MBUZI MWENYE BUSARA
Senior Member
- Nov 24, 2019
- 143
- 160
Heri ya mwaka mpya nawe pia mkuu.Wakuu heri za mwaka mpya!
Kwanza mnisamehe kama nitauliza swali katika jukwaa ambalo silo. Lakini naamini wataalam wapo humu pia.
Niende Sasa kwenye mada; Nimekuwa nikiota usiku nakimbia lakini Mara nyingine naweza kukimbia mwenyewe lakini nisijue nakimbiza nini na Mara nyingine naweza kukimbizwa na kitu kama nyoka au watu wanaotaka kunidhuru. Mara zote huwa nashinda. Lakini pamoja na hivyo style ya kukimbia ndio kilicho nifanya niandike hii thread. Huwa nakimbia kama mshale unaorushwa si kama mtu anayekimbia kwa miguu. Sijui kama nitaeleweka. Yaani nakimbia kwa mtindo kama wa kujivuta.
Nadhani nitakuwa nimeeleweka.
Naomba tafsiri ya hiyo ndoto.
Asanteni
Umeripoti polisi au unasubiri upatwe na janga kwanza?
Kuna uhusiano gani kati ya kulala uchi na ndoto ilihali nina imani?Pia pendelea kuvaa nguo ukilala hata laini kama boxer hivi usilale uchi...
Mkuu nashukuru sana kwa tafsiri. Nadhani niongeze jambo ambalo pia sikuandika mwanzoni. Mimi kwasasa sina gari ila Mara nyingi naota naendesha gari. Hilo nalo naomba unisaidie.Kukimbizwa na nyoka means kuna uadui unakunyemelea kutaka kudhuru maisha yako ya familia au uchumi au afya au vyote maana vinategemeana, kasi ya mshale na inatoa taswira ya nguvu uliyo nayo na unayotumia ni kubwa kushinda challenge ulizonazo, hizo nguvu yaweza kuwa za kiuchumi kiakili kimwili na hata kiroho.
Ushauri wangu ongeza juhudi katika mambo ya kiroho maana hii ndoto ungeitafsiri bila shida... Kama ni mkristo mshike Yesu wako sawasawa, Roho Mtakatifu hutusaidia kutafsiri ndoto na mafumbo magumu tunapohitaji.
Mkuu nashukuru sana kwa tafsiri. Nadhani niongeze jambo ambalo pia sikuandika mwanzoni. Mimi kwasasa sina gari ila Mara nyingi naota naendesha gari. Hilo nalo naomba unisaidie.
Heri ya mwaka mpya nawe pia mkuu.
Katika ndoto inategemea unaamini njia ipi ya kupata tafsiri.Mimi naomba niielezee kidogo kwa njia ya biblia ikiwa imekupendeza.Iyo kuota kuwa unakimbizwa au kukimbia ina maana kuna jambo la hatari ambalo unakuwa unaliepuka na hili linaweza kudhihirika kwenye maisha yako halisi,inawezekana kuna changamoto unakuwa unazipata lakini unazishinda kwa kasi ya ajabu baada ya kujituma sana maana huo moyo unao,mf kwenye biblia Yakobo alipigana na malaika na aliweza kumshinda kwa sababu ile haikuwa mipaka yake lakini kwa bidii alipambana mpaka akapata mbaraka wake (Mwanzo 32:22-31).ivyo ni vizuri sasa kuomba na kung'ang'ania ujue kuna nini katika iyo hatima ya mapambano yako.Yakobo hapo hatima yake ni ule mbaraka na kubadilishwa jina.
Ni hayo tu kwa kifupi.ahsante
Asante mkuu. Mara nyingi huwa naendesha vizuri tu kwa kuonesha kuwa sasa naweza kuendesha maana kwa sasa nina ujuzi kidogo tu. Lakini Mara nyingine napata shida kuendesha kwa kuonesha ule ujuzi mdogo nilionao hivyo Mara nyingine nakuta kigongo lakini naruka lakini sijawahi kukwama.Kuota unaendesha gari means kuendesha maisha yako, je unapokuwa unaendesha can you describe that feeling? Mfano hofu ya kuchelewa kufika uendako, je unafurahia Safari ? Je unaexperince hali gani za kushindwa au kuweza mfano kukata kona au kutokuona mbele, giza mbele? Je unakwama labda mashimo au unagonga kisiki au ukuta Abiria unaobeba wanaupinzani wowote labda kukwambia ongeza mwendo, umekosea njia, punguza mwendo, how do you drive, je unapita njia za maporini, kupanda milima, je ni tambarare makorongoni etc
Asante mkuu. Mara nyingi huwa naendesha vizuri tu kwa kuonesha kuwa sasa naweza kuendesha maana kwa sasa nina ujuzi kidogo tu. Lakini Mara nyingine napata shida kuendesha kwa kuonesha ule ujuzi mdogo nilionao hivyo Mara nyingine nakuta kigongo lakini naruka lakini sijawahi kukwama.
Gari huwa linaweza wakilisha maisha/huduma sasa inategemea kuwa ni gari ya aina gani na rangi ipi.Mkuu nashukuru sana kwa tafsiri. Nadhani niongeze jambo ambalo pia sikuandika mwanzoni. Mimi kwasasa sina gari ila Mara nyingi naota naendesha gari. Hilo nalo naomba unisaidie.