Kukuwazabanga
Member
- Jan 12, 2017
- 19
- 178
Wabunge wajitathmini tuliwachagua sisi....na tutawaondoa sisi.....
Mwenye kiti wa Kamati ya Maadili ya Bunge amewaambia waandishi kuwa wao wamemhoji Makonda kwa agizo la Spika. Hivyo Spika alikubaliana na maazimio ya kikao cha bunge.
Azimio hili likipitishwa Mkiti Mtu alikuwa Chenge. Chenge ambaye wote tunamkumbuka kwa kashfa ya Rada na mikataba mibovu ya madini. Almaarufu mzee wa vijisenti.
Lakini tujiulize kulikoni? Yaani Spika na Kamati na wabunge waliotaka Makonda ahojiwe kwa kuwa tu kasema wanasinzia bungeni!!! Hapana hili ni jibu jepesi sana.
Wabunge hawakuona umuhimu wa kumhoji aliyedai mkuu wa nchi atakufa? Anayetoa maneno ya uhaini anabaki salama. Lakini anayesema wabunge wanalala bungeni anahojiwa. Hili ndilo bunge letu. Wabunge hawa wa CCM hawajahoji wabunge wenzao wanaodai naibu spika hafai!!! Bunge halikuona umuhimu wa kumhoji Spika aliposema kuna baadhi ya wabunge wanaovuta bange!!! Hivi anayekwambia unasinzia na anayekwambia hufai au unavuta bangi nani kakuvunjia heshima zaidi????
Hivi Makonda kadanganya? Wabunge ni kweli wanasinzia!!! Na picha na video za wao wakiwa wansuchapa usingizi bungeni zipo!
Lakini bunge na Spika wetu wameona la kusinzia ambalo ushahidi upo ndio kudharau bunge! Nadhani "mshtakiwa" ana kazi nyepesi mno kuthibitisha wabunge huwa wanasinzia!!!
Nimkumbushe tu mmoja wa wabunge alipouchapa usingizi wa pono aliulizwa na alijibu eti alikuwa anatafakari!!
Naamini kwa dhati kabisa nyuma ya juhudi hizi za bunge letu kutembelea Clouds na kumhoji aliyesema ukweli kuwa huwa wanasinzia bungeni kuna nguvu za giza. Zisiachwe zikashinda maana taifa litaangamia. Na wapiga kura haswa ndani ya CCM nadhani mnawaona wasaliti wa Taifa! Tuwasubiri 2020 tuwaadabishe!
Mwisho niwaulize wasomaji wote Makonda alikuwa kipenzi cha wabunge wa CCM sana. Mbona mapenzi yamekufa baada ya yeye kuanzisha vita dhidi ya madawa ya kulevya?
Swali la pili upinzani ulimkataa peupe Naibu Spika Tulia wa CCM. Bunge likagawanyika kwa hoja hiyo? Iweje hoja ya mtu anayepambana na madawa ya kulevya iwalete wabunge hawa pamoja???? NINI KINAWALETA PAMOJA???