niokoleeni ndoa yangu waungwana

mfu

Member
Apr 6, 2012
74
59
Mke wangu amekata tamaa ya maisha kisa hatna mtoto tunalea WA wengine,tumejaribu njia zote za kisasa na kienyeji kwa miaka6 bila mafanikio,kila anapopata siku zake ni kilio kiukweli hana tatizo lolote la kiafya,nifanyaje jamani nampenda mke wangu namuonea huruma anavuosononeka kiasi natamani nimuache akaanze maisha na mtu mwingine labda atazaa,sina jinsi jamani,IVF tumefanya hamna kitu,nisaidieni jamani labda kuna njia mbadala siijui
 
Poleni sana. Kujipa pressure kiasi hicho pia huchangia sana katika kushindwa kupata ujauzito maana mke na mume huwa na usongo mkubwa wa kimawazo na kila wanapokutana faragha wanachofikiria ni kama tendo lao hilo litakuwa na mafanikio ya ujauzito na wengi wanapoamua kurelax na kumuachia Mungu basi ujauzito hutokea ndani ya miezi sita. Poleni sana.
 
Je umepimwa wewe? Maana usiseme hana tatizo inaeezekana sperm count yako iko chini sana.
IVF ni njia nzuri. Ila na yeye aache kujipa stress mambo haya hayahitaji stress.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa ushauri wangu nawasihi msikate tamaha mahana kuna watu walikuwa kama nyie na wengine zaidi ya miaka yenu kwaiyo fanyeni maombi kwa kumuomba mungu nendeni kanisani kamuone mchungaji wenu mkafanyiwe maombi. Kama mkiamini hayo maombezi ipo siku itajibiwa
 
.......Kati yako na mkeo nani aliambiwa anatatizo la viungo vya uzazi?
 
mkuu pole sana kwa sonono mlilonalo katika familia yenu. nakuomba print hii post mpe mkeo aisome na wewe uiimbe kila siku.

Iko hivi watoto ni baraka kutoka kwa Mungu, hivyo mwanadamu huwez kusema kwamba nataka kuwa nae ila tu huwa tunamwomba Mungu atupe baraka ya watoto.

Mungu ndiye hutupa neema hii na anapokataa pia kutupa neema hii hatupaswi kulaumu manake biblia inasema "" mwanangu usikasirike kuachwa na Mungu wala usishangae kurudiwa nae"" inamaana kama Mungu kaacha kukupa neema ya mtoto basi asikasirike la amshukuru kwa hilo manake hajui Mungu kamkusudia nini.

Yawezekana kabisa Mungu, anajua nini kitakachokuwa hatma yenu mkiwa na watoto, pengine anajua wazi kwamba mkiwa nao wanaweza kuwa mzigo kwenu hadi mkaanza kumlaumu na kumkufuru.

yawezekana pia Mungu anajua muda wake na muda wake haujafika so msimlazimishe wala kuhuzunika bali mshukuruni kwa kuwa mpo hai na mnaish kwa upendo. wakati mwingine mnaweza kujikuta mna amani na upendo kwasababu hamna watoto lkn mkiwa nao ndoa yenu ikaishia hapo.

Hebu msitake kumlazimisha Mungu, wala msitake shetani akasimama kuwashtaki kwa Mungu kwamba ninyi mnamkufuru Mungu. wala msitake shetan akajiinulia utukufu kwamba amewaadabisha hadi mmemuacha Mungu na kugeukia imani nyingine.

nakusahuri sema maneno haya wewe na mkeo kila siku saa nane usiku tena ukiwa umemkubatia.

SEMA'' Mwenyezi Mungu, wewe ndiye unayetawala duniani na Mbinguni, ni Mungu usiyesema uongo na NI mUNGU mwaminifu tena ambaye uaminifu wake unakuzunguka.Nakumbuka maneno yako uliyosema ENENDENI MKAIJAZE DUNIA na hata uliposema NITAKUBARIKI WEWE NA UZAZO WAKO naamini Mungu maneno yako haya ni amini na kweli na kwamba bado yapo mbele zako.

Sasa tunakuja mbele zako sisi kama mwili mmoja tukikukumbusha kwamba hitaji letu la kupata mtoto. mananeo yako yanasema hapatakuwa na tasa wala mwenye kuharibu mimba katika nchi nikupayo, na sisi tunakukumbusha mungu ahadi hizi zitimie katika ndoa yetu. Tunaamini ndoa yenu ni njema manake wewe unasema kila kutoa kuliko kwema na kila kitolewacho kilicho kamili hushuka kutoka juu kwa baba wa mianga kwake yeye hakuna kubadilika wala hakuna kivuli cha kugeuka geuka kama ndivyo Mungu basi tunakusihi mapenzi yako yatimie juu ya ndoa yetu.

Mkumbushe Mungu aliyempa sara mtoto akiwa na miaka 90 mwambie bado hamjakata tamaa manake mkimuangalia sara mnapata ujasiri juu ya uwezo wa Mungu katika maisha yenu.

Nawatakia maisha mema na Mungu akutane na haja ya mouyo wenu. Msilaumu wala kunung'unika manake kila jaribu lina mlango na Mungu hupendezwa na sifa na moyo wa shukrani kuliko moyo wa laumu.
 
Kiuwazi miimi nilikuwa na tatizo la low sperm count,ndo maana tulifanya ivf,tulistore sample nyingine tukatumia kama mara 3bia mafanikio,ndo maana namuhurumia mke wangu anavyoumia,ILA mungu ndo anaejua sababu,asanteni kwa kunipa Moyona namuomba mungu atupe mioyo ya subra,kabla sijamuoa Alisha zaa na mtu mwingine ILA mtoto alifariki na miaka mitatu,ndo inayomuumiza zaidi
 
Je umepimwa wewe? Maana usiseme hana tatizo inaeezekana sperm count yako iko chini sana.
IVF ni njia nzuri. Ila na yeye aache kujipa stress mambo haya hayahitaji stress.

Kweli mnapokuwa faragha yatakiwa kutuliza akili mlipo na mnachokifanya, pia maombi ni muhimu.
 
Kiuwazi miimi nilikuwa na tatizo la low sperm count,ndo maana tulifanya ivf,tulistore sample nyingine tukatumia kama mara 3bia mafanikio,ndo maana namuhurumia mke wangu anavyoumia,ILA mungu ndo anaejua sababu,asanteni kwa kunipa Moyona namuomba mungu atupe mioyo ya subra,kabla sijamuoa Alisha zaa na mtu mwingine ILA mtoto alifariki na miaka mitatu,ndo inayomuumiza zaidi
wakati wa Mungu bado haujafika, kuwa na low sperm count ni sababu lkn pia inaweza isiwe sababu kabisa manake kama ziko na afya njema na sikapata propulsion force nzuri mbona zinatosha kuchavusha yai??

hivi mkeo amewah kujiuliza kwanini Mungu aliamua kumchukua mtoto ambaye alikuwa amempa mwanzoni?? je amewah kujiuliza juu ya ukuu wa Mungu katika hili?? Binafsi kwa jins unavyonieleza naona kuna ukuu wa Mungu wa ajabu ambao sidhan kama tunapaswa kuanza kulaumu bali kumshukuru.

Muda mwingine ni busara kushuru Mungu hata kwa yale tuyaonayo ni magumu manake Mungu hujua kuliko sisi kwanini anayaruhusu haya na ni zaid ya uwezo wetu kibinadamu.
 
Ngoja arudi aje kujibu kama naye kapimwa kwa kina ili kujua mwenye tatizo si yeye.

Je umepimwa wewe? Maana usiseme hana tatizo inaeezekana sperm count yako iko chini sana.
IVF ni njia nzuri. Ila na yeye aache kujipa stress mambo haya hayahitaji stress.
 
Aisee pole sana hebu badili hiyo ID yako kwanza nina shemeji yangu ana holi tatizo na yeye umri umeenda nikamshauri sababu anakaa huko nchi za wenye akili afanye sperm donation mara mbili tatu them a emplant kwa mkewe wakasema watafanya japo ni ghali sana ,najua inakatisha tamaa ila mwombeni mungu pia
 
Punguzeni usingo; fanya tendo kwa lengo la kujiburudisha kazi ya kuumba ni ya mwenyezi ninyi ni kumuomba.
Siku zile zenyewe hakikisha huchoki hamna msongo na ikiwezekana mhame mkajipumzishe hotelini mle maisha mtafanikiwa
 
Mtapata tu mtoto. Nitajie chakula chako kwa wiki 1, niandikie nini unakula kuanzia asubuhi mpaka usiku kila siku kwa muda wa wiki 1. Fanya hivyo usidharau kwani mimi huwa nafundisha kwa mifano.

Mke wangu amekata tamaa ya maisha kisa hatna mtoto tunalea WA wengine,tumejaribu njia zote za kisasa na kienyeji kwa miaka6 bila mafanikio,kila anapopata siku zake ni kilio kiukweli hana tatizo lolote la kiafya,nifanyaje jamani nampenda mke wangu namuonea huruma anavuosononeka kiasi natamani nimuache akaanze maisha na mtu mwingine labda atazaa,sina jinsi jamani,IVF tumefanya hamna kitu,nisaidieni jamani labda kuna njia mbadala siijui
 
Ngoja arudi aje kujibu kama naye kapimwa kwa kina ili kujua mwenye tatizo si yeye.
nilipima mkuu tena India tukiwa na wife kila kitu chske kipo safi mimi ndo nilikuwa na tatzo
 
Funguka zaidi hapo kwenye rangi watu wakusaidie kwa ushauri kama unahitaji ushauri.

nilipima mkuu tena India tukiwa na wife kila kitu chske kipo safi mimi ndo nilikuwa na tatzo
 
mfu , kwanza jina ambalo umejipa hapa ni la kukata tama sana, kwanini ujiite MFU? Please mtegemee Yesu Kristo nawe utashangaa na kujishangaa. Barikiwa wewe na mkeo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom