Nipeni Uzoefu kwa Watoto Wenu!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Habari wanajamvi!

Kwa mara nyingine tena najimwayamwaya jamvini nikija na 'kamba' nyingine ya kimalezi zaidi. Awali ya yote niwaombe samahani wale waliokwazika na 'thread' yangu ya awali ya ugomvi wa remote na watoto. Wengi walitoa ushauri mzuri, na wengine walipendekeza niwe nakesha bar kuepuka 'karaha' za kugombea remote na makid wangu. Kwa kuzingatia ushaur wa wengi kwamba nijaribu kutuliza majeshi home ili kuboresha malezi, basi kuna mambo mengi nimegundua miongoni mwa watoto wawili ambao ndiyo huwa lile vurumai la remote ndo huwa linanitokea nao.

Nimegundua kuna vitu watoto, ingawa wamekuwa hawawezi kusema hapana, wamekuwa wakiniambia hivyo 'indirectly'. Mara chache inapotokea mtoto wangu (miaka 4) hataki kula baadhi ya vyakula asivyovipenda, nimegundua amekuwa akitoa sababu na visingizio vya aidha tumbo linamuuma au atakula baadae. Mwanzoni nilikuwa nikiamini kuwa ni kweli, ila with time nikagundua kuwa mara nyingi ni janja ya nyani ya kukataa kula. Baada ya kulazimishwa sana amekuwa anakula chakula pamoja na awali kudai kuwa tumbo linamuuma. Hali hii imekuwa ikitokea pia ktk kuoga na mambo mengine ambayo kwa namna moja au nyingine amekuwa hapendezwi kuyafanya wakati fulani au hataki kufanya kabisa.

Hali kama hii imekuwa ikitokea hata kwa baadhi ya siku ambazo hajisikii kwenda shule asubuhi. Anapoamshwa sometime hudai anaumwa, lakini baada ya kukomaliwa sana, huwa anarudi kwenye mood na kutenda lile analokazaniwa alifanye-kwenda shule. Kaka yake pia alikuwa na tatizo kama hili, ingawa alipofikisha miaka 5 aliacha haka katabia.

Kwa mara nyingine, wanajf naomba tueleweshane hapa. Je na ninyo wazazi mmeshakutana na hali hii kwa watoto wenu? Na kama mlishakutana/mmeshakutana nayo ni mbinu gani mlizitumia kuitokomeza hali hii? Kuna wakati natamani nitumie bakora kuitokomeza hii hali lakini nachelea kusema kwamba pengine kuna njia muafaka pasipo kutumia mabavu kukabiliana na hili 'tatizo'.

Naombeni mchango wenu waungwana!
 
Back
Top Bottom