Nipe muda nikafikirie

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Hii ni kauli maarufu sana kutoka kwa akinadada mara baada ya kutongozwa na akinakaka. Wanajamvi tuelimishane,ni nini hasa ambacho hufikiriwa na akinadada kabla ya kukubali au kukataa kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi?
 
tunafikiria mengi sana.
Yepi hayo..??? Halafu huwa nashangaa wakati mwingine huwa mnakubali huku mnaendelea kufikiria... Au wakati mwingine mnakataa katakata huku bado mnaendelea kufikiri...
 
kama yapi dada husninyo

kama yapi dada?

Yepi hayo..??? Halafu huwa nashangaa wakati mwingine huwa mnakubali huku mnaendelea kufikiria... Au wakati mwingine mnakataa katakata huku bado mnaendelea kufikiri...
tunafikiria tu kama wewe ni mtu sahihi na utayari wa kuingia katika hayo mahusiano. mara nyingine tunahitaji kuwafahamu japo kidogo, kuona kama tunaweza endana ama au tutashindwana kabla hatujaanza mahusiano rasmi.
 
Duh, Wanaume tunashida, tukikubaliwa mapema shida, tukiombwa tuwe na subira shida, sasa lipi Jema kwetu???
ila siku hizi mna haraka kama ushuzi, hamna subira hata kidogo. mie nikiona una haraka sana najua hunifai. kuku wako manati ya nini? subiri aingie bandani umkamate kiulaini.
 
tunafikiria tu kama wewe ni mtu sahihi na utayari wa kuingia katika hayo mahusiano. mara nyingine tunahitaji kuwafahamu japo kidogo, kuona kama tunaweza endana ama au tutashindwana kabla hatujaanza mahusiano rasmi.
sasa unapokuja kuingia kwenye mahusiano halafu ukagundua kuwa ulikosea, ina maana hukufikiri au..??
 
Kabla hujakubali unakuwaje kuku wangu mwenyewe bana..???
 
hayo ni matokeo tu ila wakati wa kufikiria ni wakati wa kuridhisha nafsi zetu kwamba tunaingia katika mahusiano na mtu sahihi. kuiset akili na mwili vilevile kwa maamuzi utayofanya.
 
Kabla hujakubali unakuwaje kuku wangu mwenyewe bana..???

kuna wanaoomba kufikiri kwa namna mbili. wapo ambao washakubali ila wanataka kukufahamu vizuri kabla hamjaanza rasmi.. hapo kuku anakuwa ni wako tu na huitaji papara. kuna wale ambao hawajatoa jibu rasmi, mpaka afikiri kwanza ndio ajibu ndio au hapana.
 
Mkuu ushawahi kuona wapi ukipeleka maombi ya kazi unaajiriwa pasipo kupitia usahili au walau hata wasifu wako kutazamwa kidogo?

Si jambo rahisi kama mnavyofikiri, namna ubongo wa mwanamke utendavyo kazi si kama sisi wanaume.

Wakati mwanaume hupenda kwanza kupitia maumbile, mwanamke huanza na hisia halafu maumbile baadaye.

Jambo lolote linalohusisha hisia huitaji tafakari ya kina na kumbuka hapo si wewe pekee uliyemtongoza bali kuna wanaume wengine kibao wapo kwa queue.
 
tunafikiria tu kama wewe ni mtu sahihi na utayari wa kuingia katika hayo mahusiano. mara nyingine tunahitaji kuwafahamu japo kidogo, kuona kama tunaweza endana ama au tutashindwana kabla hatujaanza mahusiano rasmi.

Hivi unajua kwamba nakupendaga sana?

Yaani usiku silali nakuwaza wewe tu
Nikinywa maji nakuona kwenye jagi

Yaani wewe unanimaliza kabisa
Tafadhani likubalie uwe mupenzi wangu ....lol!!!!!!
 
njo pm chap chap, nna hamu ya kutongozana... ila utanipa muda nifikirie eeeh?
 
Hii ni kauli maarufu sana kutoka kwa akinadada mara baada ya kutongozwa na akinakaka. Wanajamvi tuelimishane,ni nini hasa ambacho hufikiriwa na akinadada kabla ya kukubali au kukataa kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi?

nipe muda nifikirie ntarudi ku comment.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…