Explainer
JF-Expert Member
- Dec 16, 2015
- 517
- 508
Niweke wazi kuwa takribani njozi nyingi niziotazo na kisha kuendelea kuzikumbuka kwa zaidi ya siku moja njozi hizo huja kujitokeza wazi katika ulimwengu wa vitendo.
Na mara nyingi nimekuwa nikijilaumu kwanini sikuwa naziweka wazi kwa watu hadi pale zinapotokea wazi wazi. Kuna wakati niliamua kuanza kumshirikisha mke wangu baadhi ya ndoto na siku za mwanzo hakuwa akiamini kabisa, lakini baada ya kuona kile nikisemacho kinatokea kweli alianza kuamini na wakati mwingine Kuna baadhi ya njozi zenye kuwakilisha jambo baya kuhusu familia au mtu binafsi basi yeye mke wangu utanguliza kilio kabisaaa kabla hata ya jambo husika kwa maana anajua ni lazima litokee
Turudi kwenye ndoto husika, ambayo nahitaji kuishirikisha hapa jukwaani.
1: WAHUSIKA
Mh Rais wa awamu ya tano akiwa amevalia suti nyeusi, Mimi mwenyewe watu kidogo waliova nguo zenye rangi tofauti tofauti bila kuwakilisha chama chochote cha siasa (hapa ni wananchi wachache waliokuwepo njozini) Askari polisi mmoja mwenye mwili mdogo sana akivalia mavazi yake ya kiofisi (FFU), Askari jeshi mmoja mwenye mwili mkubwa sana akivalia mavazi yake ya kivita, viongozi wachache sana takribani wa tano
2: NJOZI YENYEWE
Kwa pamoja tulikuwa sehemu ambayo haitambuliki kabisa, yaani jangwa si jangwa, mbuga si mbuga, wala sio uwanja wa mpira ama sehemu yoyote ya wazi.
( Ndoto zinatengeneza maeneo ya ajabu sana kwa hakika, hapa nadhani mnanielewa, ndoto zinaumba vitu na maeneo tusiyo yajua wala kuyaona katika ulimwengu wetu huu.
Lakini sehemu hiyo kulikuwa na sehemu ya kukaa viongozi, ijapokuwa hakukuwa na jukwaa lolote zaidi ya turubai ya kuzuia jua. Sasa ikumbukwe kuwa lile eneo halikuwa likieleweka kabisa na japo kuna turubai lakini sikuweza kufahamu kama ni mchana, usiku au asubuhi.
Wananchi walikuwa wachache na wakiwa wamekaa chini mita chache kabisa toka sehemu walipokuwa viongozi.
Kwa upande wangu mimi nilijiona Kama mlinzi eneo hilo na nilivalia mavazi ya kawaida tu.
Nilikuwa naandaa kitu kwaajiri ya kukaa, huku macho nikielekeza mahali alipokaa Mh Rais, wakati huo Rais alikuwa kimya kabisa bila kuongea chochote hata ndoto ilipokata.
Wananchi walikuwa wakilalamika kwa sauti kubwa, wakiwa wanauliza mbona maandalizi yamekuwa mabovu namna hiyo, yaani hapakuwa na miundombinu mizuri katika mkutano ule au sehemu ili tuliyopo.
Sasa wakati hayo yakiendelea pembeni yetu, mara ghafla anaonekana askari jeshi mmoja mwenye nguvu na amevalia mavazi ya vita kanakwamba yupo vitani.
Askari huyo lengo lake ni kwenda kumvamia Raisi, lakini kabla yakumfikia Rais ndipo yule Askari polisi aliyevalia nguo za (FFU) na mkonini ameshika fimbo ya kawaida kabisa na mwenye mwili mdogo sana anatokea na kumdhibiti yule mwana jeshi kwa kumpiga na ile fimbo katika sehemu ya mbele ya uso wake.
Wakati hayo yote yanatendeka sisi watu wengine, kuanzia wananchi na hata Mh Raisi tulikuwa tukiwashangaa tu wale askari wawili.
Hakuna aliekimbia wala kuogopa kila mtu alibaki anaangalia tu kile kilichokuwa kinaendelea kwa wale askari wawili.
Na mwisho wake yule askari mdogo anafanikiwa kumdhibiti na kumwua yule askari mwenye mavazi ya kivita.
Nawasilisha kwa dhati na shukrani kubwa kwenu kwa mawazo na fafanuzi zenu ndugu zangu. Ahsante.