Ni kweli jiwe au mawe yana siri na maajabu mengi, maajabu ya jiwe yamezungumzwa ata katika maandiko ya dini Mbalimbali
Mfano kwenye bibilia tunaona shetani anamjaribu yesu kwakumwambia ageuze jiwe kua mkate, Kwanini jiwe na si kitu kingine.
Daudi anamdondosha Goliath jitu lililoogopwa na jeshi zima la mfalme sauli kwa kutumia jiwe dogo moja tu.
Tazama maandamano ya raia dhidi ya serikali katika nchi za kiarabu, waandamanaji hutumia mawe tu kuiondoa serikali yenye wanajeshi na silaha za moto.
Ata ukikutana na mbwa mkali ukimshikia jiwe au Fanya kama unaokota jiwe atakimbia kuliko ukimshikia fimbo ama silaha nyingine.
Katika msikiti mtakatifu wa majeshi kuna jiwe jeusi (Hajarul as wad) inaaminika kwa kuligusa ama kulibusu basi unaweza kupata hitaji la moyo wako.
na linapozungumziwa jiwe watu wa daressalaam hawataelewa maana ata ukimtuma Mtoto niletee jiwe anakuletea kipande cha Tofali hapa tunazungumzia natural rock.
Kwahiyo ata hilo la kuweka jiwe mfukoni ukanuwia haja isishuke adi ufike unapotaka naamini kabisa.
Ata madini yenye asili ya mawe mfano almasi Rubi tanzanite hutumika Sana kiimani kuliko madini yakuyeyuka mfano dhahabu Silva nk