema asubuhi saa 12 jisomeee weee mpk saa tatu tatu unapiga kazi,na ikifika saa tisa na nusu nenda chuo kapige ngeli ndio utaratibu wengi tumetokea huko
 
Ni vizuri kuwa muwazi na mkweli toka siku ya kwanza. Wahusika wengi watakuwa tayari kukushauri.
 
Maliza UE then andika barua ya kuahirisha masomo ukakamate ajira,then mambo mengine yatafuata
 
Mkuu ukishaajiriwa usiache kazi kisa chuo.ni bora usome evening class,ingia kazini mapema asubuhi saa 12 jisomeee weee mpk saa tatu tatu unapiga kazi,na ikifika saa tisa na nusu nenda chuo kapige ngeli ndio utaratibu wengi tumetokea huko
Kwa MD hakuna evening classes, hivyo ili afuate ushauri wako itabidi abadili fani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…