Nini kimetokea mpaka kufa kwa uzalishaji wa Ngano hecta 350,000 kule Bassotu Manyara?

Umekumbusha mbali sana. Ni maeneo yaliyokuwa mazuri sana miaka ya mid 80 hadi mwishoni mwa miaka ya 90. Kulichangamka sana kwa biashara, watu toka kila pembe ya nchi n.k.

Ngano iikuwa inalimwa sana, kama sikosei mashamba ya Basuto yaliongoza Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kuna Setcheti, Basuto, Gawali, Murijanda, Gidagamowdi, Mulbadow n.k. Kateshi ilichangamka haswa, hata Mwagitu, Kendabi, Nangwa n.k.

Kuna mameneja/meneja wasaidizi kama Mzee Mndeme, Kimaro, Shetui, Koopa n.k walikuwa wanachapa kazi sana.

Jandu plumbers ndio aliyevuta maji kutoka Kindabi (mlima Hanang) na kuyasambaza kwenye hayo mashamba.

Wengi waliokuwa mameneja na wasaidizi wao walisoma Canada.

Ila wengi walikufa na ukimwi sana. Halafu wengi wao hawakuwekeza , ukikutana nao sasa hivi wamepigika kimaisha na utawaonea huruma. Walipenda sana starehe maeneo ya Arusha, Katesh, Babati na Basuto Central.

Kulikuwa na wanawake wengi sana wazuri kutoka kila pembe ya Tanzania ukijumlisha na dada wa Kiiraq, ilikuwa burudani haswa.

Karibuni Katesh, Kindabi, Mwagitu, Hydom, Masakta, Endasaki, Dareda Centre na Mission, Balang'ida Lalu na Dirima, Milima ya Logia, Gendii, Bonga, Managha, Galapo, Maweni, Maisaka, Murara, Magugu n.k.

Saitaaaaa/Gabaseyuuu.
Hongera Sana kwa uchambuzi wako mzuri. Yaelejea maraha yalizidi na kazi ikawekwa pembeni.
 
Back
Top Bottom