Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Kutaka Zanzibar huru sio kuvunja mahusiano na Zanzibar. Kuna watu wanachanganya mambo. Nimeona watu "wakubwa" wakiwaza "hovyohovyo". Baadhi wanasema Zanzibar ikiwa huru ni kuvunja mahusiano na Bara, jambo ambalo ni baya kwa kuwa tuna muingiliano wa muda mrefu wa jamii hizi mbili. Kuna Wazanzibar wanaishi bara na Wabara wanaishi Zanzibar, wanafanya biashara, kazi, wameoana, wana familia.
SWALI: Je Zanzibar ikiwa huru (yenye mamlaka kamili) ni sababu ya kuvunja mahusiano na bara?
JIBU: Si kweli. Hakuna uhusiano wowote kati ya Zanzibar huru na kuvunjika kwa mahusiano ya jamii hizi mbili. Zanzibar inaweza kuwa huru na mahusiano yetu yakaendelea vizuri. Mbona Kenya ni taifa huru lakini uhuru wao haujawahi kuathiri mahusiano yetu na wao.
Wapo Wakenya wengi nchini wameoa, wameolewa, wanafanya biashara na wengine wameajiriwa nchini TZ kama ilivyo kwa WaTZ wengi waishio Kenya. Profesa aliyenifundisha Logic and Argumentation Skills, aliyenifundisha Critical Thinking na aliyenifundisha Philosophy wote ni Wakenya. Uhusiano wa TZ na Kenya umezidi kuimarika licha ya nchi hizi mbili kila moja kuwa na mamlaka yake kamili.
Sasa kama ndivyo kwanini tunaaminishwa kwamba mamlaka kamili ya Zanzibar itaathiri mahusiano yake na bara?? Zanzibar ikiwa na mamlaka kamili itaathirije Wazanzibar kuishi bara au wabara kuishi Zanzibar? Itaathirije watu hawa kufanya kazi kwa kuingiliana na hata kuoleana?
Zanzibar wakiwa huru mahusiano na bara yataendelea kama kawaida ila kitakachobadilika ni utaratibu tu. Badala ya "free movement" kutakuwa na "Passport". Kwahiyo watu watatumia Passport kwenda Zbar na kuja Bara lakini mahusiano yetu yatabaki palepale. Undugu wetu na Wazanzibar hauwezi kufa kwa sababu eti imekuwa nchi yenye mamlaka kamili.
Uhuru wa Zanzibar si kwenye mahusiano ya kijamii baina yetu na wao (social interaction). Ni kwenye mamlaka kamili ya kuwa na maamuzi katika mambo yao. Yani Wazanzibar wamiliki Uchumi wao, wawe na taifa lao, wapate international recognition (watambulike kimataifa), warudishiwe kiti chao Umoja wa mataifa, wawe pia na uwezo wa kuingia mikataba na nchi nyingine duniani. Wawe na uwezo wa kukopa ktk taasisi kubwa kama World Bank na IMF kwa maendeleo ya nchi yao.
Leo Rais wa Zanzibar akienda nje ya nchi hatambuliki kama "Mkuu wa nchi" na hapewi heshima ya Urais kwa Sababu Zanzibar haina "International recognition". Lakini Zbar ikiwa na mamlaka kamili Rais wake atatambulika kimataifa na atakaposafiri atapewa heshima ya Mkuu wa nchi.
Hii pia itasaidia kuimarisha uchumi wa Zanzibar kwa sababu wataweza kuweka mipango mizuri ya rasilimali walizonazo. Kwa mfano mafuta yaliyogunduliwa ktk upwa wa Zbar, yamewekwa ktk mambo ya muungano. Wakati mafuta ya Zbar yakiwekwa katika mambo ya Muungano, hakuna mchanganuo wa kueleweka unaoonesha Wazanzibar wananufaikaje na dhahabu ya Geita au gesi ya Mtwara.
Wazanzibar wakipewa mamlaka kamili wanaweza kufanya assesment ya mafuta yao, wakajua yapo kiasi gani, wakaamua waanze kuchimba lini, wachimbe kwa miaka mingapi, na yawanufaisheje kwa maslahi yao na vizazi vyao.
Malisa GJ.!