Nipeni ushauri nifanyeje juu ya hili?

Nipeni ushauri nifanyeje juu ya hili?

Ondoa kbsa carbohydrates kwenye mlo wako. Kula proteins zaidi. Ukishindwa kupungua nenda ukapimwe growth hormones
 
Kwa ambao ntawaudhi kwa hili ntakalolisema mtanisamehe lakini nahisi hapa JF naweza pata ushauri au msaada wa nini cha kufanya kwa hii hali yangu.

Mimi ni kijana, umri wagu ni miaka 28 nimetimiza tu mwezi wa tisa mwaka huu. Naishi gongo la mboto, Dar es salaam. Changamoto yangu kubwa ni unene. Unene huu unanipa muonekano wa kibaba, yaani naonekana kama 'mbaba' hivi. Kuhusu mazoezi ya kukimbia nimefanya sana lakini unene haunitoki, hata mpira nacheza sana katika timu yetu ya mtaani lakini hainisaidii kupunguza unene angalau na mimi niondoe ule mwonekano wa 'kibaba'.

Muonekano huu unanipa changamoto sana kwani mpaka sasa sina mahusiano ya kueleweka. Wanawake (wa umri wangu) karibia wote wananikataa wanahisi mimi sio umri wao, wengine wananiamkia. Yaani mwanamke nikishamwita tu anaanza kuniamkia. Mwingine anaweza akaja akaniambia ukweli kabisa kuwa "mimi sio umri wako".

Hapa nimeshadangwa sana, mpaka nafikia hatua naogopa KABISA wanawake. Wakiniona tu wananiona 'danga material' yaani baba fualni hivi (mwenye mke na watoto) anapenda watoto wadogo. Ikitokea mwanamke akanipa namba basi kinachofuata ni mizinga MIZITO akihisi kalipata danga la kumhudumia. Rafiki zangu wawili wamepata wanawake na wameshaoa lakini changamoto ipo kwangu kutokana na huu muonekano wangu. Nifanye nini mimi nisionekana 'mbaba', mazoezi ya kukimbia nayafanya kila siku asubuhi na jioni lakini nipo vile vile nakula kidogo sana na sometimes hata usiku nalala bila kula ili nipungue lakini wapi.

Nimeajiriwa, hapa ninapofanyia kazi vijana wenzangu hata hawapendi kushirikiana na mimi, wanahisi sio mwenzio, wanaweza kuamua kukutana kula bata jumamosi lakini mimi hawatoniambia wanaona kama huyu mbaba akija hapa "atatunyima uhuru". Naweza sema labda wananiheshimu maana hata nikiwepo hawaongei stori zao za kiujana lakini kuniweka mbali nao inanipa maswali sana.

Nipeni ushauri jamani nifanyeje ? Maana hapa nilipo kwenye ujana sipo na kwenye uzee sipo.
We jamaa kuna uzi wako hapa ulikuwa unatafuta mke ukasema una miaka 26 hata mwaka haujaisha umeshatimiza 28? Hadi mwaka uishe si utakuwa na 30! Kwa uongo huu sikupi ushauri endelea tu kuwa tukunyema
 
Asante kwa ushauri lakini mimi sina tatizo la kujiamini. Na suala la kujiamini halihusiani na kesi yangu. Asnate lakini!
halihusiani na kesi yako wakati unadai hupati wanawake kwa sababu ya mwili wako,marafiki wanakutenga hapo unajiamini vipi
 
Ingekuwa namna tungebadilishana maumbo, natafuta unene kwa hali na mali lakini wapi.
 
Njoo nikupangie mlo wa wiki nzima, ndani ya miezi mitatu utapungua kwa kiasi kikubwa sana.. hakikisha unafuata ratiba bila cheating
 
Hata mm nina miaka 24 lakini nina muonekano kama mbaba lakini hiii hunipa advantage sana nina uwezo wa kula mmama yoyote yule inshort kwa upande wangu hiii ni advantage najikubali sana
 
Mazoezi fanya intensive exercises na kula responsibly. Ruka kamba kila jioni na kimbia vya kutosha. Kua na consistency ya mwezi mmoja utaona mabadiliko
 
Nenda gym uwe na trainer kabisa fanya mazoezi mfululizo kwa miezi 6 utaona matokeo
 
embu weka picha nikuone,ficha tu uso pengine nawaza kuwa mkeo
 
Ila ujue kujipenda,kuvaa vizuri na kujipiga manukato
 
Back
Top Bottom