Ninje: Nimeleta mfumo Mpya Diamond Formation Tanzania

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
2,360
2,000
Baada ya kilimanjaro stars kuvurunda sana Michuano ya Cecafa wakubwa kocha wa timu Hiyo Ninje akipenda kutumia neno Untill next time ameibuka na kusema watanzania wampe nafasi kwani amekuja na mfumo mpya wa Soka ukiitwa Diamond formation na anataka kuutambulisha Tanzania,kocha huyu tukiiambiwa kafundisha soka Uingereza ila sijui ni timu zipi vile.

Maoni Yangu kwa kocha Ninje na Tff.
Huwezi kutambulisha mfumo mpya kwa wachezaji ambao karibia wanafikia peak/treshold volume ya kucheza mpira ni ngumu kama wanataka kuimplement huo mfumo ni bora kocha Ninje akapewa timu za watoto under 7 hawa ndo wepesi wa kushika vitu ila kwa hawa wakubwa baba utachemka.

Pili elewene Soka linabadilika kila siku,kila siku inakuja mifumo mpya Wabrazil walitambulika kwa kucheza Soka matata aina ya Samba wakipiga pasi nyingi ila siku hizi nao wamebadilika wakicheza mifumo tofauti tofauti kutokana na aina ya matokeo wanayoyataka na aina ya timu wanazokutana nao leo sio ajabu ukiona viungo wa Kibrazil wakipewa Red Card kutokana na Mpira wa Nguvu wanaocheza,tulizoea Wajerumani na mpira wao wa nguvu nyingi enzi za kina Ballack ila siku hizi nao wanacheza soft game kulingana na aina ya wachezaji wao,Gotze,Kroos.nk

Tatu huu mfumo wa Diamond formation ulikua ukitumiwa sana na makocha waliopita pale man utd,Sir Fergie na Moyes kidogo ila baadaye wapinzani waliugundua na kujua njia za kupambana nao ref Man utd vs Ac Milan chini ya mtu katili wa mpira Gennaro Gatuso man utd kidogo wakimbie uwanja siku ile,huu mfumo lazima uwe na winga wenye Spidi kama Bolt mfano Man utd walikuwepo C.Ronaldo,Nani,Valencia,Young..nk enzi za Sir Fergie atleast ulifanya kazi ila kwa Moyes ulifeli Kabisa.

Tff Kama Ninje kaja na mfumo wake tunaomba apewe timu za watoto kwanza huko atengeneze Mawinga wake kwanza,Viungo wenye kupiga pasi ndefu,na beki jamii ya kina Vidic kwanza ndo aje apewe timu za wakubwa.

[HASHTAG]#MpendasokaTz[/HASHTAG].
 
jebs2002

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
7,148
2,000
Kama mchezaji alikuwa na kipaji...
Ukocha?! HAPANA! Tapeli tu..TFF imekula kwao vibaya sana, na wasione aibu, tupa kule, weka anajielewa na sio kutwa kuponda wachezaji na sio kukubali ni kosa lake..
 
inamankusweke

JF-Expert Member
Apr 24, 2014
6,307
2,000
diamond kafundisha mourinho Chelsea awamu ya kwanza na Erikson kwa three lions miaka hyo..ni 3,6,1..inatengeneza umbo LA almasi
 
makaveli10

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
15,377
2,000
Japo mie nampinga ninje ila humu nimeona wengi hawaijui diamond formation, watu wametoa maboko..

Yoyote kwa yote mzee wa always mext time umetuangusha.. umeshindwa kuiingiza mfumo wako kiusahihi kwa wachezaji, hakunaga utetez kwenue mabaya, we tupishe tuu,
Mfumo huo unahitaji muda, na aina ya wachezaji ulionao sioni jinsi diamond itakavyokwenda lazima ufeli tuu hata tukikupa miaka kedekede labda utafute wachezaji wengine.
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
21,325
2,000
Diamond Midfield :

Number 6 ndiye mlinzi mkuu kwenye mfumo huu unaokuwa na viungo 4 wote wakizunguka eneo la katikati, Number 6 atahakikisha walinzi wanne wapo salama muda wote na kuhakikisha anampa room number 10 kucheza na mpira.

Number 10 yeye ndiyo mchezaji muhimu sana, anatakiwa awe na jicho zuri kugawa mpira na awe na uwezo mkubwa wa pasi zenye uhakika ili ziwafikie number 11 na 9, kwenye mfumo huu ticha wetu alimtumia Ajibu kama number 10.

Number 8 na 7 hawa watakuwa wanakamilisha hii Diamond formation, hawa hawatacheza pembeni sana sababu na kufungua uwazi wa kupigwa counter attack.

Wachezaji Muhimu kabisa kwenye huu mfumo ni number 6 na 10. Kwenye mechi tuliyokaa kwa Rwanda alicheza Mkude na Ajib.

Swali: Je Mwalimu ariridhika kabisa kuona mfumo huu umeeleweka hadi utumike kwenye mashindano??

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
24,072
2,000
Yule kocha anambwembwe balaa anasema mimi ni mswahili wa ilala....ila hiki kingereza ni kukaza ulimi tu wabongo msichanganyikiwe.
 
bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
2,360
2,000
Yule kocha anambwembwe balaa anasema mimi ni mswahili wa ilala....ila hiki kingereza ni kukaza ulimi tu wabongo msichanganyikiwe.
Isee Sijui Tff walitumia kigezo gani au kuona anapiga ngeli nini na kusikia kafundisha Uingereza siyo.

[HASHTAG]#Untillnexttime[/HASHTAG]
 
babumapunda

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
4,636
2,000
cv ya huyu kocha ipo vp wakuu,maana tunaeza mlaumu yeye kumbe shida ikawa ni aina ya wachezaji tulio nao
 
Twamo

JF-Expert Member
May 27, 2017
2,175
2,000
Huyu Ninje amefanya watu wamuone kocha Mayanga ni mtu muhimu
 
ZE NDINDINDI

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
1,890
2,000
alikuwa anafundisha under 13 ya Notss county tena akiwa wa nne kwa cheo kwenye academy,lahaula kaja kang'ata ulimi kaongea english mbele ya wale majamaa yaliyokosea kuandika hata community shield yakachanganyikiwa kusikia english yakampa team ya taifa
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
79,198
2,000
Baada ya kilimanjaro stars kuvurunda sana Michuano ya Cecafa wakubwa kocha wa timu Hiyo Ninje akipenda kutumia neno Untill next time ameibuka na kusema watanzania wampe nafasi kwani amekuja na mfumo mpya wa Soka ukiitwa Diamond formation na anataka kuutambulisha Tanzania,kocha huyu tukiiambiwa kafundisha soka Uingereza ila sijui ni timu zipi vile.

Maoni Yangu kwa kocha Ninje na Tff.
Huwezi kutambulisha mfumo mpya kwa wachezaji ambao karibia wanafikia peak/treshold volume ya kucheza mpira ni ngumu kama wanataka kuimplement huo mfumo ni bora kocha Ninje akapewa timu za watoto under 7 hawa ndo wepesi wa kushika vitu ila kwa hawa wakubwa baba utachemka.

Pili elewene Soka linabadilika kila siku,kila siku inakuja mifumo mpya Wabrazil walitambulika kwa kucheza Soka matata aina ya Samba wakipiga pasi nyingi ila siku hizi nao wamebadilika wakicheza mifumo tofauti tofauti kutokana na aina ya matokeo wanayoyataka na aina ya timu wanazokutana nao leo sio ajabu ukiona viungo wa Kibrazil wakipewa Red Card kutokana na Mpira wa Nguvu wanaocheza,tulizoea Wajerumani na mpira wao wa nguvu nyingi enzi za kina Ballack ila siku hizi nao wanacheza soft game kulingana na aina ya wachezaji wao,Gotze,Kroos.nk

Tatu huu mfumo wa Diamond formation ulikua ukitumiwa sana na makocha waliopita pale man utd,Sir Fergie na Moyes kidogo ila baadaye wapinzani waliugundua na kujua njia za kupambana nao ref Man utd vs Ac Milan chini ya mtu katili wa mpira Gennaro Gatuso man utd kidogo wakimbie uwanja siku ile,huu mfumo lazima uwe na winga wenye Spidi kama Bolt mfano Man utd walikuwepo C.Ronaldo,Nani,Valencia,Young..nk enzi za Sir Fergie atleast ulifanya kazi ila kwa Moyes ulifeli Kabisa.

Tff Kama Ninje kaja na mfumo wake tunaomba apewe timu za watoto kwanza huko atengeneze Mawinga wake kwanza,Viungo wenye kupiga pasi ndefu,na beki jamii ya kina Vidic kwanza ndo aje apewe timu za wakubwa.

[HASHTAG]#MpendasokaTz[/HASHTAG].
Kwi! Kwi! Kwi!
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
79,198
2,000
alikuwa anafundisha under 13 ya Notss county tena akiwa wa nne kwa cheo kwenye academy,lahaula kaja kang'ata ulimi kaongea english mbele ya wale majamaa yaliyokosea kuandika hata community shield yakachanganyikiwa kusikia english yakampa team ya taifa
Ha! Ha! Ha!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom