Nini kimewakumba BvB?

Nini kimewakumba BvB?

Ziroseventytwo

Platinum Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
9,468
Reaction score
17,973
Borussia Dortmund club yenye mafanikio baada ya Bayern Munich. Ikiwa na kocha aliyefanya vizuri miaka mi5 iliyopita. Jurgen Klopp, ameipa BvB ubingwa wa ligi mara mbili mfululizo, FA ya ujerumani, ngao ya hisani ya kijerumani, makamu bingwa wa ucl miaka miwili iliyo pita.

Leo timu imekuwa na matatizo makubwa kiasi hiki? Game 10 alama 7, nafasi ya 17 kwenye ligi ya timu 18? Kuondoka kwa Lewandovsky na Gotze ndio kumepelekea hii timu kuyumba kiasi hiki? Mbona ina world class players na wachezaji wenye quality wengi tu?

Nini kimeisibu hii club jamani?

Tujadili.
 
Katka ligi ya UEFA wanafanya fresh kweli, ila bundesliga ndo majanga.
Maybe timu za bundesliga zimeshazisoma mbinu za Jurgen Klopp, ndo mana wanajipigia tu.
 
Wana majeruhi kuliko timu yoyote ulaya sa hivi ... !
 
Katka ligi ya UEFA wanafanya fresh kweli, ila bundesliga ndo majanga.
Maybe timu za bundesliga zimeshazisoma mbinu za Jurgen Klopp, ndo mana wanajipigia tu.

borussia Dotmond 4 galatasaray 1. Umesema kweli mkuu, ulaya wanaweza, german wanachemsha. Mpaka hapo wamequalifing kwa knock out stage. Game 4 wamepata zote point 12. What happening in bundasliga?
 
borussia Dotmond 4 galatasaray 1. Umesema kweli mkuu, ulaya wanaweza, german wanachemsha. Mpaka hapo wamequalifing kwa knock out stage. Game 4 wamepata zote point 12. What happening in bundasliga?

Hata mi sijaelewa, hii inshu sijui tatizo ni nini? Kuna mdau kasema maybe majeruhi, kama ni hivyo kwanini Uefa wanatoa vipigo vizito? Lakini katika ligi yao wanagongwa na hata vitimu ambavyo vipo katika zone ya kushuka daraja. Kocha anatakiwa awe makini, mana hivi sasa wanashika nafasi ya 17 kati ya timu 18.
 
Naona wameshaona Ujerumani hawana chao, wameamua kuweka nguvu Ligi ya Mabingwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom