Adelina Johnbosco
Member
- Jun 6, 2016
- 20
- 2
Imekuwa kawaida kwa wavulana wengi na wasichana wakihitaji kuanzisha mahusiano, hutazama mwonekano wa mtu,yaani uzuri na mvuto wa nje, je hii ni sahihi, au hata tabia iangaliwe pia?
itakuwaje endapo mwonekano unaopenda mwisho wa siku hana tabia unayotaka, na tayari umeanza mahusianoMuonekano wa nje unamata kufikia ndoto ya mtu umtakae maana kila mtu ana ndoto za mtu amtakaye kimwonekano lakini hiyo haitoshi tabia ina kuja kuchukua nafasi kubwa sana kuliko muonekano wa nje.
Uhusiano huwa na stages kuna kujuana ama kutamaniana kutokana na muonekano wa nje stage ya pili nikusomana kujuana tabia na malengo ya kila mmoja na stage ya tatu nikukubaliana kuwa wapenzi rasmi sasa uhusiano mwingi wa mtu makini hautazidi stage namba 2 kusomana tabia ukiona mwenzako kitabia haendani na wewe unapiga chini.itakuwaje endapo mwonekano unaopenda mwisho wa siku hana tabia unayotaka, na tayari umeanza mahusiano
Kama kuna kitu maisha yamenifunza ni kua uzuri wa sura unapotea miaka inavozidi kwenda, mdada hata awe na uzuri gani kama hamuendani character miezi michache tu anaanza kuboa, ile sura nzuri sijui inapotelea wapi ghafla, ofcoz sura nzuri mwanzoni inavutia, ila kama ndicho pekee alichonacho kinaisha fasta, siku zote atakuwepo mzuri zaidi yake, hii ni from my experience, wanaume tuna tofautiana lakini. Mimi hakuna kitu kinanivutia kama intelligence.