navin bobby
Member
- Feb 17, 2016
- 21
- 39
Wadau,
Ukoo upo kwenye vikao na maandalizi ya mwisho kabisa ya kumsafirisha baba yangu mkubwa kuja Dar kwa matibabu zaidi baada ya ugonjwa wake kushindikana katika hospital ya mkoa.
Ukoo wamepanga afikie kwangu na mimi ndie nishughulike na masuala ya Muhimbili na hiyo rufaa kwa ujumla, baba amenipigia simu kunijulisha kuhusu mgonjwa kufikia kwangu, hakutaka majadiliano, ni kama amri vile, mzee wangu ni mkoloni hakuna mfano.
Kinachotutisha ni hali ya mgonjwa ilivyo, chances za kupona ni very slim, watotoa taarifa wameniambia kwanza akifika hai Dar basi mungu mkubwa, hivyo nikamgomea mzee kuwa haiwezekani hatuna nafasi.
Mzee akasema tutaona, kwamba anajua ni mke wangu ndio kakataa, sababu anawajua wanawake, hivyo akadai atamsafirisha mgonjwa hivyo hivyo tupende tusipende, akampigia na wife simu akamfokea sana.
Wadau, tunalikataa suala hili kwa sababu wote mnajua hali ilivyo kwa sasa, posho za vikao zimefutwa, mianya yote ya deals imefungwa hapo kazini, naishi kwa mshahara tu ambao nao nilishaukopea hivyo hauji kama ulivyo, sasa kwa hali hii nije nipate msiba hapa which is more likely, maana mgonjwa sasa amevelop kwiki kwiki isiyokatika muda wote.
Gharama za kusafirisha msiba kwenda mkoa wetu kwa coaster ni karibu 4 million, na mimi sina watu kihivyo hapa mjini, haya, bado gharama za hospital, tuseme Mungu ametenda muujiza akafika akalazwa najua gharama zote za hospital wataniachia mimi, maana wanaendelea kufikiria nina hela kama zamani
Wanampigia mke wangu simu na kumtisha kuwa watamtoa kwenye hii ndoa kama mgonjwa akifa, baba kila saa ananipigia simu nitume hiyo nauli ya ndege mgonjwa asafirishwe haraka mimi nakua namchenga.Sasa jambo hili limekua kubwa katika familia na limeleta mzozo mkubwa.
Msaada wenu wa mawazo unahitajika haraka sana.