Nini sababu ya damu kwenye kinyesi

Nini sababu ya damu kwenye kinyesi

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,788
Reaction score
5,027
Leo nilikuwa chooni nikatowa haja kubwa
Ambayo ilikuwa mgumu kutoka niliteseka saana kutowa sasa baada ya kutoka nika cheki kinyesi changu Nikaona damu ambayo ipo kwenye kenyesi haikuwa nyingi ni ndogo ilikuwa kama imejipaka kwenye kinyesi
Nini sababu ya ivo
 
Pole maana ulianza na makalio kuwa makubwa, sasa hivi nyaa plus damu..
Screenshot_20220924_194816.jpg
 
Mkuu hiyo inaweza kusabanishwa na choo ngumu kama ulivyosema, mzigo unakuwa mgumu sana hadi kusabanisha kukwangua njia ya haja kubwa.

Kuepuka hili jitahidi usile chakula kizito usiku, kula mlo kamili; mboga mboga, matunda, juice na maji ya kutosha.

Ukizembea kwenye hili unaweza kusabanisha au tayari unaweza kuwa na bawasiri (hemorrhoids):- kinyama kilichoota kwenye njia ya haja kubwa, choo ngumu inapopita hapo hupasuka na kusabanisha damu kutoka.

Kwa ushauri zaidi nenda kituo cha afya mkuu.
 
Leo nilikuwa chooni nikatowa haja kubwa
Ambayo ilikuwa mgumu kutoka niliteseka saana kutowa sasa baada ya kutoka nika cheki kinyesi changu Nikaona damu ambayo ipo kwenye kenyesi haikuwa nyingi ni ndogo ilikuwa kama imejipaka kwenye kinyesi
Nini sababu ya ivo
Inaonyesha unapata choo kigumu na una maradhi ya bawasiri ya ndani nenda hospitali ukatibiwe usipo pona nitafute kwa wakati wako ili niweze kukutibia maradhi yako upate kupona uguw apole.

(HEMORRHOIDS)

Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.

Kuna aina mbili za Bawasiri
Nje:


Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.
Ndani: Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.

Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.

Je bawasiri husababishwa na nini?

Bawasiri husababishwa na;

  • Tatizo sugu la kuharisha
  • Kupata kinyesi kigumu
  • Ujauzito
  • Uzito kupita kiasi (obesity)
  • Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
  • Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
  • Umri mkubwa

Dalili za bawasiri


  • Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
  • Maumivu au usumbufu
  • Kinyesi kuvuja
  • Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa

Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri


  • Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
  • Strangulated hemorrhoids


786813_f260.jpg



Vipimo na uchunguzi




  • Digital rectal examination
  • Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
  • Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)

Matibabu

Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri

  • Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
  • Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
  • Coagulation (infrared, laser and bipolar)
  • Upasuaji;
    • Hemorrhoidectomy
    • Stapled hemorrhoidopexy

Njia za kuzuia Bawasiri


  • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
  • Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)
  • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.Dr.Henry Mayala
 
Back
Top Bottom