Nionavyo mimi

mtweve

Member
Joined
Mar 28, 2009
Posts
96
Reaction score
8
Baada ya mkutano mkuu wa CCM,wakaagizwa na mwenyekiti wao kuwa pamoja na mambo mengine kuwa mawaziri waweke utaratibu wa kuwaambia wananchi yale 'mazuri' waliyo fanya. Hapa nikakumbuka usemei usemao " matendo huongea vizuri kuliko maneno". Inawezwekama mimi ndio mpofu katika hili,Kwa maoni yangu sidhani kama unahitaji useme ulichokifanya kama ulichokifanya kinaonekana.
Kwa mfano,Zahanati imejengwa,dawa zipo,wahudumu wapo,huhitaji uwaambie watu kuwa umejenga zahanati,watajua tu kwa kuwa wanaona.
Ushauri wangu,CCM wangetumia muda mwingi kufanya mambo ambayo yatajieleza yenyewe tena bure,na si kutumia mamilioni ya fedha kueleza mambo ambayo yana uwezo wa kujieleza
 
Ndugu yangu hizo ni dalili za magamba kuachia ngazi kwani wamesha firiska kifikra na hawana jipya la kufanya zaidi ya kutapa tapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…