Nini maoni yako kuhusu video assistant Referees?

Southern Highland

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
8,393
2,000
Haki kweli inapunguza mchecheto wa ushangiliaji. Though inaleta usawa pale madhambi yanapotokea. Yaan badala ya mtu mwingine kuonewa. Sijui nini kifanyike
 

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,837
2,000
Tumpe Malinzi awamu ya pili atuletee hapa hiyo system kwa haraka.

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
malinzi ameingiaje huku? anahusika vipi ?
IMG_20170619_092503.jpeg
IMG_20170619_092503.jpeg
 

Hansss

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,371
2,000
Ni ujinga mkubwa wa teknolojia hiyo yaani inaboa mfano ureno peoe alifunga goli wakashangilia, zaid ya sek 40 wanasubiri majibu afu unaambiwa sio goli yaan inakera sana mpira ni mbinu ili ushinde game
 

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
54,572
2,000
Baada ya miaka kadhaa itakuwa sawa tu, ubongo wa mwanadamu huwa unahitaji kuzoea jambo jipya kabla ya kuliafiki...

Miaka mingi iliyopita mchezo wa mpira wa miguu haukuwa na offside, na pale sheria hiyo ilipoanzishwa kulikuwa na malalamiko mengi maana ilionekana ya ajabu lakini ilitumika na inaendelea kutumika (Nadhani ndio sheria iliyofanyiwa mabadiliko mengi na imekuwa ikiwasumbua sana waamuzi)

Sisi wengine tuliozoea kutazama na kufuatilia michezo kadhaa kama mpira wa kikapu, mpira wa wavu, riadha, tenis n.k tumeshazoea kuona mchezo ukisimama na mwamuzi kujiridhisha kwa kutazama marudio mgando ya picha...
 

mojave

JF-Expert Member
Apr 30, 2016
5,564
2,000
fifa imeanzisha rasmi matumizi ya video assistant referees kwenye michuano ya mabara
utaratibu huu umezua maoni tofauti kwa wadau
View attachment 527175
cha ajabu timu inaweza funga goli na kushangia alafu linakataliwa mnaonekana kama maboya
kuna watu wanasema sheria hii inaondoa msisimko
nini maoni yako mdau?
Kikubwa waboreshe tu, refa asiwe uwanjani awe kati ya hao wenye video ili msisimko ubaki pale pale kama mwanzo.
 

pangalashaba

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
1,234
2,000
Tutaizoea taratibu ndugu zangu wapenda soccer.. Hii technology inatumika pia kwenye NBA na msisimko umebaki palepale.. Cha msingi ni kuondokana na uonevu na maumuzi tata ndani ya pitch!!!!
Hongereni sana FIFA.
 

yellow wall

JF-Expert Member
May 25, 2017
648
250
Naiunga mkono hii technology kwa asilimia zote, haya ni mapungufu madogo madogo ambayo marefaa nina uhakika watayafanyia marekebisho.

Mwanzoni wakati inaingizwa kwenye mchezo wa Rugby pia kulikua na malalamiko chungu nzima lakini yakafanyiwa marekebisho saiz tuna enjoy tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom