Nini mamlaka ya askari barabarani!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini mamlaka ya askari barabarani!!!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by ngoshwe, Apr 11, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Tujadiliane kwa kueleweshana kisheria katika haya ambayo yamekuwa kero kwa baadhi yetu tukiwa barabarani: NINI Mamalaka ya askari na haki ya raia??

  Polisi akiwa barabarani


  • anatokea ghafla kichakanina kusimaisha , anakueleza amekumulika na kamera yake ya "Closed Circuit TeleVision "CCTV" ya mkononi" imekuona ulikuwa katika mwendo kasi ambapo kwa eneo hilo haliruhusiwi kisheria kwenda kwa spidi hiyo. - Je, ukibishana nae, kilelezo hicho cha kamera kinanguvu ya kisheria??., , Je kipimo hicho cha kumulika kinavilelezo vyote vya kina kuitambua gari yako??
  • Anakueleza yeye ni askari, yupo kazini, japo katika mavazi ya kiraia au mwenye mavazi ya kawaida (sio yale meupe ya kama wa Usalama wa Barabarani) anakukamata anasema umevunja sheria barabaraini na anakutaka haraka mwende kituoni au lah, mmalizane hapo hapo.
  • anakupunga mkono ukiwa barabarani, ukisimama anakuangalian usoni, anakueleza kuwa umelewa sana kwa kukuangalia tu usoni tu na kukuambia husitaili kabisa kuendesha gari lako na anakuambia paki pembeni na umkabidhi funguo.
  • anakukamata, anakuambia umevunja sheria hivyo, uende nae kituoni na kama unajifanya una haraka, anachukua kadi ya gari na lesini yako na kukueleza utavikuta kituon fulani ukimaliza mambo yako.
  • anakukamata, anasema ulitenda kosa la kuenesha vibaya wiki iliyopita, na wale waliokuona walikulipoti kituoni hivyo unatakiwa kupeleka gari kituo cha polisi.
  • anakukamata anasema paki pembeni, anaingia katika gari yako na kukuambia haya twende kituoni haraka pasipo hata kujitambulisha vizuri yeye ni nani.
  • anakupunga mkono, ukisimama anaingia katika siti ya abiria na kukuamuru ebu endesha kwa kasi sana tuifukuzie ile gari pale mbele imevunja sheria...
  • Anakukamata kuwa huna lesini,unapomweleza umeisahau nyumbani , anasema umetenda kosa kubwa naakuandikia faini au kukutaka uende kituoni haraka kwa ajili ya kukufungulia mashtaka au mmalizane.
  • anakukamata, anakuambia umevunja sheria za barabarani, na umpe mara moja funguo wa gari, anakupkonya na anaingia upande wako na kukuelekeza ukae kiti cha abiria nae ili mwende haraka kituoni.
  • anakuikuta gari yako labda umepaki ssehemu isiyoruhusiwa, anachoma kibao cha namba (plate number) na kuondoka nazo akiwaeleza wale waliokaribu kuwa ukija wakuleleza kuwa ukifuatilie kituo fulani cha polisi.
  • anakupunga mkono na ukisimama anakueleza yeye ni polisi, wa usalama barabarani yupo kwenye msafara wa kiongozi, au yupo katika operesheni fulani hivyo umepeleke haraka sehemu fulani ili awahi awahi kazini....
  [​IMG][​IMG]  [​IMG]
  [​IMG]


  [​IMG]

  [​IMG]
   
Loading...