Zipo maana mbili za unyonge, ya kwanza ikimaanisha yule mtu wa chini kabisa wa kijijini mwenye kuishi ndani ya nyumba za nyasi, aina hii inaanza kutoweka kwani maendeleo na vitu muhimu kama maji na umeme vimeanza kufika huko.
Maana ya pili ni mtu anayenyimwa haki zake, anayo haki ya kupata hati ya ardhi lakini anazungushwa kila kukicha, anayo haki ya kupata huduma fulani lakini anazungushwa pasipo sababu za msingi.
Ili kuielewa dhana ya unyonge ni lazima kwanza iwepo dhana ya uonevu, lazima iwepo dhuluma.