Nini maana ya hizi picha?

Nini maana ya hizi picha?

Sina chakula, nguo zimeniisha pakutokea napaona ila sina ufunguo/ mtaji
 
Picha ya kwanza inaonyesha watu weupe wakisheherekea harusi ya mpendwa wao.

Pia picha hiyo wanaonekana watu weusi, wanawake kwa wanaume wakifanya/fanyishwa kazi kusafisha/kuokota majani eneo ambalo sherehe ya watu weupe inafanyika. Hapa maana yake ni kwamba jamii yetu/zetu zimetengeneza aina ya maisha ambayo mtu mwenye wadhifa/mali huona kutumikiwa ndio aina sahihi ya maisha. Inawezekana harusi ya hao watu weupe ikasheherekewa na wote bila ubaguzi lakini kama unavyoona msanii ameonyesha weusi wakifanyishwa kazi kwasababu wao hawashahili kujumuika katika furaha. Ni kama viongozi wa kiafrika vile, huona mwafrika maskini hatakiwi kabisa kujua furaha, kuwa na chapaa etc.

Picha ya pili inalenga zaidi mahusiano yalivyo jenga misingi katika chapaa/fedha. Mwanaume anatazamiwa awe financially stable huku mwanamke awe na mwonekano mzuri/wakuvutia. Ni kama tunavyona mitaani ukiwa na mwanamke/msichana then mkatoka you have to pay bills to prove your masculinity. Ni pressure jamii imetengeneza na inaumiza wanaume wasio na vipato vizuri.

Picha ya tatu msanii ameonesha vitu mob. Kwanza picha inaonyesha mtu aliye kwenye mawazo mengi. Tena mawazo hayo ni yakukata tamaa tu. Ndio maana unamwona jamaa ndani amejikalia chini hadi mice wamemzunguka. Ni kama vile masikini awazavyo. Lakini mtu huyu kidogo anaona mwanga kupigia dirisha dogo ambalo linaweza kutafsiri opportunity huyu mtu anaweza ifanyia kazi na akafanikiwa. Tena kuthibitisha ni opportunity nzuri kwenye dirisha kuna ndege/njiwa mdogo anamtazama kana kwamba anamwambia kwanini usijaribu hapa? Lakini pengine jamaa anakata tamaa kuona mbona dirisha lenyewe dogo?

Picha ya mwisho ni aina ya trick inatumiwa kuwahadaa watu wetu kwenye mambo mengi. Bunduki ni ishara ya mauti. Lakini mauwa ni ishara ya upendo na amani. Mara nyingi watu wanaotaka kitu kwako huweza kujidai wao ni msaada mkubwa kwako lakini ni mbwa mwitu ndani ya ngozi ya kondoo. Hii inaweza eleweka kirahisi tu. Mfano mwingine hapa unaweza fit ni siasa za Afrika. Wanasiasa kipindi cha uchaguzi huonekana kama maua. Ndio kama maua vile....wanawapa mananchi kila aina ya matumaini lakini kumbe agenda waliyobeba ndani yao ni sawa na mtu aliyeshika bunduki tu.....anakuhadaa na maneno matamu (maua) ili akumalize bila purukushani.
 
picha ya kwanza ianonyesha matabaka mawili tofauti katika maisha maskini na matajiri
maskini wanaangaika shambani kulima na kuvuna wakati matajiri wanatumia mavuno hayo katika matumizi ambayo si msingi(?)(kwaida jamii nyingi hata za kiafrika hutumia nafaka kuwamwagia wali au maarusi).Watu waliopo hapo wanaweza kuwa watu wa dunia ya tatu hasa Asia (Vietnam/China) na wale wa nchi za magharibi

picha ya pili kuna mwili wa mwanaume mwenye kichwa mithili ya ATM kadi (Visa card) na mwili wa mwanamke mwenye kichwa cha mashine ya kutolea fedha(ATM machine) hiyo ni ishara simple kwamba akili ya mwanamke iko katika fedha za mwanaume na mwanaume ndiye mmilki na mtoahi wa fedha kwa mwanamke.

ya tatu ni mtu aliye na ufukara ambaye anawaza juu ya misha yake yalijaa ufukura(yanwakilshwa na panya,nguo zilizochakaa) wakati huo huo anatamani utajiri(Unawakilishwa na vipande/mirabaha ya dhahabu)

Picha ya nne kuna bunduki,mkono na maua.Bunduki imefichwa nyuma ya maua.Bunduki inawakilisha uadui,chuki na unafiki wakati maua yanawakilisha upendo,amani na furaha na mkono unawakilisha mtoaji.Tafsiri yake ni kwamba mtoaji anaonyesha upendo wa kinafiki ulioja chuki na uadui nyuma yake.Kwa methali ya kiswahili tungesema chui aliyevaa ngozi ya kondoo.
 
Asee si mchezoo nimetoka mtupu wongo m'mbaya.
Kaka Mkuu hiyo ya kwanza ina Maana kuwa kuna watu Masikini wana lima na kupanda Mpunga kwa tabuu ni hao walio inama wamevaa kofia lakini kuna watu wanauchezea ndiyo hao mabibi harusi wanarushiana mchele
 
Ya pili na ya mwisho nimezielewa.
Kaka Bavaria hii ya tatu ina maana kuwa Mawazo yako (kichwa) yanaweza kukufanya mfungwa yaani ukiwa na fikra (mawazo finyu ) basi ww nimfungwa kutokana na mawazo yako mwenyewe
 
picha ya kwanza ianonyesha matabaka mawili tofauti katika maisha maskini na matajiri
maskini wanaangaika shambani kulima na kuvuna wakati matajiri wanatumia mavuno hayo katika matumizi ambayo si msingi(?)(kwaida jamii nyingi hata za kiafrika hutumia nafaka kuwamwagia wali au maarusi).Watu waliopo hapo wanaweza kuwa watu wa dunia ya tatu hasa Asia (Vietnam/China) na wale wa nchi za magharibi

picha ya pili kuna mwili wa mwanaume mwenye kichwa mithili ya ATM kadi (Visa card) na mwili wa mwanamke mwenye kichwa cha mashine ya kutolea fedha(ATM machine) hiyo ni ishara simple kwamba akili ya mwanamke iko katika fedha za mwanaume na mwanaume ndiye mmilki na mtoahi wa fedha kwa mwanamke.

ya tatu ni mtu aliye na ufukara ambaye anawaza juu ya misha yake yalijaa ufukura(yanwakilshwa na panya,nguo zilizochakaa) wakati huo huo anatamani utajiri(Unawakilishwa na vipande/mirabaha ya dhahabu)

Picha ya nne kuna bunduki,mkono na maua.Bunduki imefichwa nyuma ya maua.Bunduki inawakilisha uadui,chuki na unafiki wakati maua yanawakilisha upendo,amani na furaha na mkono unawakilisha mtoaji.Tafsiri yake ni kwamba mtoaji anaonyesha upendo wa kinafiki ulioja chuki na uadui nyuma yake.Kwa methali ya kiswahili tungesema chui aliyevaa ngozi ya kondoo.
Upo sahihi kabisaaa kaka mkuu safiiii sanaaa
 
1: Matabaka ( Wengine wanasherehekea wengine muda wa kusherehekea ni muda wa kuvuja jasho)

2: Wanawake wawezeshwe ( Badala ya kutegemea rasilimali za mwanaume)

3: Ufungwa wa fikra ( Mhusika yupo chumba cha giza ana sare na dirisha dogo linalomuaminisha anaweza kuona nuru akitaka)

4: Kibaraka ( Alieleta maua, atakaefyatua risasi hata haonekani).
 
Back
Top Bottom