Ninunue lori ya kichina 0 KM au Scania used from Saab Scania

Mnyukano wa michango ni mkali sana. Sijui mwisho wa siku utaamuaje ?

Na bado hajatokea mjinga achangie kwa kukuambia chukua Vitz new model! Lazima uchanganyikiwe.
 
Habari natumaini wakongwe mko vizuri

Nina mpango wa kuanzisha kampuni ya usafirishaji nikiwa na mpango wa kusafirisha mizigo kutoka nchini kwenda nchi jirani kwa maana DRC, Zambia, Burundi, Rwanda n.k
(Transit)

Katika kuuliza uliza nimekutana na mawazo makuu mawili ambayo yamekuwa yakinipa mawazo nikaona ni vyema niilete kwenu kwa majadiliano wakongwe

WAZO LA KWANZA

Wazo la kwanza ni kuchukua lori 0 Km kutoka kwa wachina aidha Howo au Faw

WAZO LA PILI

Wazo la pili ni kichukua scania used kutoka saab scania ambapo pale naweza kupata P360 iliyosimama

Trip ni kusafirisha makontena kuelekea maeneo kama vile Congo Kolwezi, Likasi, Lubumbash, Kasumbalesa, Lusaka, Rwanda, Burudi na Malawi

Hivyo basi nataka kujua gari sahihi ambalo wakongwe mtanishauri ninunue kutokana na aina ya safari zangu hizo

Tayari Agent yupo ambaye uhakika wa kutupa tenda za kusafirisha ni uhakika

Kwa kuanza tuna mpango wa kuanza na magari sita (06) lakini upo uwezekano wa kununua mpaka kumi na mbili (12)

UTAFITI WANGU WA AWALI

Gharama za mchina na Scania hazitofautiani sana mathalan kwa mfano ukienda kwa Dr Howo pale kurasini gari N7 na tella lake ambazo ni 0 Km ni $81,000 wakati saab scania used p 360 ni Tsh 150M , ukichukua na tella la superdol na bima na kila kitu ni kama 250M ambayo ni $106,000

MANUNUZI

Mchina:Truck and trailer (both brand new) $81,000
Scania : Used and trailer (brand new) $106,000

MAFUTA

Kwa upande wa mafuta wachina kwenye mafuta wako vizuri kwa maana trip ambayo scania atatumia lita 1900 mchina anaweza kutumia lita 1700 hiyo lita 200 unakuwa umeokoa ambayo ni takribani laki sita (600,000)

Kwa maana mchina gharama za ununuzi ziko chini, uendeshaji ziko chini ila hazidumu sana kwa maana baada ya miaka yako mitano gari kwisha kazi

Ila scania gharama za ununuzi ziko juu, uendeshaji, iko juu ila zinadumu hadi miaka saba hadi nane..

Naileta hii mada kwenu kwamba je niingie kwa mchina au niingie kwa msweeden?

WHY SAAB SCANIA NA SIO KUAGIZA SCANIA KUTOKA UINGEREZA

Watu wamenishauri kuagiza scania gharama haitofautiani iwapo ukaenda kununua saab scania lakini haina guarantee unaweza agiza gari kutoka UK used limetembea km 400,000 ukaanza safari kufika chalinze tu ngoma imesizi, hapo uneshapokea mzigo wa mtu ni lazima ufanye engine overhaul na mambo mengine mengi

Hapo unakuta unapoteza mpaka 9 M kwa engine na fundi etc

Lakini pia kwa upande wa kichina ni kwamba madereva wazuri wanazikimbia sababu ya aina ya magari kiafya sio rafiki kwao hivyo ukiwa na scania kama p360 ni rahisi kupata madereva wazuri kwani talent pool ya madereva wanaotaka kuendesha hizo p360 ni kubwa pia

Hivyo basi naomba kuuliza kwa gari 6 mpaka 12, agent tayari kashakuwa spotted anaweza kutupa kazi trip ni za kwenda Congo Kolwezi, Likasi, Lubumbash, Kasumbalesa, Lusaka, Rwanda, Burudi na Malawi je nishukue mchina au niingie kwa m sweeden naomba kujua sana sana technical know hows za hizi chuma mbili

Maana kuna watu wanashauri kuwa ni bora mchina na wengine wanashauri ni bora m sweeden used

Tayari eneo ambalo nitalifanya kama yard nimesha li spot ambapo ni Kibaha kwa mathias itakapokuwa makao makuu na main yard ya chuma kwa maana agent akikamilisha kila kitu chuma zinaamsha toka kibaha kwenda bandarini kupakia kisha kuamsha...

Natanguliza shukrani

C.T.UView attachment 2566531View attachment 2566532

Ndugu ulinunua lorry aina ipi?
 
Hakuna kitu kama hicho ikifa option ni kununua injini mpya
hebu twende taratibu bro....

Lori au basi la kichina halina kipuri cha ndani ya engine kinachouzwa ???

Yani HOWO na FAW ikichemsha ikahitaji head gasket inabidi utupe engine kwa sababu ya gasket moja ????
 
Fatilia utakuja kunipa jibu.
 
Kwakua unaanza ni bora kufanya risk diversity usichukue zote scania Au zote Mchina.Changanya chukua 2 china the rest scania Au viceversa.Hii itasaidia kukupa experience tena sio ya kuambwiwa Bali kushuhudia Mwenyewe.
 
Habari natumaini wakongwe mko vizuri

Nina mpango wa kuanzisha kampuni ya usafirishaji nikiwa na mpango wa kusafirisha mizigo kutoka nchini kwenda nchi jirani kwa maana DRC, Zambia, Burundi, Rwanda n.k
(Transit)

Katika kuuliza uliza nimekutana na mawazo makuu mawili ambayo yamekuwa yakinipa mawazo nikaona ni vyema niilete kwenu kwa majadiliano wakongwe

WAZO LA KWANZA

Wazo la kwanza ni kuchukua lori 0 Km kutoka kwa wachina aidha Howo au Faw

WAZO LA PILI

Wazo la pili ni kichukua scania used kutoka saab scania ambapo pale naweza kupata P360 iliyosimama

Trip ni kusafirisha makontena kuelekea maeneo kama vile Congo Kolwezi, Likasi, Lubumbash, Kasumbalesa, Lusaka, Rwanda, Burudi na Malawi

Hivyo basi nataka kujua gari sahihi ambalo wakongwe mtanishauri ninunue kutokana na aina ya safari zangu hizo

Tayari Agent yupo ambaye uhakika wa kutupa tenda za kusafirisha ni uhakika

Kwa kuanza tuna mpango wa kuanza na magari sita (06) lakini upo uwezekano wa kununua mpaka kumi na mbili (12)

UTAFITI WANGU WA AWALI

Gharama za mchina na Scania hazitofautiani sana mathalan kwa mfano ukienda kwa Dr Howo pale kurasini gari N7 na tella lake ambazo ni 0 Km ni $81,000 wakati saab scania used p 360 ni Tsh 150M , ukichukua na tella la superdol na bima na kila kitu ni kama 250M ambayo ni $106,000

MANUNUZI

Mchina:Truck and trailer (both brand new) $81,000
Scania : Used and trailer (brand new) $106,000

MAFUTA

Kwa upande wa mafuta wachina kwenye mafuta wako vizuri kwa maana trip ambayo scania atatumia lita 1900 mchina anaweza kutumia lita 1700 hiyo lita 200 unakuwa umeokoa ambayo ni takribani laki sita (600,000)

Kwa maana mchina gharama za ununuzi ziko chini, uendeshaji ziko chini ila hazidumu sana kwa maana baada ya miaka yako mitano gari kwisha kazi

Ila scania gharama za ununuzi ziko juu, uendeshaji, iko juu ila zinadumu hadi miaka saba hadi nane..

Naileta hii mada kwenu kwamba je niingie kwa mchina au niingie kwa msweeden?

WHY SAAB SCANIA NA SIO KUAGIZA SCANIA KUTOKA UINGEREZA

Watu wamenishauri kuagiza scania gharama haitofautiani iwapo ukaenda kununua saab scania lakini haina guarantee unaweza agiza gari kutoka UK used limetembea km 400,000 ukaanza safari kufika chalinze tu ngoma imesizi, hapo uneshapokea mzigo wa mtu ni lazima ufanye engine overhaul na mambo mengine mengi

Hapo unakuta unapoteza mpaka 9 M kwa engine na fundi etc

Lakini pia kwa upande wa kichina ni kwamba madereva wazuri wanazikimbia sababu ya aina ya magari kiafya sio rafiki kwao hivyo ukiwa na scania kama p360 ni rahisi kupata madereva wazuri kwani talent pool ya madereva wanaotaka kuendesha hizo p360 ni kubwa pia

Hivyo basi naomba kuuliza kwa gari 6 mpaka 12, agent tayari kashakuwa spotted anaweza kutupa kazi trip ni za kwenda Congo Kolwezi, Likasi, Lubumbash, Kasumbalesa, Lusaka, Rwanda, Burudi na Malawi je nishukue mchina au niingie kwa m sweeden naomba kujua sana sana technical know hows za hizi chuma mbili

Maana kuna watu wanashauri kuwa ni bora mchina na wengine wanashauri ni bora m sweeden used

Tayari eneo ambalo nitalifanya kama yard nimesha li spot ambapo ni Kibaha kwa mathias itakapokuwa makao makuu na main yard ya chuma kwa maana agent akikamilisha kila kitu chuma zinaamsha toka kibaha kwenda bandarini kupakia kisha kuamsha...

Natanguliza shukrani

C.T.UView attachment 2566531View attachment 2566532
Mkuu piga mixer
 
Back
Top Bottom