Nini kitatokea kama wezi wa Escrow account hawatowajibishwa?

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,218
11,283
Haya ndo yatakayo enda ikiwa wabunge hawato waajibisha wezi wa escrow?
1. Uzalendo na upendo wa wananchi kwa serikali yao utashuka jambo ambalo litakuwa ni hatari kwa usalama wa taifa
2. Kwa kuwa bunge ndio lilikuwa tumaini lao la mwisho basi nidhahiri shahiri watalichukia bunge na kumchukia spika wa Bunge
3. Mataifa yanayo tufadhili pamoja na umoja wa mataifa wataenda kuzuwia misaada jambo litakalo fanya taifa kukopa na kufanya serikali kuwa na mzigo mkubwa wa madeni
4. Kwa kuwa taasisi ya Rais imetajwa ina maana umoja wa nchi zilizoendela watakuwa hawana imani na serikali yake
5. Chama tawala kinaweza kwenda kusambaratika kwa kuwa viongozi wake wakubwa wameshiriki ktk wizi huu na hakuna hatuwa zozote za kisheria zimechukuliwa kwao ivyo wale walio wajibika tangu mwanzo wanaenda kuungana ili kupambana na wale walio lindwa hapa ni vigumu cc kuwa wamoja na ndipo pale Mkapa atakumbukwa wosia wake pindi akimaliza Muda wake
6. Mh Makianda anaenda kuwa spika wa kwanza ambae uwenda akapigiwa kura yakuto kuwa na imani nae maana kuna watu wataleta hoja maalumu kumuhusisha kiti chake na uwamuzi alio ufanya ambao umeipendelaa serikali na cc.
7. Kamati ya bunge itakuwa ilio tumwa itakuwa ni pini ambayo itawatesa wabunge kiasi hata kumuangusha Mh Makinda maana vipo vifungu vita wabana.
8. Nchi imetikisika na mwisho wake ni kuanguka maana sasa watu wamepewa nafasi yakutumia vibaya pesa za serikali hii ni hatari
9. Sekta ya kifedha itachafuka jambo linaloweza kuwekewa vikwazo na nchi za ulaya na Amerika
 
Wananchi nchini kote waambiwe marufuku kutoa mchango wowote kwa serikali tukianza na hii ya maabara kwani serikali inakusanya kodi, na kodi inayokusanywa ndiyo hiyo inayogawanwa kama sadaka.
 
Wananchi nchini kote waambiwe marufuku kutoa mchango wowote kwa serikali tukianza na hii ya maabara kwani serikali inakusanya kodi, na kodi inayokusanywa ndiyo hiyo inayogawanwa kama sadaka.


Hii sawa kabsa...jambo la mwsho wabubge wanapaswa kufanya km watuhumiwa wacpo tekeleza ni kupiga kura ya kutokua na iman na wazir mkuu ata rais pia
 
Imekuwa faida kubwa kwa watanzania kujua kuwa baadhi ya wabunge wa viti maalumu ni makuwadi wa mafisadi.
imesaidia kujua kuwa Anna Makinda ni mtetezi wa mafisadi;
Imesaidia kujua kuwa baadhi ya wabunge wa CCM wana uchungu na nchi yao. ....
 
Hii sawa kabsa...jambo la mwsho wabubge wanapaswa kufanya km watuhumiwa wacpo tekeleza ni kupiga kura ya kutokua na iman na wazir mkuu ata rais pia
Sasa hata kama kwa Maswi inakuwa ngumu kuwajibishwa, kwa waziri mkuu ndiyo itawezekana kwa bunge hili? Ccm wameunda solidarity katika kuitafuna nchi. Wasipoteze muda na posho, warudi tu majimboni.
 
Back
Top Bottom