Kwa mtazamo wangu;Kusamehe nafikiri umeuliza kuhusu watu waliokua kwenye mahusiano.Kama ni hivyo kusamehe hapo kuna mambo yafuatayo;1.Kwanza kumsamehe kuhusiana na tukio alilofanya,hapa mtaendelea kusalimiana na story zingine hii haijalish kama amekutafuta kuja kuomba msamaha au hajaja,unamsamehe as binadam kama wewe.2.Hapa tayari umeshamsamehe na umeamua kuwa nae tena kimahusiano,lakini hili hutegemea sana na mkosaji kama ataonesha utayari huo yaani atakutafuta na kukuomba msamaha na kuomba mahusiano yarudi na yeye kuonesha kuhitaji hilo!
Kwa mimi nachukulia msamaha ni lazima nitoe ..kwa imani yangu nisiposamehe nami sitasamehewana bbaba yangu wa mbinguni maana kwa huyu mtu aliyenikosea inawezekana sijawahi kumkwaza/kumkosea lakini haimaanishi kuwa mimi sifanyi makosa au haimaanishi kuwa mimi ni mtakatifu ..msamaha wa kweli hauambatani na masharti..km vile mtu anakwambia nimekusamehe lakini usirudie tena..unasamehe ukiamini mwenzio amejuta ndani yake na anapenda mahusiano yenu ya awali yarudie katika hali yake la sivyo asingesema samahi nisamehe.
Unaposema nimekusamehe hakikisha umesamehe binafsi kama sijaskia kusamehe huwa nakaa kimya na kujipa muda ili nitafute amani coz siwezi kukuonyesha jino kwa kucheka wakati bado nina uchungu nawe kila mtu ana njia zake za kuondoa uchungu na kuanza upya..kuna mwingine anajiskia kulia mwingine anaongea sana kila mtu kwa jinsi alivyoumbwa ..Msamaha lazima uendane na kuacha kurudia kuliongelea hilo kosa ni njia mojawapo isaidiayo kusahau...
Kumwambia mtu ''usirudie tena'' ni sharti ama angalizo??
Kuna ubaya gani kumpa mtu angalizo??Maana hiyo inatumika sana kwa watoto...ni namna ya kumwelewesha mtu kwamba umesamehe alichofanya ila asirudie tena kwasababu sio kitu kizuri. What's wrong with that???
kusamehe ni ku let go kama ulivyosema..
mimi nna ndugu nimewapiga marufuku kuja kwangu ingawa naweza kutuma pesa kuwasaidia..
nimewasamehe lakini sitaki wanikaribie...kabisa.....huko huko walipo
tunakutana kwenye harusi au misiba...basi...hakuna simu wala kutembeleana...
Hata simu? Kwanini lakini?
Mamito hii mada ni pana. Kwangu mimi ninauchukulia msamaha kama kusamehe pasipo doa. Kama ni mwenzi alokukosea unapotamka nimekusamehe kwangu ina maanisha nakusamehe na turudi kama zamani so it means the whole package mydia. Unasamahe na mapenzi yanarudi moto moto as if nothing has happened.
Kama kuna kusamehe na kisha hamuendelei mimi nadhani YAMEKWISHA is more appropriate than NIMEKUSAMEHE. Yamekwisha but kila mtu aendelee na maisha yake. Kwangu mie KUSAMEHE ina maanisha ni pamoja na kuzika na kusahau lililojiori.
Ni nini maana halisi ya kusamehe??
Je ukimsamehe mtu unalazimika kuwa karibu yake tena?? Kurudiana kimapenzi kama ndivyo mlivyokua mwanzo?? Kuongea mara kwa mara kama ndivyo mlivyokua mwanzo? Kutembeleana mara kwa mara kama ndivyo mlivyofanya mwanzo??
Nauliza kwasababu mara nyingi nimeona/sikia watu wakisema ''mi nilidhani umenisamehe/umemsamehe'' pale wanapotaka mambo yarudi kama mwanzo/au hata yawe zaidi na kuambiwa kwamba haiwezekani. Ina maana ukimsamehe mtu moja kwa moja unategemewa/una jukumu la kumchukulia/treat kama vile hilo kosa alilofanya halikuwahi kutokea?
Binafsi naamini kwamba kumsamehe mtu ni kile kitendo cha kuachilia (letting go) kile kilichotokea. Kumruhusu awe na amani..na kufungua ukurasa mpya ambao unaweza ukachagua awepo ndani yake au asiwepo na sio kukifuta kabisa alichofanya na kulazimika kurudi mlipokua mwanzo bila mhusika (mkosewaji) kutaka/penda kufanya hivyo. Yani inawezekana kumsamehe rafiki mwizi bila kumkaribisha tena nyumbani kwako...kumsamehe mke/mume/mpenzi cheater bila kurudiana nae tena..kumsamehe ndugu/rafiki mmbea bila kumshirikisha mambo yako tena. I don't know...inawezekana kwa kufanya hivyo mtu anakua hajasamehe ila ndivyo nnavyoamini na kufanya pia...hata mimi siwezi lazimisha/taka/tegemea mtu niliyemkosea na akanisamehe kurudisha mahusiano yetu ya mwanzo kwasababu tu ameniambia ''NIMEKUSAMEHE''. Ntategemea anipotezee/awe karibu na mimi kwasababu anapenda/taka kufanya hivyo na sio kama jukumu linalofuatana na msamaha wake.
We unaonaje...?
Hata urafiki ni mahusiano...na naongelea mahusiano ya aina yote...kimapenzi..kirafiki..kindugu n.k
Swali...kumsamehe mtu kunahusiana vipi na utayari wako kurudia mahusiano yenu ya mwanzo???
Boss mimi na wewe tupo kwenye ukurasa mmoja...ila naona tunatofautiana na MJ hapo chini.kusamehe ni ku let go kama ulivyosema..
mimi nna ndugu nimewapiga marufuku kuja kwangu ingawa naweza kutuma pesa kuwasaidia..
nimewasamehe lakini sitaki wanikaribie...kabisa.....huko huko walipo
tunakutana kwenye harusi au misiba...basi...hakuna simu wala kutembeleana...
Mamito hii mada ni pana. Kwangu mimi ninauchukulia msamaha kama kusamehe pasipo doa. Kama ni mwenzi alokukosea unapotamka nimekusamehe kwangu ina maanisha nakusamehe na turudi kama zamani so it means the whole package mydia. Unasamahe na mapenzi yanarudi moto moto as if nothing has happened.
Kama kuna kusamehe na kisha hamuendelei mimi nadhani YAMEKWISHA is more appropriate than NIMEKUSAMEHE. Yamekwisha but kila mtu aendelee na maisha yake. Kwangu mie KUSAMEHE ina maanisha ni pamoja na kuzika na kusahau lililojiori.
...kusamehe gharama,....mwj1 nisamehe na mimi basi...lol
...msamaha unategemeana na mhusika na kosa lenyewe...
kwangu mimi inategemeana impact ya kukosewa huko kulivyo athiri maisha yangu.
kuna makosa yanasamaheka na kusahaulika,
kuna makosa yanasameheka lakini hayasahauliki, na
kuna makosa hayasameheki wala hayasahauliki!