Nipo Njia Panda, Nipeni Mawazo yenu!

Ctech

JF-Expert Member
Nov 21, 2010
754
816
Poleni na majukumu ya Kila siku ndugu

Tatizo lililonileta hapa ni kuhusu mahusiano yangu na binti mmoja yupo kidato cha sita na mimi nipo chuo naingia mwaka wa mwisho!

Huyu binti nimempata miaka Miwili iliyopita na mpaka sasa tunapendana kweli, na tunatamani kuwa baba na mama siku moja ila tatizo ni kwamba mimi sina imani kama inawezekana kumuoa yeye ukizingatia bado ana safari ndefu ya kimasomo

Kingine ni Hili la kuogopa kupoteza muda wangu na energy yangu kwa mtu ambaye baadaye naweza hata nisimuoe tukaishia kupotezeana muda na kuumizana, pia ukizingatia binti kwai wapo vizuri kiuchumi na mimi kwetu pa kawaida sana, hii inanifanya nihisi kwao watataka mwanaume ambaye tayari aa financial Freedom!

Binafsi Mimi nafikiria kumuacha Maana naona im too young(23yrs) kufikiria maswala ya kuoa, hii itafanya nisiwe na ufanisi katika shughuli zangu hasa masomo yangu pia!

Baada ya kuwaza binafsi nimetamani kuwashirikisha na nyinyi ili mnipe maoni yenu isije nikafanya maamuzi ya kushtukiza nitakayoyajutia!

Santana
 
Achana nae soma dogo mambo mazur yapo mbele
Mi nlikua siamin baada ya kumaliza masomo yangu miaka sita
Sasa hivi na enjoy hatar mpaka wengine na wapiga stop wasije wakagongana geto
Tulia soma tafuta kaz ufurahie maisha hizi nyapu zipo utakula sanaaaaaa
Ila ukifeli ndiyo bas hata huyo dem atakukimbia
 
Achana nae soma dogo mambo mazur yapo mbele
Mi nlikua siamin baada ya kumaliza masomo yangu miaka sita
Sasa hivi na enjoy hatar mpaka wengine na wapiga stop wasije wakagongana geto
Tulia soma tafuta kaz ufurahie maisha hizi nyapu zipo utakula sanaaaaaa
Ila ukifeli ndiyo bas hata huyo dem atakukimbia

Mkuu nafikiriaga hivi kila siku ila nashindwa kufanya maamuzi
 
Punguza uoga na uongeze kujiamini, kama unampenda na unaona anafaa kuwa mama wa familia yako basi hunabudi kumlinda na kumtunza na yeye naamini atatambua thamani yako

Case study za watu wengine zisikukatishe tamaa na kukurudisha nyuma

Kila la heri mkuu
 
Nakushauri usimpe asilimia zote Mara nyingi wakishaingia chuo ndo basi tena wanapoteana.....utaanza kuona mabadiliko so chamsingi anza kujiongeza mdogo mdogo
 
Mkuu nafikiriaga hivi kila siku ila nashindwa kufanya maamuzi
Hakuna vita ngumu kama vita ya nafsi
Ukipigana kichwa kichwa unashindwa mapema sana
Very simple way mwambie saiv upo bize na kitabu
Walah nakuambia mdg angu huyo dem hutakuja kumuoa
Ukizembea kdg utajutaaaaa maisha yako yooooteeee walah
Ngoja aende chuo
 
Back
Top Bottom