Leo Aprili 18, 2025 Kanuni za Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 zimechapishwa katika Gazeti la Serikali kupitia Tangazo la Serikali Na. 249 la mwaka 2025.
Nini Maana Yake?
Taratibu za Chama cha Siasa kushiriki Uchaguzi Mkuu, kwanza ni kuridhia na kusaini Kanuni za Maadili kabla ya kutolewa kwenye Gazeti la Serikali.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Kuchapishwa kwa Kanuni hizo katika Gazeti la Serikali maana yake ni kwamba, Vyama vya Siasa ambavyo Vimetia saini kukubaliana na Maadili hayo ndiyo vitashiriki Uchaguzi Mkuu na Chama cha Siasa ambacho hakijasaini Kanuni hizo kinakosa fursa ya kushiriki Uchaguzi kwa kuwa kinahesabika kama kimeyakataa/hakijaridhia maadili hayo.
Nini Kinaweza Kufanyika?
Kama ambavyo Chama cha ACT Wazalendo leo kimewakaribisha G 55 na wanachama wengine wa CHADEMA wanaotaka kugombea kwenye Uchaguzi Mkuu, fursa pekee iliyosalia ni wanachama wa CHADEMA kutumia fursa ya kujiunga na Vyama vingine kama vile CCM, ACT Wazalendo, CHAUMMA, CUF, NLD na Vyama vingine vilivyokubali kusaini Maadili hayo ya Uchaguzi kwa kuwa hakuna nafasi nyingine kwa CHADEMA kushiriki Uchaguzi Mkuu na Chaguzi nyingine ndogo zitakazojitokeza katika kipindi cha mwaka 2025 hadi 2030.