Nini maana ya Scatter File?
Scatter file ni aina ya file lenye format maalum ( huwa na extension ya .txt ) ambalo hutumika na program ya SP Flash tool katika kuflash simu zenye chipset za Mediatek ( NB: Scatter file inaweza pia kutumika na program nyingine kama vile za mabox ya kuflashia ila SP Flash Tool ndio official program kutoka Mediatek ). Kwa hyo program yoyote ile inayosoma Scatter file kwa ajili ya kuflashia simu iwe SP Flash au nyingine lazima iwe ina uwezo wa kuelewa format ya hili faili kwanza ili kuweza kulitumia katika kuflash.
Scatter file lina umuhimu gani?
Kwa kawaida sim inabeba memory ndani yake iitwayo ROM ambayo hubeba mafaili mbalimbali ndani ya simu, ROM hizi huja kwa size mbalimbali kutokana na simu 4GB,8GB,16GB n.k. Ili kuweza kutumika, ROM hii hugawanywa katika vipande mbalimbali viitwavyo partition na kila partition inabeba aina ya mafile yake, partition nyingine hubeba mafaili maalum kwa ajili ya sim tu na nyingine ni kwa ajili ya kuhifadhi mafaili yako ya kawaida. Mfano wa partition kwenye zilizopo kwenye scatter ni kama preloader, system, cache, boot na userdata. Umuhimu wa scatter unakuja pale katika kuflash, Je file lipi liende katika partition ipi? Hapa ndipo scatter inajibu hili swali kwani hubeba taarifa ya wapi partition fulani huanza na ina ukubwa kiasi gani. Kwa kutumia taarifa hizi program kama SP Flash tool inaweza kuflash file husika katika partition husika bila kucorrupt simu. Scatter file pia hutumika katika kufanya format ya partition na kufanya readback ambayo hubackup partition.
Wapi tunatakiwa kutumia scatter file?
Unatakiwa kutumia Scatter file muda wowote unapotaka kuflash simu yenye chipset ya Mediatek(MTK) kwa kufeed faili hilo katika program yoyote inayoflash simu za Mediatek mf. SP Flash Tool ili kuipa taarifa program hiyo ya file gani liflashiwe katika partition gani kwenye Firmware file ulilo nalo. Lakini Scatter file haiishii hapo tu kwani hutumika pia katika kazi mbalimbali Zaidi ya kuflash mafaili kama nilivyoeleza hapo juu, linaweza pia kutumia katika kuformat partition husika au kufanya readback.
Namna ya ku backup file kutoka simu nyingine.
Scatter file haikai ndani ya simu ila kuna taarifa kwenye simu ambazo program za nje hutumia katika kutengeneza scatter file, mojawapo ya program ambayo nilikuwa natumia kipindi naflash ilikuwa inaitwa MTK Droid Tool (sijui kama ipo updated au la kwa sababu sijaitumia muda mrefu). MTK Droid Tool yenyewe ilikuwa ikitengeneza scatter file kwa kutumia file la ndani ya simu za Mediatek linaloitwa dumchar_info (lipo katika location ya /proc/dumchar_info ndani ya simu) lakini sio kila simu ya Mediatek ina hili faili kwa hyo njia zingine hutumika katika kulitengeneza kama vile kusoma partition table ya simu.
Haya ni maelezo kwa ufupi ya scatter file ambayo yataweza kukuanzishia safari kama unataka kuendelea kuchimba zaidi. Ukitaka kuelewa zaidi itabidi ufanye kwa practical katika simu na kugoogle kwenye internet