Nini maana ya dhana ya kiongozi wa chama cha ACT?

Nini maana ya dhana ya kiongozi wa chama cha ACT?

Mtimbo

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2012
Posts
1,392
Reaction score
797
MOJAWAPO ya matukio ya kisiasa yaliyotawala vyombo vya habari, mazungumzo ya kawaida na mitandao ya kijamii mwezi Machi mwaka huu ni kuzinduliwa rasmi kwa Chama cha ACT-Wazalendo. Uzinduzi wa chama hiki ulifanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam Machi 29, 2015.

Mambo mawili muhimu yametawala mjadala kuhusu kuzinduliwa kwa chama hiki. Jambo la kwanza ni kuhusu itikadi ya chama, ambayo ni ujamaa wa kidemokrasia. Baadhi ya wachambuzi wa mambo ya kisiasa wamehoji uhalali na uhalisia wa chama hiki katika kuhuisha na kutekeleza siasa ya ujamaa katika mazingira ya dunia ya leo ambapo siasa za ubwanyenye zimetawala.

Jambo la pili ni muundo wa uongozi unaotumiwa na chama hiki. Tofauti na utaratibu uliozoeleka katika miundo ya uongozi ya vyama hapa nchini, ACT-Wazalendo kimekuja na muundo wenye Kiongozi wa Chama sambamba na Mwenyekiti wa Chama.

Katika makala ya leo ninajadili na kufafanua kuhusu dhana na msingi wa muundo wa uongozi wa ACT-Wazelendo. Nikipata fursa huko mbele nitajitahidi kufafanua dhana na msingi wa itikadi ya Demokrasia ya ujamaa kama inavyotumiwa na ACT-Wazalendo hasa katika mazingira ya Tanzania ya leo.

Jambo moja jema katika mjadala unaoendelea kuhusu ACT-Wazalendo ni kwamba angalau tumeanza kujadili kuhusu itikadi na mifumo ya uendeshaji wa vyama vya siasa, badala ya kila siku kujadili matukio ya kisiasa yanayotokea.

Mfumo wa uongozi wa ACT-Wazalendo unajumuisha Kiongozi wa Chama sambamba na Mwenyekiti wa Chama. Kimsingi huu ndio mfumo wa uongozi unaotumiwa na vyama vya siasa katika nchi nyingi zilizomo katika Jumuiya ya Madola.

Kwa mfano, nchini Uingereza mfumo wa uongozi wa chama cha Conservatives unajumuisha Kiongozi wa Chama na Wenyeviti wawili. Kiongozi wa Chama cha Conservatives ni Waziri Mkuu wa sasa David Cameron wakati Grant Shapps na Lord Feldman ni wenyeviti wa chama hicho. Kiongozi wa Chama cha Liberal Democrats ni Nick Clegg wakati mwenyekiti wa chama (wanamuita Rais) ni Sal Brinton.

Mifano pia ipo mingi katika Bara la Afrika. Kwa mfano, Raila Odinga ni Kiongozi wa ODM nchini Kenya wakati Mwenyekiti wa Chama hicho ni Henry Kosgey. Nchini Afrika Kusini, Kiongozi wa Chama tawala cha ANC ni Jacob Zuma wakati Mwenyekiti wa chama hicho ni mwana mama Baleka Mbete, ambaye pia ni Spika wa Bunge la Afrika Kusini.

Sababu ya msingi ya kuwa na mfumo wa uongozi wa chama tofauti na mwenyekiti ni kuepuka kutengeneza chama dola. Moja ya matatizo yanayoikumba demokrasia barani Afrika ni ukweli kwamba mfumo wa uongozi wa vyama vya siasa ni wa kidola.

Hapa kwetu, kwa mfano, CCM ni chama dola kwa maana kwamba kimejipenyeza serikalini kutokana na muundo wake ambapo mwenyekiti wake ndiyo huyohuyo anakuwa kiongozi wa serikali. Huyu akimaliza kuendesha vikao vya Baraza la Mawaziri anahamia kuendesha vikao vya chama. Ni kwa sababu hii chama kinakuwa hakina uwezo wala mamlaka ya kuhoji utendaji wa serikali yake.

Matokeo ya muundo huo ndio yanayomfanya sasa Katibu Mkuu wa CCM kufanya kazi ya vyama vya upinzani ya kulalamika na kuikemea serikali yake barabarani kwa sababu anajua kwamba hawezi kuwa na nafasi hiyo ndani ya vikao vya chama kwa sababu huko serikali ndiyo inayoendesha chama.

Mfumo wa chama dola wa CCM hauna tofauti na vyama vingine. Ndiyo kusema vyama hivi navyo vitalazimika kuwa vyama dola mara vitakapoingia madarakani. Mfumo wa chama dola ni hatari kwa demokrasia kwa sababu hulazimisha watumishi wa umma kufanya kazi ya chama tawala badala ya kutumikia serikali kwa mujibu wa taaluma zao.

Kwa hiyo, msingi wa kuwa na mfumo wa uongozi wa chama sambamba na uenyekiti ni kuondoa udola katika chama cha siasa. Mfumo huu unatoa nafasi kwa chama kuweza kuhoji na kusimamia utendaji wa serikali yake bila chenyewe kujigeuza kuwa serikali. Hiki ndicho kilichofanyika Afrika Kusini ambapo baada ya kuona Rais Thabo Mbeki ameshindwa kusimamia sera za ANC katika serikali chama kiliamua kumuweka pembeni na hatimaye kumchagua Jacob Zuma kuwa Kiongozi wa Chama na baadaye Rais wa Afrika Kusini. Jambo hili lisingewezekana katika mfumo wa chama dola.

Kwa hiyo msingi wa ACT-Wazalendo kuwa na mfumo wa Kiongozi wa Chama sambamba na Mwenyekiti ni kugawanya majukumu ya kuendesha mfumo wa chama na kueneza itikadi na sera za chama kwa umma. Kwa mujibu wa Katiba ya ACT-Wazalendo, jukumu la msingi la Kiongozi wa Chama nje ya serikali ni kueneza itikadi, falsafa, misingi na sera za chama kwa umma. Ndiyo kusema kazi kubwa ya Kiongozi wa Chama itakuwa ni kuongoza jahazi la kuzunguka nchini katika kusaka kuungwa mkono na wananchi.

Jukumu la msingi la Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo ni kusimamia uendeshaji wa chama na taasisi zake. Yeye ndiye atakuwa mwenyekiti wa vikao vyote vya maamuzi ndani ya chama ikiwemo Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu.

Siku ACT-Wazalendo ikichaguliwa na kuunda serikali jukumu la Kiongozi wa Chama litakuwa ni kusimamia uendeshaji wa serikali na kuhakikisha kwamba serikali inatekeleza sera za chama kikamilifu na atatoa taarifa ya utekelezaji wa sera katika vikao vya chama vitakavyoendeshwa na Mwenyekiti wa chama.

Mgawanyo wa majukumu ya Kiongozi Mkuu na Mwenyekiti wa Chama yanajitokeza pia katika mamlaka za uteuzi. Kwa mfano, Kiongozi Mkuu wa Chama ana mamlaka ya kupendekeza uteuzi wa wenyeviti wa kamati za kisera na washauri wa chama. Mwenyekiti kwa upande wake ana mamlaka ya kupendekeza uteuzi wa watendaji wa chama kama vile manaibu katibu wakuu.

Kwa hiyo, pamoja na kwamba kimuundo Kiongozi wa Chama ndiye mwenye mamlaka zaidi ya kiuongozi ndani ya ACT-Wazalendo, mgawanyo wa nafasi mbili za Kiongozi wa Chama na Mwenyekiti ni wa kimajukumu zaidi kuliko kimamlaka.

Tunaamini kwamba kwa kuwa na mfumo wa uongozi huu ni hatua muhimu ya kujenga chama cha siasa kisicho chama dola. Aidha mfumo huu utahakikisha kwamba Mwenyekiti wa chama anakuwa na nafasi ya kutosha ya kujenga na kusisimamia uendeshaji wa mifumo ya chama.

Chanzo:Raia mwema
 
Hadithi tu hizi za kuhalalisha u Ayatollar!
 
Kwa mujibu wa Katiba ya ACT ZZK atakuwa na madaraka yafuatato

"Kazi za Kiongozi Mkuu wa ACT-Tanzania

i) Atakuwa kiongozi mkuu wa chama kwenye mikutano mikuu ya chama Taifa, mkutano mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu.

ii) Atakuwa mkuu wa siasa, mshauri na mwelekezaji kwa viongozi wote na maafisa wa ACT-Tanzania

iii) Kuteua wajumbe watano wa Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba hii

iv) Atakuwa ndiye mtoa tamko rasmi kuhusu masuala ya sera na mtazamo wa chama

v) Atakuwa mtoa habari mahususi kwenye mkutano mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu kuhusu hali ya kisiasa nchini na masuala mengine ya kitaifa na kimataifa.

vi) Atasimamia, kufunza na kutoa maelekezo kuhusu shughuli zote za ACT-Tanzania

vii) Iwapo kiongozi wa ACT-Tanzania hayupo kwa sababu yoyote ile basi Mwenyekiti wa chama Taifa atakuwa Kaimu kiongozi mkuu wa Chama.

viii) Iwapo kiti cha kiongozi mkuu wa Chama kitakuwa wazi kwa sababu ya kujiuzulu, kuondoka katika Chama, kuvuliwa uongozi au uanachama, maradhi yenye kuondoa uwezo wa kufanya kazi au kifo, utaratibu ulioelezwa katika

(vi) ya ibara ndogo hii utatumika kwa sharti kwamba Mkutano Mkuu Maalumu wa Taifa utaitishwa katika muda usiozidi miezi sita tangu kuwa wazi kwa kiti hicho kwa ajili ya kuchagua Kiongozi Mkuu wa Chama mwingine.

ix) Ataweza kuondolewa kwenye madaraka baada ya mapendekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa azimio la Mkutano Mkuu wa Taifa
litakaloungwa mkono na theluthi mbili ya kura za wajumbe halali waliohudhuria na kupiga kura.

x) Atakuwa ni nuru na taswira ya ACT-Tanzania"

Kulingana na Katiba ya ACT hayo ndio majukumu ya kiongozi wa chama..

Nilichokipata kwenye hii 'paper'ya mkumbo ni kuwa Mwenyekiti Role yake kubwa ni kuendesha vikao vya chama, na kusimamia utendaji wa chama wakati Kiongozi wa Chama akiwa barabarani anaeneza sera.

Sasa swali la kwanza, KATIBU Mkuu (Kama yupo), atafanya kazi gani??.

Pili, kuhusu mgongano wa kimajukumu,mbona majukumu mengi ya kiongozi mkuu (see for eg ii,vi) katika katiba ya ACT yanaonekana ni ya kiutendaji zaidi tofauti na mkumbo anayetuaminisha kuwa kiongozi mkuu anapaswa kuwa barabarani kueneza sera/ serikalini akisimamia utekelezaji wa sera??. Yanatofautishwaje na ya Mwenyeketi,Katibu Mkuu??.
 
Prof Kitila naomba nikusahihishe kidgo kuwa Mwenyekiti wa ODM anaitwa John Mbadi, Kosgey ameshaachia
 
Bandugu msaada tafadhali, hivi vyama vilivyotolewa mfano kuna cha mfumo wa kijamaa? Moja.

Mbili katika mfumo huu, mtu anaepukaje kuitaja iran kama mfano? Unafiki.

Tatu zama hizi ya wezekana kumeibuka maprofu ubwabwa. Huyu aweza kuwa kati yao.
 
.....hivi vyama vilivyotolewa mfano kuna cha mfumo wa kijamaa?

Swali zuri sana, katika Dunia hii ambayo Ujamaa hauwezekani kiutendaji, nawaona ACT kama walaghai wa maneno matamu kwa wananchi wakati wakijua haiwezekani.

Pili, Ujamaa umeshindwa kupatikana katika tangazo la kwanza kabisa la mali za Kiongozi Mkuu Zitto. Mjamaa huwezi kujimilikisha maeneo chungu mzima katika sehemu tofauti nchini tena sehemu nyeti ikiwemo kitalu cha gesi MTWARA. Kwa maoni yangu hiyo ni failure at first step.
 
Swali zuri sana, katika Dunia hii ambayo Ujamaa hauwezekani kiutendaji, nawaona ACT kama walaghai wa maneno matamu kwa wananchi wakati wakijua haiwezekani.

Pili, Ujamaa umeshindwa kupatikana katika tangazo la kwanza kabisa la mali za Kiongozi Mkuu Zitto. Mjamaa huwezi kujimilikisha maeneo chungu mzima katika sehemu tofauti nchini tena sehemu nyeti ikiwemo kitalu cha gesi MTWARA. Kwa maoni yangu hiyo ni failure at first step.

ndio maana mmeambiwa n ujamaa wa kidemokrasia xaxa mnataka ZZK asimiliki kitu? wapuuz nyie nn maana ya demokrasia? chama kinakubaluana na demokrasia isiyoruhusu unyonyaji mfano unaofanywa na slaa mkutano mmoja analipwa 1M hiyo n demokrasia nyonyaj elewen. ujamaa hauruhusu lujilimbikizia mali na pia kuonesha namna mal ulivozpata
 
ndio maana mmeambiwa n ujamaa wa kidemokrasia xaxa mnataka ZZK asimiliki kitu? wapuuz nyie nn maana ya demokrasia? chama kinakubaluana na demokrasia isiyoruhusu unyonyaji mfano unaofanywa na slaa mkutano mmoja analipwa 1M hiyo n demokrasia nyonyaj elewen. ujamaa hauruhusu lujilimbikizia mali na pia kuonesha namna mal ulivozpata


Usipanic mkuu, kushout hakuwezi kufanya hoja isikike.

Kuhusu malipo ya 1M ya Slaa, I can not comment kwa sbb sina evidence ambayo hata ww nikikwambia unipe hapa utakimbia. Moreover mimi siyo mtu wa kuchota maneno ya barabarani.

Back to topic, umesema demokrasia isiyoruhusu unyonyaji..kujimilikisha maeneo lukuki katika maeneo mbali mbali ambako nako kuna wananchi ambao wanalalamikia umilikishwaji mbovu wa maeneo hayo siyo unyonyaji??. Definition ya unyonyaji kwako ni ipi?.
 
Bandugu msaada tafadhali, hivi vyama vilivyotolewa mfano kuna cha mfumo wa kijamaa? Moja.

Mbili katika mfumo huu, mtu anaepukaje kuitaja iran kama mfano? Unafiki.

Tatu zama hizi ya wezekana kumeibuka maprofu ubwabwa. Huyu aweza kuwa kati yao.

Mfumo unachagulia na chama husika na wala sio kuiga
Act inamfumo wa kijamaa
 
Usipanic mkuu, kushout hakuwezi kufanya hoja isikike.

Kuhusu malipo ya 1M ya Slaa, I can not comment kwa sbb sina evidence ambayo hata ww nikikwambia unipe hapa utakimbia. Moreover mimi siyo mtu wa kuchota maneno ya barabarani.

Back to topic, umesema demokrasia isiyoruhusu unyonyaji..kujimilikisha maeneo lukuki katika maeneo mbali mbali ambako nako kuna wananchi ambao wanalalamikia umilikishwaji mbovu wa maeneo hayo siyo unyonyaji??. Definition ya unyonyaji kwako ni ipi?.

Hii mada nzuri sana vyama vyote tajwa vyote vinatumia mifumo ya ubepari.....lkn hawa ndg zetu ni wajamaa na bado wamejilbikizia mali na kuacha wanyonge ktk dimbwi la umaskini....nakumbuka mwl kj baada ya azimio la arusha mwka 1967 kilichofaata ilikuwa ni hujumu uchumi (punguza) lengo kuu ni kutoa matabaka kt ya maskin na matajil...

Tulidi kwenye hoja.ndg.zzk kataja mali zake lkn cjaona alipo taja vywanzo vya hizo mali..na haja sema nilini ataanza kupunguza mali zake kwa ajili ya kutekeleza sera ya ujamaaa...


Ni unaovyo mm kutoka jija maswa.
 
I repeat Nobody need to apologize for being rich...Go Zitto, Go Prof.Kitila...Former DARUSO President!
 
I repeat Nobody need to apologize for being rich...Go Zitto, Go Prof.Kitila...Former DARUSO President!


Sawa Mjamaa unayefuata Unyerereism...!! Natamani Nyerere afufuke awaone haya mnayoyafanya..!!
 
China bado ni wakomunisti lakini Mabillionea wengi duniani sasa ni Wachina...Miaka ya 80's Mwalimu baada ya kutembelea china alisema sisi tunaweza kama wachina...sasa hatuwezi tena kwani tunategemea wachina hadi mayai ya kuku! Tunahitaji uongozi ambao hautajali utajiri wa watu na kuhimiza wawekezaji wazalendo..GO ACT-WAZALENDO
 
Back
Top Bottom