Nini maana ya elimu bure

Nini maana ya elimu bure

bato

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
3,960
Reaction score
3,474
Elimu bure toka chekeachea hadi F IV ni moja ya ahadi za Mh Rais,Dr John Magufuli. Kipindi hiki cha mwisho wa mwaka shule zinaandikisha wanafunzi wapya kwa ngazi mbalimbali za elimu.
Ndugu yangu amemwandikisha std 1 mtoto wake wa miaka 6,shule ya msingi Kwaang'w,Halmashauri ya Mji,Babati. Huyu mzazi na wazazi wengine wamelipishwa pesa kama sharti muhimu mwanao kuandikishwa.
1: Sh 10,000 dawati
2: Sh 2,000 maji/mwezi
3: sh 2,000 mlinzi/mwezi
Amepewa risiti ya malipo hayo. Waalimu wamewaambi wazazi kuwa haiwezekani bure kiuhalisia,labda kwenye majukwaa ya siasa.
 
Ninavyojua huwa kuna ada na michango ya shule. Wacha tulipe michango maana ni muhimu zaidi kwa shule zetu
 
Jiandae kulipa ada. Hazina itakuwa imekusanya january?
 
maana ya elimu bure yaani kila kitu bwerere hakuna kulipa waliolipa ni kiherehe chao tu, hapa kazi tu.
 
hakuna bure kila kitu mkuu, lazima muichangie serikali pesa ili hata madawati yaliovunjika mashuleni yafanyiwe ukarabati,
 
Elimu gharama na mitoto yenu inatoka na zero ikiwa bure si ndio hata shule patakua magenge tu ya kulelea.
 
In theoretical point of view, bure haipo labda kama muda hauna dhamani. Jaman kama elimu ni ghali jaribu ujinga. Lipeni fedha watoto wasome. Sasa mlinzi au mpishi, maji, umeme na vitu kama hivyo vitalipiwa kwa fungu lipi maana serikali haitoi fedha zakuhudumia hayo ambayo pia nni muhimu sana kwa mustakabali Wa shule husika.
 
Elimu bure toka chekeachea hadi F IV ni moja ya ahadi za Mh Rais,Dr John Magufuli. Kipindi hiki cha mwisho wa mwaka shule zinaandikisha wanafunzi wapya kwa ngazi mbalimbali za elimu.
Ndugu yangu amemwandikisha std 1 mtoto wake wa miaka 6,shule ya msingi Kwaang'w,Halmashauri ya Mji,Babati. Huyu mzazi na wazazi wengine wamelipishwa pesa kama sharti muhimu mwanao kuandikishwa.
1: Sh 10,000 dawati
2: Sh 2,000 maji/mwezi
3: sh 2,000 mlinzi/mwezi
Amepewa risiti ya malipo hayo. Waalimu wamewaambi wazazi kuwa haiwezekani bure kiuhalisia,labda kwenye majukwaa ya siasa.

Watanzania bana!!!!wanasiasa wametulemaza.
 
Namsifu sana huyo mwalimu aliyekupa mpaka risiti. Amekuonesha kuwa, hajakuibia. Tena amekufafanulia, kuna mlinzi, kuna dawati, kuna maji. Vitu hivyo serekali haivitoi na ni vya lazima.
Mbona mwalimu hakuwaitisha chakula cha mchana? Shule gani hamuwapi watoto chakula cha mchana?? Darasa la 1 wanatakiwa uji safi wenye maziwa fresh. Kama alisahau, usishangae akakuambia ongeza shs 20.000/= kabla ya january. Usimwamini mwanasiasa
 
Ninavyojua huwa kuna ada na michango ya shule. Wacha tulipe michango maana ni muhimu zaidi kwa shule zetu

ni kweli mkuu, pia nafikiri ni mapema mno kwa serikali ambayo bado inatumia bajeti ya serikali ya awamu iliyopita, kutekeleza hilo..
 
tatizo tunaleta siasa kwenye elimu km huwez changia elimu we tulia tuu uone mwanao anavododa s/kali haipeleki ela shuleni sasa hao walimu watapata wapi ya kulipa hz huduma mhm? akili kumkichwa
 
Ukijua kuzaa lazima utoe Huduma kwa watoto wako. Elimu tu ya 20 elfu kwa mwaka inakushinda. Hiyo 20 tau ni kama 360?20=18 kwa mwezi. Shs 18 kwa mwezi inakushinda? You can not be serious with life.
 
ni kweli mkuu, pia nafikiri ni mapema mno kwa serikali ambayo bado inatumia bajeti ya serikali ya awamu iliyopita, kutekeleza hilo..

Hii ni serikali ya Daktari wa kemia, ni serikali yenye ubunifu wa ajabu, haitegemei bajeti ya serikali ya awamu iliyopita kwa kila kitu. Mfano pesa iliyonunua vitanda na magodoro Muhimbili, haikutoka kwenye budget, kuna pesa inaokolewa kutokana na sikukuu zisizo na tija, safari zisizo za lazima, n.k.
 
Tuwe wakweli. JPM ameagiza wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi kujipanga kwa ajili ya utekelezaji wa elimu bure. Swali la msingi ni je mbadala wa michango hiyo serikali lazima ionyeshe itatoa wapi fedha hizo.

Shule zetu zilifikia kukosa hadi chaki, ofisi za walimu zenye samani, madawati, gharama za ukarabati wa miundombinu ya shule, nk. Mfano mzuri ni hiyo shule ya Babati ambapo mchango wa maji unaashiria hakuna maji hapo shuleni. Hivyo, kufuta michango kama hiyo maana yake serikali ipeleke maji kufikia January 2016, jambo ambalo ni gumu. Matokeo yake ni yepi? watoto watakosa maji kwa ajili ya kunywa, usafi wa mazingira na uwezekano wa mlipuko wa magonjwa.

Nilidhani jambo hili lisifanywe kisiasa. Walimu sio wajinga kuwabebesha wazazi michango. Isitoshe kuna mikutano na wazazi ambapo hupewa maelezo ya hali halisi na kuridhia kuchangia.

Pia, ikumbukwe binadamu siku zote anapenda mteremko/unafuu hata katika mambo yake binafsi. Hivyo, inapotokea fursa ya kuhojiwa na vyombo vya habari hulalamika sana juu ya hii michango. Lakini kama justification ya mchango ipo na kiwango cha kuchangia kiliridhiwa na majority sioni tatizo.

Sote tunajua mazingira ya shule zetu na uwezo wa serikali wa kuzihudumia shule hizo. Nadhani wakuu wa shule washirikishwe kikamilifu njia mbadala ya kugharimia mambo mbalimbali.

Back
Top Bottom