Nini kinamuandama Dk. Mwakyembe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini kinamuandama Dk. Mwakyembe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Nov 23, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe yuko nchini India anakopatiwa matibabu ya afya yake. Amelazwa kwenye hospitali maarufu nchini India ya Indraprastha Apollo iliyoko mjini Chinai.Kwa mujibu wa taarifa kutoka ubalozi wa Tanzania jijini New Delhi na ndani ya hospitali hiyo, tayari madaktari wa Dk. Mwakyembe wamechukua vipimo mbalimbali kwa lengo la kufahamu kinachomsibu.Hadi

  gazeti linakwenda mitamboni juzi Jumatatu, madaktari nchini India bado walikuwa wanaendelea kuchunguza afya yake.
  Naye balozi wa Tanzania nchini India, John Kijazi ameeleza MwanaHALISI, “Dk. Mwakyembe amefika salama Chinai; madaktari wanaendelea na uchunguzi wao.” Aligoma kutaja kinachomsumbua mwanasiasa huyo kwa maelezo kwamba hajapata ripoti kamili ya daktari wake.Naye

  daktari anayemhudumia Dk. Mwakyembe amesema, “…Bado tunaendelea na uchunguzi.”
  Alipong’ng’anizwa kueleza angalau kwa ufupi kinachomsibu Dk. Mwakyembe, haraka alisema, “…Kimaadili hatuwezi kukueleza taarifa za mgonjwa wetu. Elewa tu kwamba vipimo vyake vinafanyiwa uchunguzi,” alisema kwa sharti la kutotajwa gazetini.Wakati hayo yakitendeka nchini India, hapa nyumbani kumezuka

  mjadala kuhusu hasa kitu gani kinachomuandama Dk. Mwakyembe.
  Kabla ya kuondoka nchini, mke wa Dk. Mwakyembe, Linah Mwakyembe alinukuliwa akisema, “…Tatizo la mwili kuvimba, lilianza miezi mitatu iliyopita. Linakuja na kupotea. Lakini sasa naona kama hali inazidi kuwa mbaya.” Dk. Mwakyembe ameondoka nchini akiwa amevimba mwili mzima.Mwanasiasa huyo aliyejipatia umaarufu

  mkubwa wakati alipoteuliwa kuongoza Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba tata wa kufua umeme kati ya serikali na kampuni ya kitapeli ya Richmond, hajawahi kulalamika kuumwa isipokuwa amewahi kuripoti hofu ya usalama wake.
  Tangu kusomwa bungeni ripoti ya Richmond, Februari 2008, Dk. Mwakyembe amekuwa akidai kufuatwafuatwa ikiwemo mbinu za kutaka kumuua kwa njia

  mbalimbali.
  Tarehe 9 Februari 2011, Dk. Mwakyembe aliandika barua ya kurasa saba kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema akisema kuna genge la watu limepanga njama za kumuua.Katika barua hiyo, aliyoipa kichwa cha habari, “Taarifa ya njama za kuondoa maisha yangu na ombi kwa jeshi la polisi kulinda haki yangu ya kikatiba ya kuishi,” Dk. Mwakyembe alitaja watu wengine saba kuwamo

  katika orodha ya wanaotakiwa kuuawa.
  Waliotajwa na Mwakyembe kwamba wako mbioni kuuawa, ni pamoja na katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, mfanyabiashara mashuhuri nchini, Reginald Mengi, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe na mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Melecela.Kwa karibu miezi mitatu sasa, Profesa Mwandosya amekuwa akikabiliwa na tatizo la uti wa mgongo na

  anaendelea kutibiwa nchini India. Akiwa huko, amevumishiwa kifo mara mbili.
  Kuhusu malalamiko yake kwa IGP Mwema, Dk. Mwakyembe anasema, “Pamoja na kwamba taarifa hii ni mpya yenye matukio ya takribani mwezi mmoja tu (wakati huo), naamini kwa dhati kuwa msingi wake – kwa maana ya wahusika na maudhui –hautofautiani na ule wa matukio mengine ya awali ambayo baadhi yake

  yalisharipotiwa polisi na vyombo vingine vya usalama kwa lengo la kuchunguzwa.”
  Anasema pamoja na hayo, bado ana imani kubwa na jeshi la polisi kuwa litaifanyia kazi taarifa hiyo bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa.Msingi mkuu wa yeye kuamua kuviarifu vyombo vya dola, anasema Dk. Mwakyembe, ni taarifa alizozipata kutoka Songea, 22 Januari mwaka huu kuhusu kundi la watu

  saba lililoingia mjini Songea usiku wa 21 Januari kwa gari linalodaiwa kuwa ni la wizara yake.
  Gari hilo aina ya Land Cruiser lilikuwa na namba za usajili STK 6868, lakini baadaye namba ilibadilishwa na kusomeka STK 6869.Pamoja na kuthibitisha kupata barua ya malalamiko ya Dk. Mwakyembe, IGP Mwema alisema ilikuwa wanafanyia kazi malalamiko hayo. Hakutoa taarifa zaidi bali alielekeza aulizwe Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai wa Polisi (DCI), Kamishna Robert Manumba kwa maelezo zaidi.Hofu ya Dk. Mwakyembe kutishiwa

  maisha yake, ilikuja chini ya miaka miwili tangu apate ajali ya gari iliyomtikisa taya lake ingawa hali yake iliimarika.
  Ajali hiyo ilitokea eneo la Ihemi, mkoani Iringa akiwa kwenye gari lake aina ya Toyota Lancruiser, Na. T 362 ACH. Alikuwa akitokea Mbeya kuja Dar es Salaam. Yeye alipata mshtuko wa shingo, huku dereva wake, Joseph Msuya, akipata michubuko mwilini.Ajali hiyo ilizusha lawama nyingi kwa jeshi

  la Polisi baada ya kuwatuhumu kwa uzembe trafiki wawili waliokuwa wamepita eneo la tukio huku Dk. Mwakyembe akiwa hajasaidiwa.
  Mmoja wa trafiki hao alilalamikiwa kuwa alivunja moyo wasamaria waliotaka kutoa msaada kwa kuwaambia, “Msaidieni huyo dereva kwani Dk. Mwakyembe ameshafariki.”Tuhuma hizo zilipata nguvu pale kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Advocate Nyombi

  alipovieleza vyombo vya habari kuwa ajali hiyo ilitokana na “uzembe wa dereva” wa Dk. Mwakyembe.
  Kamanda Nyombi alisema gari la Dk. Mwakyembe lilianguka kwasababu ya mwendo wa kasi uliomfanya ashindwe kumudu usukani baada ya kupitwa kwa ghafla.Maelezo hayo yamepingwa na Dk. Mwakyembe akisema kuwa yalitokana na taarifa zisizokuwa sahihi na ambazo hazikuzingatia hali halisi ya tukio la ajali lilivyotokea.Polisi wa Usalama Barabarani hawakusimamisha na kutambua lori hilo ambalo Dk. Mwakyembe na dereva wake walisema ndilo

  lililosababisha ajali. Walituhumu polisi kwa kutoa taarifa wakati hata uchunguzi wa kina haujafanywa.
  Polisi hawakusema kama walilinasa lori hilo au iwapo walimhoji dereva wake kama sehemu ya uchunguzi.Mwenyewe Dk. Mwakyembe alimtetea dereva wake akisema kuwa ufundi wa kazi alioonesha uliwanusuru na maafa.Katika kipindi cha maandalizi ya ripoti ya Richmond kuwasilishwa mbele ya mkutano wa

  Bunge, taarifa zinamnukuu Dk. Mwakyembe akisema walikuwapo watu waliotaka kumhonga Sh. 50 milioni ili kuficha ukweli.
  Baadhi ya wajumbe wa kamati, akiwamo Lucas Selelii ambaye wakati huo alikuwa mbunge wa Nzega (CCM), walidai kwamba kilitengwa kitita cha Sh. 10 milioni kwa kila mjumbe ili kuwalainisha.
  Chanzo: Nini kinamuandama Dk. Mwakyembe? | Gazeti la MwanaHalisi
   
 2. s

  sawabho JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Ni ugonjwa. Kwa kuwa madaktari wanamshughulikia katika hospitali inayoaminiwa, tusubiri ripoti yao itaonyesha kama ni ugonjwa wa asili au wa kutengenezwa, hata kama ripoti haitakuwa wazi, itakuja toka kupitia watu walio karibu na Dr. Mwakyembe.
   
 3. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,848
  Likes Received: 465
  Trophy Points: 180
  Endelea Kupigia Mbuzi Gitaa!! Labda Siku Moja ataanza Kucheza!!
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyu anaumwa ugonjwa unaitwa upupu wa milele kwa kitaalamu
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Nov 23, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Akome chukua vitambaa vya watu mezani.
   
 6. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ama kweli huu ni uhuru wa kutoa maoni.
   
 7. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180

  Kha? kumbukeni Mungu yupo!
   
 8. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  bado wanafanya uchunguzi
   
 9. m

  mmemkwa Member

  #9
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo hatuna ujasiri wa kujitangaza jamaa amedevelop Kaposi's sarcoma ambayo ni aina ya cancer ya ngozi inayo ambatana na Ukimwi ambao anao kwa muda sasa. Mnazunguka zunguka tu kwani ni wangapi umewaona wanapata hadi fungus za ajabu shauri ya ngoma. Ndio maana hata Muhimbili hawajasema kitu, kama tungeruhusiwa tungeweka full blood screen za jamaa hapa. Babu wa loliondo alisema viongozi wameoza
   
 10. m

  mkweli1961 Senior Member

  #10
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Wewe in Daktari au mganga wa kienyeji
   
 11. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #11
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Unamuuliza nani? mi nadhani hilo swali ungelipeleka moja kwa moja kwa usalama wa Taifa
   
 12. m

  mperwa Member

  #12
  Nov 23, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni kweli maana ulimuambikiza wewe.
   
 13. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #13
  Nov 23, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kweli ukistaajabu ya Musa................
   
 14. k

  kiloni JF-Expert Member

  #14
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kweli wewe MMEMKWA wa magamba!! unaweza kutoa justification za kishenzi hadi muwamalize siyo!!
   
 15. M

  Mr. Clean Senior Member

  #15
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 195
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35


  Nakumbuka miaka ile mchapakazi Kijazi alikuwa katibu mkuu wizara ya miundombinu, akaamua kuachia ngazi baada ya kupishana speed na mramba! jk akampatia ubalozi... sasa ndo anacare naibu waziri wa wizara hiyo huko India!

  BTW tulihabarishwa mwandosya na mwakyembe wangerudi nchini wiki hii, wakiwa tele na afya zao...si alikwenda huko mpambanaji mwenzie samweli sita kumpa pale, ingawa alikimbia kupitisha mswada wa sheria ya katiba....tuwasubirie......!   
 16. k

  kiloni JF-Expert Member

  #16
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kuna &$#@&%it wa magamba bado wanashabikia huu uoza! wanataka kutusadikisha uchafu. IGP mwema ninakuomba uandae jeshi la kuzuia watz milioni 20 waliochoka na mauaji ya kisiasa ambayo wewe unayajua TIK!!TIK!!TIK!!TIK!! peoples power is coming your way!!
   
 17. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #17
  Nov 23, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wewe utakuwa jamaa ya magamba!
   
 18. M

  MWananyati Senior Member

  #18
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kinachomsumbua Mwakyembe, na ambacho kinatakiwa kuwa fundisho kwa wengine wooote, ni kosa la yeye KUFICHA UKWELI. Mfumo umejipanga vyema kuhakikisha kuwa hatapata tena hio nafasi ya kusema ambayo alibakisha.

  Yeye alifikiria kwa kubakisha mengine atakuwa salama. K-intelijensia twasema ni kosa kubwa,hasa kama kilichobaki wahusika wanajua kuwa wajua.
   
Loading...