GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,645
- 10,867
Asali mbichi ya nyuki wakubwa.Mkuu ni asali ipi unayoiongelea 🤔
Nimekusoma mkuuAsali mbichi ya nyuki wakubwa.
Changamoto ni kwamba ni tamu! Naipenda sana ladha yake!Evsrything too much is harmful.
Fanya kwa kiasi mkuu.
Siku hiyo nilikuwa maingira ya nyumbani.Duh hata kazin unaenda nayo
Kuna mdau alishasema sukari ya kwenye asali ni tofauti na ya kiwandani. Kwamba, yenyewe Haina madhara kama ya kiwandani. Ukweli ni upi?Usisahau kwamba asali ni chakula jamii ya Carbohydrate (Fructose & Glucose), madhara ya matumizi ya asali katika mwili yanafanana na madhara ya matumizi ya vyakula vingine vyenye sukari.
Kisukari.Naipenda sana asali, hasa asali mbichi. Ni tamu, na ina faida za kiafya. Je! Kuna ubaya endapo nitatumia kiasi kikubwa cha asli mbichi?
Nimejiwekea utaratibu wa kutumia asali mbichi mara kwa mara. Mwanzoni nilikuwa nikitumia Kwa siku chache mfululizo, kisha naacha kipindi kirefu kipite bila kuitumia. Lakini kwa siku za hivi karibuni, nimebadilisha utaratibu. Nimekuwa nikitumia kila siku, kiasi kwamba imeshakuwa kama moja ya viburudisho vyangu.
Kwa sasa, ninatumia Asubuhi mara tu ninapoamka, kabla ya kupiga mswaki, na Usiku muda mfupi kabla ya kulala!
Changamoto imekuwa kwenye kujipimia! Nilikusudia niwe natumia kijiko kimoja Asubuhi na kimoja Usiku, lakini mara nyingi nimekuwa nikitumia zaidi ya vijiko viwili kwa wakati mmoja. Kwa siku nzima, kuanzia Asubuhi mpaka Usiku, naweza nikatumia mpaka vijiko Sita vya chakula vilivyojaa asali.
Kuna siku nilitumia karibia nusu kikombe, kama si zaidi, ila kidogo kidogo. Niliiweka mezani nikawa naitumia kidogokidogo huku nikiendelea na shughuli zingine!
Je! Utumiaji wa aina hiyo unaweza ukawa na athari mbaya?
Wewe ulifikri asali gani?😁😁Nimekusoma mkuu
Nashukuru. Kiasi gani kwa mkupuo? Ni sawa nikitumia alau vijiko viwili Usiku na viwili Asubuhi? (Vijiko vya chakula)Kisukari.
Glycemic index ya asali ni karibu sawa na ya sukari. Tumia kwa kiasi
Kila kitu kina madhara kama kisipofanywa kwa kiasi.Kuna mdau alishasema sukari ya kwenye asali ni tofauti na ya kiwandani. Kwamba, yenyewe Haina madhara kama ya kiwandani. Ukweli ni upi?
Si rahisi kusema utumie vijiko vingapi kwa sababu kiafya matumizi ya sukari ya ziada (added sugar/free sugar) unayoipata kwenye bidhaa zilizowekewa sukari, na asalli, yanatakiwa yasizidi gram 36 kwa mwanaume na gram 24 kwa wanawake na watoto, changamoto ni bidhaa zetu nyingi ikiwemo asali, soda n.k hawaandiki ina kiasi gani (gram ngapi za sukari).Nashukuru. Kiasi gani kwa mkupuo? Ni sawa nikitumia alau vijiko viwili Usiku na viwili Asubuhi? (Vijiko vya chakula)