LUCKYHUSTLER
Member
- Jul 9, 2012
- 14
- 11
FIKRA TUNDUIZI 1.
Nini maana ya fikra tunduizi ? ( critical thinking) Je kuwa critical thinker ni lazima ujadili masuala ya siasa? Uchumi ? au mambo ya kisheria ?
LENGO LANGU NI KUKUFIKIRISHA KUHUSU FIKRA PEVU.
Moja ya msamiati ambao umeenea zama hizi za taarifa ni huu unaohusiana na kuwa na fikra tunduizi/ kufikiri kwa kina. Majukwaa mbali mbali yameanzishwa kuwapa watu fursa na changamoto ya kufikiri kwa kina/ fikra pevu.
Think critically, be a great thinker , think big misamiati hii imeenea sana, yote hiyo inaonesha kuwa tatizo la kutokufikiri limekuwa kubwa miongoni mwa jamii yetu. Katika historia ya mwanadamu hakujawahi kuwa na kizazi ambacho kiko connected kama kipindi hichi, teknolojia ya habari na mawasiliano imerahisisha muunganiko wa wanadamu.
Ila pia imeleta tatizo la kutokufikiri, mfano nakuuliza nini maana ya fikra pevu ? what is critical thinking? Siku hizi mambo ni rahisi tu ya nini uumize akili yako, njia ya kwanza fungua browser yako ingia google itakupa jibu la hilo swali. Sasa naamini unaona tatizo la kutokufikiri lilivyo, hali hii imetuathiri sote.Tuna changamoto ya kutokufikiri !
Hatutaki kujichosha hivyo hatufikiri sana, mpaka pale ambapo utabanwa kisawa sawa. Njia ya pili siku hizi mawasiliano ni rahisi unamuuliza mtu mwingine akusaidie jibu. Sasa haimaanishi kuwauliza wengine ni vibaya au ku google upate jibu ni vibaya. Google itakupa majibu ya kitaalamu ila itakunyima fursa ya kufikiri mwenyewe.
Je tusi google au kuwauliza wengine ? La hasha bali yale tutakayoyapata kutoka mtandaoni inafaa yapimwe na kufikiriwa si kwamba kwa sababu expert fulani ametoa maoni yake basi huo ndio msimamo pekee kuhusu hilo jambo. Kila mtu yuko huru kupokea taarifa, kuzichambua na kutengenezea msimamo wake binafsi kuhusu jambo fulani.
Muda mrefu kidogo nilisoma kitabu cha Harvey Segler “Critical thinking Powerful strategies that will make you improve decision making and thinking smarter” yeye ame define critical thinking kama ifuatavyo ;-
Critical thinking” is defined as: The objective analysis and evaluation of an issue in order to form a judgement.
Kwenye hiyo maana kitu kilichonivutia kuhusu fikra pevu ni sentensi ya mwisho inayosema …..in order to form a JUDGEMENT. Sasa tufikiri pamoja judgement ni nini? Kwa sababu kuchambua na kutathmini kunafanyika ili kutengeneza judgement. Judgement inahusisha kufanya maamuzi, kuwa na maoni juu ya jambo fulani, msimamo au mtazamo.
Unavyo muona mtu kwa nje ni matokeo ya vile alivyo ndani (Law of Relection), ndani ya mtu kuna vitu vingi ila vinavyoongelewa hapa ni akili ( fikra), hisia na nia ( willpower) ambavyo viko kwenye nafsi. Kwahiyo mabadiliko yanaanza ndani ya mtu halafu yanaonekana nje. Ukitaka kubadilika badilika ndani kwanza halafu matokeo ya kubadilika kwako yataonekana nje.Kinachoonekana nje ni matokeo ya kubadilika sio kubadilika kwenyewe.
Tupo jinsi tulivyo kulingana na namna ambavyo kila mmoja wetu anafikiri, kwahiyo suala la KUFIKIRI ni la muhimu sana hasa kama tunahitaji mabadiliko.
ILI UBADILIKE BADILI KWANZA UNAVYOFIKIRI.
Goodluck Edington Moshi.