Nini unaweza kufanya ili mwanaume atimize ahadi alizokupa?

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
1. Msimamo

Kuonyesha upo naye kwenye wakati wote iwe kwenye shida na raha, kwenye changamoto zake na zako. Kuacha ile tabia ya pale unapokuwa unahitaji kitu toka kwake unakuwa mpole ila ukishapata basi umemaliza mjuaji ni wewe.

Kuonyesha huna tamaa za kutaka kila mwanaume na kila kitu uwe wewe tu. Onyesha umetulia ushtushi na mbwembwe za watu na maisha.

2. Onyesha kuwa na nia na unachokusudia

Iwe ni biashara, ndoa, kuwa na maisha bora, kuleta faida ama kusaidia. Basi onyesha unajitenga na matumizi ya ovyo, mawazo povu ya maisha, vitabia vya kukera nk. Mfanye aone ni sifa na hadhi kuwa nawe kwa kuonyesha kweli umekusudia kitu chema. Jitenhe na vyote vitavyokuonyesha wewe huna nia kama kujichanganya na watu asiopenda, kufanya asiyoyataka na kuwa mtu wa hasara kwake.

3. Usiwe mchoyo

Anapohitaji kutetewa basi mtetee, kitu, ushauri, msaada, penzi, nk. kama vipo kwenye uwezo wako fanya. Unaposema unampenda na uwezi kumpa atakacho nalo ni tatizo, siyo wanaume wote ni wavumilivu wa kusubiria au kufumbia macho baadhi ya mambo. Wanaume wanatabia ya kupenda na kushindwa kulazimisha mwanamke wake afanye atakacho badala yake uanzisha mahusiano mapya pembeni ambapo atapata atakavyo.

4. Onyesha una muda naye

Usimtenge, usijifanye uko bize, kujiweka mbali nae nk. Hata kama unamtambua hulka zake, unapohitaji kitu ziweke pembeni ufanikiwe malengo aliyokupa.

5. Mheshimu na mheshimishe

Mkweze aone yeye amefika sehemu sahihi, usimchunge kwa uwazi, muweke wazi kuwa ni shemeji kwa rafikizo na nduguzo, penda kuzungumza naye pale penye gumu katika faragha. Unapofanya haya ni rahisi yeye kuona hekima yako, kukua kwako, uhuru kuwa nawe hivyo ufanya akuamini.

6. Onyesha chochote unachofanya/ utachofanya kina maslahi ya kwake/wote

Kumjali yeye, kumlinda yeye, maendeleo yenu ya baadae, kuogopa kumkosa maishani, kumpa faida, kuwa muwazi katika ndoto zako na unachowaza kukifanya. Mwanaume ni rahisi kutoa nguvu zake na mawazo yake kwenye jambo au kitu chenye kumpa faida.

7. Kuonyesha kupenda waliokaribu naye

Muonyesha mapenzi, jali familia yake kama amekuonyesha, watu wake na kile anachokifanya. Wanaume wengi uolea familia na siyo wao. Sifa zinazotoka huku uzidi kupanda thamani kwake. Mwanaume anaposifiwa alichokichagua moyo wake huwa mwepesi na ukitunza.

8. Jiongeze kimapenzi na kimaisha

Cheza na hisia zake na mitazamo yake ya maisha. Kama hana kitu basi onyesha wewe siyo muoga wa maisha, mpe faraja, mnogeshe kwa mahaba, kuwa mtundu, pendeza, mtege, mvuruge akili kimahaba, onyesha kujali kilichopo, usiwe na papara, tambua muda sahihi wa kukumbushia ahadi ama kuomba kitu. Hii itamfanya aamini wewe ni wake.

9. Kuwa na nadhimu

Iwe fedha, mali, mawazo, vitu,utiifu,maelekezo akupayo yazingatie, utunzaji, ukumbushaji, weka umbali na mambo asiyopenda na usimpande.

10. Kuwa mlezi

Onyesha unajali, unapenda kuwa mke, kuwa mama, mwenye mambo machache, toa bila kuombwa, hata kama huna mtoto, au huna ndoto za kupata mtoto au una tatizo lipo nje ya uwezo wako. Ulezi ni kuweza kuishi na mtu wako.

20230206_120924.jpg
 

Attachments

  • textgram_1675399505.jpg
    textgram_1675399505.jpg
    171.8 KB · Views: 5
Watu wanaogea chumvi hamna kitu,

maji ya bahari hamna kitu,

sala zote za Mama Maria hamna kitu.

Acha nitafute hela zangu mwenyewe.
Mamndenyi, binadamu ni kiumbe mwenye hulka, hatufanani, ila yako mambo kwa asilimia 70 upenda kufanyiwa.
Na hata kwa binti yako anapoolewa ndiyo utayomuelekeza akaishi nayo kwa mumewe. Mengine ni matokeo.
 
Hivi dunia hii yuko mwanaume asiyetaka kufanyiwa hayo na mwanamke?
textgram_1673126351.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom