nini maana ya adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie?

CharmingLady

JF-Expert Member
Apr 16, 2012
18,250
12,868
heshima mbele wanaMMU, Huwa nasikia huu msemo kuwa adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie, naomba ufafanuzi
 
heshima mbele wanaMMU, Huwa nasikia huu msemo kuwa adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie, naomba ufafanuzi

Nafikiri ni kwa sababu matukio mengi huonyesha wanawake baadhi hutendwa na wanawake wenzao! Mfano: Kuibiana wanaume, Ugomvi wa mawifi, kupeana ushauri mbaya wa kumgombanisha mwanamke na mumewe, kubaniana kwenye kazi (bosi wa kike kumbania mwanamke mwenzake), wivu, tamaa, nk.
Lakini ngoja niache nafasi kwa wataalam waamke kuja kuchangia ....
 
HorsePower kwani hakuna wanaume wanaotembea na wake za rafiki zao? kwan mwanaume hawezi kuwa na hizo tabia?
 
Last edited by a moderator:
CL,
ni kweli..... Mfano mdogo angalia mashosti wanavyovurugana....
Ikija kwenye biashara /kazi wanawake hawasaidiani kivile....hupenda kuharibiana...

Majungu na umbea walaahhhhh wanaweza kukuharibia hivi hivi....

Nimetoaa mifano michache nimechoka kutype
 
CL,
ni kweli..... Mfano mdogo angalia mashosti wanavyovurugana....
Ikija kwenye biashara /kazi wanawake hawasaidiani kivile....hupenda kuharibiana...

Majunhu na umbea walaahhhhh wanaweza kukuharinia hivi hivi....

Nimetoaa mifano michache nimechoka kutype

ok, nimekupata BT lakini mbona hata wanaume wengne wana tabia kama hzo?
 
Mara nyingi,wanawake huwa hawa-appreciate each other,na utakuta mwingine akimsifia mwenzie lazima amuwekee neno 'lakini.. yaan mpaka amuwekee kasoro ndo anaridhika.
 
Dah!Kwa kweli hata sijui ni kwanini,hebu ngoja nitege sikio . . . . . . . . .!!
 
HP na BT wamesema mengi, wanawake wana kinyongo (grudge) cha muda mrefu na mnaweza kulipiza kisasi kwa kosa mlilofanyiwa miaka iliyopita. hii inaudhii. pia badala ya kuongeza bidii ili umzidi mwenzio wewe unam-sabotage ili ashuke na kuwa level yako as a result hamuendelei.
 
Nafikiri ni kwa sababu matukio mengi huonyesha wanawake baadhi hutendwa na wanawake wenzao! Mfano: Kuibiana wanaume, Ugomvi wa mawifi, kupeana ushauri mbaya wa kumgombanisha mwanamke na mumewe, kubaniana kwenye kazi (bosi wa kike kumbania mwanamke mwenzake), wivu, tamaa, nk.
Lakini ngoja niache nafasi kwa wataalam waamke kuja kuchangia ....

La kuibiana wanaume, mtendaji hapo ni mwanaume na si mwanamke mwenzangu!

Mimi boss wangu ni mwanaume na anabana kishenzi.

Mimi nafikiri hiyo propaganda inaendekezwa na wanaume ili wanawake wachukiane wao kwa wao. Na kusema kweli imework sana, na yote hiyo ni kwa manufaa ya wanaume!

Wewe chukulia una wake wawili, halafu kila unapoenda unamsema mmoja vibaya kwa mwenzie unategemea nini? Au hata kama usipomsema lakini kitendo cha wewe kuwa na wanawake wawili unatengeneza ushindani na chuki kati yao!

Adui wa mwanamke ni mwanaume, this is my stand; kama tunaweza generalize like that!
 
Back
Top Bottom