Nionavyo Mimi, ( Tafadhali soma na changia) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nionavyo Mimi, ( Tafadhali soma na changia)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Elisha, Feb 10, 2011.

 1. E

  Elisha Member

  #1
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Heshima zenu wapendwa!

  Hili nalo linanichanganya mwenzenu sijui kama mwenye kuweza kunisaidia.

  Kwa mtazamo wangu mimi nadhani wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni wengi kuliko kazi wanayofanya. Wanasema 'two heads are better than one' lakini kusema kweli bunge letu halina tija na ni mzigo mkubwa sana kwa nchi.

  Jambo linalonikera zaidi ni pale baadhi ya watu wanapoitetea serikali kana kwamba hawaoni uozo uliopo. Napata shida sana kuamini kama ni watanzania au ni mawazo mgando ndiyo unaowasumbua.

  Jamani tushirikiane kuikomboa nchi yetu. Sioni sababu ya kuwa na wabunge wengi wanaokwenda kulala bungeni au hata kutetea uchafu unaofanywa na viongozi wetu.

  Sitaki kuamini kwamba nchi hii haina tena watu wenye hekima kwamba wote ni mbumbu. Sipendi kuamini pia kwamba hakuna hata mtu mmoja mwenye uchungu na nchi hii ambayo wananchi wake walio wengi wanaishi katika umaskini japo kuna rasilimali nyingi zinazowanufaisha wachache.

  Nawakilisha kwa mjadala, idadi ya wabunge katika bunge la JMT inaendana na utendaji wake?
   
 2. S

  Sinamatata Member

  #2
  Feb 10, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu unahitaji kupigiwa makofi :clap2: inagwa wengine watakubeza!!!!. Hakuna haja ya kuwa na wabunge ambao hata mara moja ni kupindisha ukweli kwa ajili ya kutetea maslai binafsi. Mfano mzuri ni wabunge toka upizani " NCCR na TLP" tuliodhani wamechaguliwa kuongeza nguvu, kumbe kelele zao ni bure. Sikutaja CUF kwa kuwa wao ni wazanzibar kama wanavyojisema. Ninamshanga KAFULILA na CHEYO ambao dhahri walionekana kuanadaliwa kwa kupigiwa makofi na wale CCM.

  Ukweli bunge la sasa linahitaji watu makini na si wababaishaji kama tunavyoona. Mijadala na malumbano yanapindisha ukweli wa nini bunge linatakiwa kufanya. Kanuni na masuala mengine ya udini yanayoanzishwa na CCM na wabunge kutoka vyama pinzani ya chama pinzania ni kutaka watanzania tusahau kudai haki yetu kwa serikali kama vile umeme, barabara, maji, hospitali, elimu n.k ili waendelee kutuibia mapato yetu yatokanayo na kodi za watanzania. Wenye ukaribu akina "Mhe"!!. Kafulila washaurini watambue kuwa CUF walidangajwa wakadanganyika sasa wanataka kuwatumia kupandia migogoni mwao huku bara baada ya Zanzibar kuwekwa chini ya miguu ya CCM.
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu sisi ccm unataka tugawane vp? kazi hizi ndo jinsi ya kupeana ajila, sasa wakipungua wabunge watu wasiokuwa na kazi wataongezeka saana bana!
   
 4. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Well presented thank you!
   
 5. makandokando

  makandokando JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kuna watu wako loyal na chama chao....wanajua ni uozo, ila inawapa chakula na vijisenti, wanasema mkono unaokulisha hau nini sijui......ofcourse uzalendo sifuri hapo.
   
 6. M

  Matarese JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  kwa ufupi hatuna haja ya kuwa na bunge kwa sasa!
   
 7. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  HTML:
  kwa ufupi hatuna haja ya kuwa na bunge kwa sasa!
  TUNASUBIRI MAANDAMANO YA KUMTOA MKOLONI MWEUSI IKULU
   
 8. Dyslexia

  Dyslexia Senior Member

  #8
  Feb 10, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tushirikianeje tuambie? manake uliyoyasema tunayajua sasa hapo kwenye kuikomboa em fikiria zaidi utuambie,mi pia nafikiria!
  Kule bungeni watu wako kwa maslahi yao zaidi,akilala au akikaa bila kuongea yeye analipwa,huwezi ona kazi ila be assured wana lipwa hela nzuri sana!
   
 9. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #9
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Nilishasema Tanzania hatuna revolution square kama tahrir ya Misri? Uozo uko known kifuatacho ni kutoana njiani basi. Mie hadi nsha choka kuchangia hoja hizi za mapinduzi. Nikianzisha thread ya kulishuriz jeshi la wananchi lichuklue nchi thread haikai hata dakika mbili. HAHAHAAaaaa hadi nacheka. JWTZ wakati wenu wa kuandika historia nchini ni huu
   
 10. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Yaaaani, usiseme kuhusu huo mlundikano wa hao jamaa huko mjengoni, jamani!!!!! halafu wengine wanaendelea kuapishwa, eti wabunge maalum, hilo jimbo la maalum liko kona gani ya nchi hii, hao wenye majimbo tu hakuna wanaemuakilisha ila wao wenyewe na matumbo yao, sasa niambie jimbo la maaaalum. heeeeeeeee kweli lakuvunda halina ubani!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 11. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #11
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Their days are numbered..kuna siku tutasema enough is enough..wala siyo mbali
   
 12. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mapinduzi katika nchi zote duniani yalianza katika nyakati kama hizi. Mimi najua kwamba hata hao ambao wanaongea na kutetea uozo uliopo kuna wakati inawauma, kinachowashinda ni mahali walipoingia. Yaani wamejaa kwenye matope ngaaaa! Hawawezi kutoka kabisa.
  Ukiangalia historia ya mataifa yaliyoendelea kuna wakati ambapo viongozi walifanya uozo mkuu. Hapa kwetu tupo katika kipindi hicho cha upotofu, yaani watu wanaona kutofanya kazi ndiyo mtaji, kula kisicho halali ndiyo utakatifu na unyofu wa moyo. Kuwanyanyasa watu ndiyo wema, kukemea wema ndiyo saburi, kutetea mamlaka ndiyo kazi waliyotumwa na wananchi.
  Ninachoona sisi wananchi tunaweza kufanya sasa ni sisi wenyewe kuungana na kufanya kazi zile ambazo tunaweza, mfano kama bara bara ni mbuvo ni bora tukapitisha michango na tukasimamia sisi wenyewe ujenzi wake. Kama hospitali hazitoi huduma nzuri kama jamii tunaweza kuungana na kujenga hospitali zetu na kuziendesha kwa michango yetu tutakayokubaliana kutoa kwa vipindi maalumu. Tunapaswa kuelewa kwamba hatuna watetezi kabisa tumeachwa kama kondoo walioachwa na mchungaji wao. Bila kufanya hivyo tutaendelea kulalamika tu.
   
 13. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #13
  Feb 10, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280

  My comment hapo kwenye red!! Vileviel tunahitaji waandishi wa habari wazuri wanaoweza kuuelimisha umma siyo hawa design za kina Maggid!!
   
 14. d

  donald2011 New Member

  #14
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu nchi hii ni kubwa sana na wabunge ni wachache ndo maana wengine wanaweza kulala kwenye session bila kupigiwa kelele. Tunahitaji wabunge zaidi ili kufikisha uwiano wa wabunge wa Zanzibar yaani kila mbunge awe na watu elfu nane hivi nyuma yake. KUTACHIMBIKA
   
 15. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45


  Well done.
   
 16. Gudlucky

  Gudlucky Member

  #16
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :clap2: Ninachojua, Hakuna malefu yasiyokuwa na ncha, na kila chenye mwanzo kina mwisho wake, Hata hivyo mbio za sakafuni Huishia ukingoni! Alafu, Haki ya mtu haipotei bure........ Watanzania tuna haki ya kula vinavyotokana na nchi yetu lakini hatuvioni...... Tuombe kwa Mungu wachache wanaotafuta haki Bungeni wawe na Nguvu.... Si unajua mtu 1 chadema akiongea itawapasa watu 10 ccm waongee ili kwamba lau waweze kumfikia huyo mmoja! na kwa sababu hiyo wanawafunga kinywa kwa kubadili taratibu za bunge na kuwanyima haki yao!

  Wahenga walisema hayawi hayawi Huwa na Chachu kidogo Huchachua donge zima! Kweli siku zao zinahesabika (Hao mafisadi) Na Hakuna haja ya kuwa na Wabunge wote hao kwa nchi hii!
   
 17. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #17
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni mzigo mkubwa sana kwa taifa hili, kuna wabunge ambao wanawajilisha watu 1000 na wengine hawana watu wanaowawakilisha ni bora tu wamepata ajira.
   
 18. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #18
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Msemo wa "umoja ni nguvu" ni dhaifu sana.

  Kweli Bunge la Tz ni kubwa sana, hakuna tija zaidi ya kupeana ulaji. Na pia uwakilishi ulipaswa kuwa reflected kwenye uwezo wa nchi kiuchumi. Mbona wanadai viko vipaumbele vya taifa (?), sasa wangesubiri kwanza uchumi wao ukue ndo waongeze idadi ya uwakilishi (?)

  Lakini bila Katiba Mpya na uzalendo wa dhati mambo haya hayawezi badilika kirahisi.
   
Loading...