Wana JF na watu wote wenye mapenzi mema na Tanzania, naomba mnijulishe ni nini tunaweza kufanya kama week ijayo Rais akimteua mshikaji wake E Lowasa kuwa Waziri Mkuu. Au je katiba ya nchi hairuhusu Waziri Mkuu aliyejiuzuru kwa manufaa ya umma kurudi tena kuwa waziri mkuu?
Kama katiba inaruhusu sitashangaa kusikia jina la Lowasa au Rostam linatoka kama waziri mkuu au Waziri katika wizara ya fedha. CCM hawana haibu............
Amekwisha fanya majaribio mengi tu kubwa ni la Wizi wa kura litamshinda la kuwachagua Mafisadi papa? Aendelee kujaribu tu. Kwani jua si linazama.
embu thibitisha kwa data sio maneno . majungu sio issue
Vipi imekuingia kwenye mfupa? Hadi utoboke ndio utasikia uchungu.
tunataka uhakika sio mambo ya kuoneana mkuu .
nitazimia mara tatu lafu asipobadilishwa naenda iringa kulima nyanya