Nini , nani, kivipi, wakati gani, kwanini, iweje ?


Mtazamaji

Mtazamaji

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
5,971
Likes
44
Points
0
Mtazamaji

Mtazamaji

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
5,971 44 0
Viulizo hivi watu tunavitumia kwakujua ama kutokujua katika kufanya mambo mbali mbali kama

  • Kwenda kazini, Kutongoza , nk teh teh teh teh

  • Kufanya maamuzi kama kuchagua kati ya kutembelea mikumi au Serengeti , Zanzibar, nk
  • Kununua vifaa kama kati ya laptop ya Toshhiba , HP, DELL au aina ya gari
Hivi viulizo vitumike wakati gani

Kwa mambo madogo madogo hatuna utaratibu maalum lakini tunajikuta tumefanya maamzi tukizingatia vitu fulani bila kufuauta mpangilio au bila kufuata uzito(Priority)
Lakini linapokuja suala la mambo ya msingi, stratetic (ya muda mrefu),mambo yanayogharimu kiasi kikubwa cha pesa au muda(manhour) au maarifa basi ni muhimu kuwe na utaratibu na njia ya muhusika kupata majibu kulingana a uzito wake na kufuta mpangilio anaaaona unafaa
Katika IT kuna mifumo na taratibu za kisasa ambazo katika somo linaloitwa kwa jina la kitaalama kama System Development Methodologies .Sio lengo la makala hii leo.


Nitakachoaribu kufanya ni kuweka kamfumo ka vimwasali vya kizushi lakini vya msingi ambavyo mtu yeyote aayetaka kuwa na "project" yeyote iliyo serious anatakiwa afuate. Ni kamfumo ambao tofauti na njia ngumu na ndefu za kitaalam za IT hata mtu asiye kuwa mtaalama wa mambo ya dot.com anaweza kuelewa na kuutumia. Ni mfumo utamsaidia mtu kufanya maamuzi bora. Ni ka mfumo unaweza kupunguza risk .Kwa neno moja tunaweza kusema maswali hayo tuyaite MCHAKATO

Tutumie mfano wa kuanzisha system ya TOVUTI /BLOGU

Hivi leo kila mtu anaazisha au anafikiria blog na tovuti, wengine zaidi ya kutumika kama chombo cha taarifa na maarifa lengo ni kupata "mshiko" aka Pesa kutoka kwenye tovuti au blog yake. Wengine wanataka kupata japo vistors 200. Lakini je kabla ya kuansiha blog/ Tovuti tunatakiwa kujiuliza au unatakiwa kujiuliza maswali gani?
Katika kuanzisha tovuti/blog swali la WAKATI GANI japo ni muhimu halitakiwi kupewa msisitizo na umuhimum wanzoni sana kiliko maswali mengine. Maswali ya muhimu kwa mtu nanayetak kuanzisha system mpya kama blog ni kama a


Maswali yakujiuliza kuhusu system


Kwa nini (WHY) naanzisha system hii fulani. Hata kama sio Tovuti ukitaa kutengezakitu chochote au kuazisha hata bishara yeyte hili ni suala muhimu ulipatie jibu na mjibu ya msingo. Kifupi ni Lengo ( Objecives and goals)
Kwa nini ni muhimu kufanya mradi huu?
Nani au kina nani watawezesha project au susytem hii anzishwe na uamilika kabla ya kutumika ? – Human resrces
Vitu gani vitahitajika – Web server , Host.worpress au blogspot. Pesa


MASWALI YA KUJILIZA KUHUSU WALENGWA WA SYSTEM HUSIKA YAANI WATUMIAJI


ISuser1.jpg
nani, yuko wapi

kina nani wanatarajiwa kuwa watumiaji wa system ikikamilika – Rika na umri (Age group), taaluma au elimu
Jinsi gani au kivipi watumiaji watarajiwa atafahamu uwepo wa system hii?Utatangaa redioni, kwenye TV ,kwenye shule au kwenye tovuti ?
Wakati gani hasa watumjai watatratjiwa kutumia system hii sana

MASWALI YA KUJIULIZA KUHUSU WASHINDANIcompetotor-150x150.jpg

Nani au kina nani ni washindani wa system hii? Mapungufu na nguvu zao zikoje
Jinsi gani system yao ilivyo.System yangu iweje ili iwe bora zaidi au tofauti
Nini walifanya na kinawafanya kufanikiwa na Nini inawafanya walaumiwe na watumiaji ?

MASWALI MENGINE

Kivipi system itapenya na ujuliana kwenye soko? Je kuna umuhimu wa kufanya sabotage .PEPSI COLA vs COCA COLA inasemake wamewahi kutumia mbinu hizi wa njia za kificho ili kuharibu bidhaa ya mshindani wake.
MWISHO

Maswali na majibu kama haya tunayafanya lakini inawezekana hatuyaweki kwenye maandishi . kwa hiyo mara nyingine tukitaka kuazisha kijimradi,na kufanya mamauzzi makubwa ua kuwekeza pesa nyingi tukae chini tafute kijitabu kitachokuwa na kumbukumbu za maswali na majibu kama haya na mambo mengineyo kuhusu maamuzi au mradi wako iwe ni BLOG, TOVUTI, NDOA, KUNUNA GARI n.k

YAAAANI NENO MCHAKATO NA UTARATIBU WAKE NI MUHIMU KWENYE PROJECT YEYOTE MAKINI

Mtazamaji kaandika chapisho hili pia kwenye Ka Blog kake ka mazoezi
 

Forum statistics

Threads 1,235,314
Members 474,525
Posts 29,217,809